1. Mtakatifu ni Mungu mwenye enzi
Ataka roho zetu ziokoke
Na dhambi tupate uzima
Tuishi mbinguni milele
2. Mtakatifu ni Mungu wa mapenzi
Katoa mwana wake wa pekee
Ili kila amwaminiye awe na uzima milele
3. Mtakatifu Ni Mungu wa wokovu
Ni roho haonekani Kwa macho
Unapo abudu sharti uabudu Kwa roho Na kweli.
1. Hoosana Hosana mbarikiwa ajaye Kwa jina la Bwana x2
Hosana juu mbinguni!
ALL: x2
Yerusalem mji huu umebarikiwa,
Kwa kumtambua yeye,
Ajaye Kwa jina la Bwana.
2. Ewe mwenzangu unaye mbarikiwa ajaye Kwa jina la Bwana x2
Katika maisha yako!
ALL: x3
Unamwitaje yeye, akuongozaye,
Nabii mbarikiwa,
Ajaye Kwa jina la Bwana.
1. Tulijenge Kanisa la Mungu wetu
Tulijenge kwa pendo
Watu wengi wamjue Mungu wetu
(Chorus)
(Jamani) tulijengeni
(Kanisa lake) Mungu muumba
(Tulisimamishe) Tuliimarishe Kanisa lake Mungu
2. Kanisa la Mungu ndilo takatifu
Limejengwa imara
Hakuna chochote kitaliyumbisha
(Chorus)
3. Mwili wako ni kanisa lake Mungu
Heri ujitakase
Matendo yako yaokoe wengine
(Instruments Chorus)
(Chorus)
1. Tazama nimekuja niliondoe la kwanza
Na tena, nilisimamishe la pili
(Chorus)
Ondoeni la kwanza, uovu uliotangulia
La pili uumche Mungu
Ukaupate uzima x2
2. Umeasi Mungu wako piga hatua nyingine
Ya pili, umrudie Mungu wako
(Chorus)
3. Umedumu na uovu hivi leo umkubali
Yesu awe nawe siku zote
(Chorus)
4. Shetani aliweka misingi ya kutomcha
Mungu, Yesu amevunja yote.
(Instruments Chorus)
(Chorus)
Ondoeni la kwanza, uovu uliotangulia
La pili uumche Mungu
Ukaupate uzima x3
1. Tutunze imani imani ya kweli
Imani ile ya utakatifu×2
Imani ile ya kutubu dhambi
Hata kama dhambi ni kubwa sana
Uiungame na kuacha
Usirudie dhambi tena ×2
2. Tuutunze kutoa kutoa kwa kweli
Kutoa Mungu anavyokutuma×2
Kutoa mali kwa kazi ya Mungu
Zaka sadaka pia shukurani.
Ubarikiwe kwa mapato
Ubarikiwe kazi yako ×2
3. Tuutunze umoja umoja wa kweli
Umoja ule wa kukusanyaka×2
Mmoja wetu asijaribiwe
Kufanywa mgumu katika dhambi
Ulete kwake muhubiri
Utaushinda ulimwengu×2
4. Tuutunze kupona, kupona kwa kweli
Kupona kule kwa jina la Yesu×2
Jina la Yesu laweza kuponya
Kwa kujitoa kwake tumepona
Utakasike na upone
Utayarike kwa mbinguni ×3
1. Kiongozi aliyembele, unapaswa kumuheshimu
Akuongozaye kwa imani, na kwa uwezo wa roho ×2
Utiifu ,heshima ,yampasa awaye yote kuyafuata
Ndilo shina la mema, hukumu achia Mungu
2. Aliyembele kuongoza amepata uwezo pia
Na mamlaka kutoka juu ili kwa kazi ya Bwana ×2
Maongozi hutaki Kama unayo haki basi acha kuteta
Mungu yuko atabatilisha usiyopenda
3. Tafakari ulikotoka haya mema hukuyajua
Mungu ndiye amekurehemu sasa fahamu umepata ×2
Malaumu na chuki kiini cha mambo haya ni tama zako
Fundishika mwenzangu tumika ulivyoitwa ×2
1. Unaposikia wito wa Bwana Mungu
Hima hima ukaitike, (usiachwe nyuma kamwe
Fanya kazi yake)x2
(Chorus)
Kazi ni nyingi, mbele za Mungu
Kazifanye kwa bidii sana
Usilegee wala kujuta
Mungu Baba hapendezwi.
