KANUNI ZA WITO

Miracle Revival Fellowship Pentecostal Church Choir 2014

KWA WANA CHOIR MRFPC

Kuimba kanisani ni kazi ya wito kutoka kwa Mungu mwenyewe, si kazi ya kuajiriwa na kutazamia malipo. Hivyo;

  1. kwa anaye tumika:
    • inabariki
    • inainua
    • inalinda
  2. kwa anaye hudumiwa:
    • inajenga
    • inaponya
    • inaokoa
Ni kazi njema haipaswi kufanywa kwa ulegevu; aifanyae kwa ulegevu afanya dhambi (Yeremia 48:10). Aifanyae pia apaswa kuwa kielelezo, matendo yake yakiambatana na nyimbo anazo imba (hatusemi tu watakatifu bali tuna chuchumilia kuifikilia iliyo haki).

Ili kufikilia yote yaliyo katika fungu la kwanza

Inamlazimu mwimbaji yeyote kuzingatia fungu la pili kwa njia ya NIDHAMU. Na haya ndiyo baadhi yayaliyo ya nidhamu tukijua kwamba si ya sheria bali kwa mapatano, maana sheria iliwekewa wasioamini, wasiojua kutenda haki.

  1. kuwaheshimu viongozi kwa kuwa wamepata kibali kutoka kwa Mungu wala si kwa wanadamu.
  2. kufuata kanuni zilizowekwa na viongozi wa choir:
    • a. kutokosa zoezi
    • b. kuzingatia masaa
    • c. kujua nyimbo na miondoko (dancing) ipasavyo
    • d. ukikosa zoezi na ikibidi usiimbe basi uwe mtulivu
  3. kuitambua huduma yako mwenyewe (kabla wengine waitambue) kwa kufanya mawasiliano kila mara unapokuwa na udhuru wa kutokuwepo unapohitajika.
  4. kuwaheshimu na kuwahesabu bora wenzako ukujitolea kwa upendo na kuwatakia wajue unavyojua, usiongozwe ni roho ya kiburi kwa kuwa yote ufanyayo umepewa tu na Mungu, aweza kukuondolea na kumpa mwingine unayemdharau.

Basi ukosefu wa nidhamu huleta ulegevu

Na wafanyao kwa ulegevu wanatenda dhambi (Yeremia 48:10). Ulegevu unaharibu kazi ya Mungu na kukusababishia laana badala ya Baraka, maana utawakosesha watu wa Mungu wanaongojea huduma yako inayotokana na wito wa Mungu. Ni hatari.

Ushauri

1. Kila mmoja afanyapo jambo la kujenga, asijisifu wala kutukuka ndani, bali mpe Mungu utukufu naye atazidi kukuinua, kwa kuwa wewe ni chombo tu katumiwa na Mungu.
2. Pia umekuwa katika shughuli zako wiki yote na Mungu amekupa uwezo wa kufanya mengi katika shughuli zako hizo, mbona usitenge muda mchache tu kwa siku ya mazoezi ukamridhisha Mungu pia.

© 2014