2. Kazi zake Mungu nyingi ukazifanye
Bila uoga au hofu, (kwa moyo ukazifanye
Utabarikiwa)x2
3. Mungu akishakuita ajua yote
Unyonge wako ee mwenzangu, (tumika kwake Mwokozi
Bila kuogopa)x2
1. Tushangilie Kanisa la Mungu lilivyoimara
Umoja wetu wadumu milele tena na milele
(Chorus)
Tumsifu baba Mungu Kanisa
Kanisa bado ladumu milele
2. Shetani naye hapendi kanisa la Mungu lidumu
Tuweni macho na hila za huyu baba wa uongo.
3.Kazi ya Mungu aliyoanzisha mtumishi wake
Tuidumishe kwa kumuheshimu kiongozi wetu.
1. Ewe mwenzangu umeshatambua
Pendo la Yesu lilivyo kuu kwako
Katoa uhai wake msalabani
Kwa ajili yako upate okoka. ×2
(Chorus)
Basi sasa ni wakati uonyeshe pendo lako
Kwani yeye alishakupenda na akajitoa ×2
2. Basi hii ndiyo ni siku yako
Achana na anasa za ulimwengu
Na urithi mema yaliyotayari
Pia na uzima ule wa milele×2
(Chorus)
Bwana Yesu ndiye yule jana leo na milele
Aita njoni kwangu wenye mizigo
1. Wokovu kwako ni lazima
Kama vile kufa ni lazima
Kwani hayabadiliki
2. Alisamehe dhambi zao
Hata sasa bado asamehe
Kwani hajabadilika
3. Magonjwa yote aliponya
Pia sasa nawe uamini
Atakuponya kabisa.
1. Baada ya kuumba vitu hivi vyote
Mungu katuumba kwa mfano wake
Katupa uwezo juu ya vyote
Ili turithi mema yote kwake.×2
(Chorus)
Kwanini waviogopa
Wanyama kulia usiku ni kawaida
Naa ndege kulia usiku ni kawaida
Wewe wasema umerogwa
Sivunje safari yako ukimkuta kobe njiani
Sivunje safari yako ukimkuta mbwa njiani×2
2. Mungu yuko katika neno lake
Ukimuamini na atakuponya
Na imani mbaya ulizonazo
Naye atakuweka huru kabisa.
1. Bwana wetu Yesu ni mwema
Yuko tayari kukuponya
Lete na shida zako zote
Yeye ataondoa
(Chorus)
Hakunaa kabisa dawa ya magonjwa
Damu yake Yesu ndiyo inaponya ×2
2. Hivyo ndugu ukiamini
Mungu aweza kukuponya
Atakusamehe na dhambi
Uwe wake daima.
1. Jina la Yesu ndilo lenye uwezo
Laponya labariki linaokoa
(Chorus)
Hakuna jina jingine chini ya mbingu
Hakuna jina jingine juu ya nchi
Yesu ni jina juu ya majina yote
Ni tamu jina lilo nilitajapo.
2. Hata na mashetani wanaogopa
Kwa jina lake Yesu wanatoroka
3. Ni kuu jina hilo lanipa nguvu
Ni kiwa nalo hilo lanishindia
4. Ndilo furaha yangu tumai langu
Nikiwa nalo hilo ni ngao yangu.
1. Yesu ni tabibu wa kweli
Ndiye kimbilio la wote
Anaweza yote yaliyokulemea ×2
(Chorus)
Na Yesu huyo aliyemfariji wetu
Tena mganga kama ukishamuamini
Kimbilio la wanadamu duniani ×2
2. Mimi unaaniona hapa
Yesu ndiye ameniponya
Ni shahidi kwamba yeye ni mponyaji ×2
3. Nawe mbona wafadhaika
Na magonjwa uliyonayo
Njoo kwake Yesu akuponye kabisa ×2
1. Bwana Yesu alisema,
Nitalivunja kanisa
Na kulijenga kwa siku tatu
(Chorus)
Kanisa ni mwili wako
Ni uwe mtakatifu ×2
2. Yesu alimaanisha
Atakufa na kuzikwa
Na afufuke siku ya tatu
(Chorus)
Kanisa ni mwili wako
Ni uwe mtakatifu ×3
1. Limetimia tabirio alilotabiri mtumishi (wake Mungu)
Akasema, tujenge kanisa liitwalo safina
Kama vile Bwana Mungu livyonena na Nuhu
Ndivyo nasi twatimiza lake nabii ×2
(Chorus)
Watu wote tujenge tujengee tujenge safina
Nyumba ya Mungu wetu
Heri yeye, heri mtu yule atakayeingia
Katika nyumba hii.
2. Ewe baba tunakuomba tuajalie kuwa na moyo (wa umoja)
Na bidii, tujenge safina kwa utukufu wako
Kama vile roho wako anenavyo na sisi
Tutumike nyumba yako iimarike ×2
3. Katika safina ya Bwana waliingia waliotakaswa na dhambi
Na walomwamini yehova katika maisha yao
Nakuomba ewe baba unijalie nami
Niwezeshe niingie kwa nyumba yako.
(Ewe baba) Ee baba,ee baba,ee baba naomba takasa roho yangu
(niepushe) uniepushe katika mawimbi ya ulimwengu huu ×2
1. Ijapo walihubiriwa kusanyiko lenye hasara
Wafundishwa mchana wote wasiweze kufahamu lolote
Kumbe kwa macho yao na kwa masikio yao
Na kwa fahamu zao hawakuokoka kwayo
Mioyo ya kupumbaa.
2. Wewe ni mwenye upungufu roho anayajua yote
Na majibu uliyonayo yaache usikilize ya roho
Maana moyo wako ni ule wa kupumbaa
Na roho aokoa moyo wa kuongezeka
uwachao yale yake.
3. Simtakie mhubiri akufundishe upandavyo
Atende kama upendavyo hutaokoka kwa yako mwenyewe
Si kama upendavyo, wala kwa uwezo wako
Bali kuongezeka kupokea la mwengine
Nawe utafanikiwa.
1. Nguvu mara mbili kotekote baada ya mwanzilishi wetu
Maendeleo yote twayaona. ×2
(Chorus)
Basi hivi ndivyo ilivyo kama Elisha kwa Eliya
Alipokea nguvu mara mbili na mitume wote wa
Yesu waliamuru kwetu sisi tuipokee nguvu mara mbili
(Hivyo) awaye yote atendaye mema azidi sana kutenda mema (Naye) naye yule atendaye uovu azidi sana kutenda huo (mara natha)
2. Ulimchukia mwanzilishi hata hivi mwenyewe wajua
Chuki yako sasa ni mara mbili ×2
3.{ACAPELLA }
Sasa wewe mwenyewe chagua mambo yote ni dhahiri kwako
Matendo yako yakushuhudia. ×2
1. Roho mpya tuwe nayo
Roho ya nyama isiyo ya jiwe
Roho iliyo na hofu
(Chorus)
Twaomba tuajalie maishani tuwenavyo
Uungame na kuacha uende kimungu
(uwe mtakatifu) siku kwa siku
(uwe safi mbele) za Mungu wako
2. Roho isiyo na hofu
Yatokana na dhambi kwa wazazi
Dhambi iliyo ya laana.
(Chorus)
Twaomba tuajalie maishani tuwenavyo
Uungame na kuacha uende kimungu
(uwe mtakatifu) siku kwa siku
(uwe safi mbele) za Mungu wako ×2
1. Kanisa tuweni macho na wale ndugu za uongo
Wanataka kuwapotosha\kwani ndimi zao nyepesi maneno ni mengi
2. Hunena hata kwa lugha, ili msiwatambueni
Maneno huyabadilisha
Na kuyafanya kuwa vile wanavyotaka
3. Hutahadharisha wengi, ili wakajitosheleze
Na mafundisho kuyafanya
kuwa mizaha mbele zao na kicheko kwao
4. Fahamu ni roho gani, yafanya kazi ndani yao
Kwenu msio watiifu
Mnaletewa nguvu hii ili mpotee
1. Kweli uvivu huleta umasikini
Utakayohitaji yatakuwa ni mengi
Hivyo umasikini, ni kama mnyang’anyi
(Chorus)
Tafakari njia za chungu
Kwani yeye hana akida
Wala msimamizi ×2
2. Kwani uvivu ni kudumu kwenye dhambi
Ukaidi na pia kutofuata la Mungu
Utiifu ujivike, utashinda uvivu
1. Njoni nyote tumwabudu
Aliyebwana wa mabwana
Furaha tukimwabudu
Mungu wa kweli siku zote
(Chorus)
Ewe nafsi yangu moyo wangu
Na vilivyo ndani yangu vihimidi
jina lake
Afanya yaliyo ya ajabu
Ukimuamini fadhili zake
Ni za milele
2. Njoni nyote tuhimidi
Jina lake muumba wetu wema wake kwetu sisi
Ni dhahiri tumeshauona
3. Mwimbieni kwa zaburi
Tafakari ajabu zake
Jisifie jina lake
Enyi wateule wake Mungu
1. Mchagueni Mungu wa kweli mtakaye muabudu
Mtasitasita kwa mawazo mawii hata lini
(Chorus)
Ndipo uwe na uhuru wa kuabudu kwa hiari
Nawe uwe na hakika unapoomba kwa imani
2. Kama Eliya alivyowakusanya watu mlimani
Wakasadiki kuwa Mungu wa Eliya ndiye Mungu
3. Nanyi ombeni kwa jina lake Mungu mliechagua
Mungu ajibuye kwa moto ndiye Mungu tasikia.
1. Imani ya umoja miujiza yake yavivia
Kwani maongozi yake yadumisha utakatifu
(ambao) bila huo hutamuona Mungu
(Chorus)
(Imani) ya umoja na uvivio
(Ni thabiti) haikosi pendo
(bila pendo) hakuna umoja ×2
2. Na wote wa imani hii wanao huo umoja
Wanapofundishwa hofu ya dhambi hutii pamoja
(kwa kuwa) ni umoja wa kushinda shetani.
3. Injili ya umoja yaenezwa mahali popote
Waihubirio waihubiri katika umoja
(ili wa) liofungwa wapate funguliwa
4. Watoa mali zao pamoja injili itangazwe
Kama pendo la Mungu mwenyewe alimtoa mwana
(Mungu ba)ba na mwana wakiwa na umoja).
1. Tumikia Mungu wako kimo ulicho nacho
Fanya kazi kwa bidii kama alivyo kuita
Mwenye cheo na asiyenacheo
Kila mmoja anapopahali pake
(Chorus)
Ee ndugu acha kutafuta cheo
Nafasi Mungu amekupatia bidii na heshima
Kwani ndio njia pekee ya madaraka ×2
2. Mrefu hawezi kuingia mahali pafupi
Na mfupi hawezi kufikia mahali parefu
Natuheshimiane tulivyo
Utumishi wa bwana uimarike
3. Mdogo atatua dogo lililodharauliwa
Mkubwa atatua kubwa mdogo asiloliweza
Isawazishayo ni heshima
Na hivyo ndivyo twamtumikia bwana.
1. Je mwenzangu umeshatambua maisha yako kwamba ni mafupi
Jaza maisha yako, tele matendo mema
Matendo ya Mungu yakumpendeza ×2
2. Mahubiri yanatuambia njia ni mbili utafata ipi
Fata njia ya Yesu na fundisho la Yesu
Utie matendo upate Baraka ×2
3. Sikiliza sauti ya Mungu ukaungame pia ukatubu
Kisha tolea Mungu tena tumika kwake
Uwakaribishe wageni kwako ×2
(Chorus)
Bwana yesu yu hapa naye anawaita
Wa mizigo mizito atawapumzisha
1. Ndugu usiwe mgumu moyoni
Kubali Yesu awe kiongozi wa maisha yako ×2
2. Wokovu wa maisha yako yote
Wategemea uamuzi wako hapa duniani ×2
3. Amua leo usiseme kesho
Mungu muumba ndiye ajuaye ndiye apangaye ×2
Chorus ×3
1. Yanyosheni, yanyosheni mapito ya bwana
Ili apitie ×2
Mwokozi amekuja kuwaokoa ×2
Wenye dhambi na waliopotea
2. Wamwamini Mungu baba juu pia umwamini
Na Yesu mwokozi ×2
Yeyote anayemuamini Yesu ×2
Atatenda Yesu anayosema
3. Njoni kwangu mnaolemewa, mizigo ya dhambi
tawapumzisha ×2
Maana nira ya bwana ni laini ×2
Mzigo wake na pia ni mwepesi.×3
1. Uwe hodari wa moyo, na pia ushujaa mwingi
Hapatakuwa na mtu, mbele yako maishani
Utende kama alivyo kuagiza mwanzilishi
Mimi bwana nikuamuru
Ee Joshua usiache enda mbele
Mtumishi usiache enda mbele
Na wachache uliowapata, wenye hofu watupie mbali
Maana mimi Mungu sipendezwi naye
Mtu wakusitasita.×2
2. Mimi ni pamoja nawe kuwaongoza watu hawa
Watafuata popote kulia hata kushoto
Nami nikufanikishe wairithi nchi hiyo
(Chorus)
Mimi bwana nimeahidi
Ee Joshua usiache enda mbele
Mtumishi usiache enda mbele
Na wachache uliowapata, wenye hofu watupie mbali
Maana mimi Mungu sipendezwi naye
Mtu wakusitasita ×3
1.Mungu wetu ndiwe mtukufu na umkamilifu muweza
Mapenzi yako yatendeke, unapoongoza kanisa
(Ewe Mungu) sikia
Tunakililia, tuongoze (bwana) kwenye njia ya kweli ×2
2. Tunamuomba kiongozi atawaliwe na roho wako
Kampe na uwezo wako ujasiri hekima yako
3. Na wazee wa kanisa hili wajaze nguvu zako eee Mungu
Na sisi waimbaji wote tuongozwe na roho wako
4. Tunawaombea wahubiri watangaze injili kwa moyo
Na wasiokujua Mungu wawavute kwako waokoke.
Chorus ×3
1. Njoni tumsifuni Mungu baba yetu
Afanya yaliyo ya ajabu
Njoni tumfanyie shangwe enyi mataifa
Maana yeye ndiye mwenye vyote
(Chorus)
Uzima (na uzima)ni wake (wa milele)
Ni wake muumba wetu
Na mali(mali zote), ni zake(za dunia)
Ni zake muumba wetu
(Kwa hivyo )tusifu kwa moyo wote
2. Njoni muone kazi zake Mungu
Anavyojidhihirisha wazi
Basi tumsifuni Mungu kwa pendo lake
Kutupa kiongozi wa kweli
(Chorus)
Njooni (tuje sote) kwa nguvu, (tumsifu)
Kwa wema anaotenda
(Kwa kuwa), katupa, (muhubiri)
Mtu wa kunena kweli
(Kwa hivyo) heshimu upate heri
1. Sote tufurahi kwa kuwa Mungu ameshatimiza
Ahadi yake ya kutuinulia nabii
Atakayetueleza kweli yote Mungu atakayo x2
(Chorus)
(Watu wote) njoni na tumkaribishe (kwetu) moyoni
Elimu zetu tuache pia na kujua kwetu
Tuone uwezo wa Yesu. x2
2. Hivyo uko hapa na utaraji jaambo jipya leo
Bila kukosa na ukauone uwezo
Atakaokupa bwama hivi sasa Mungu atukuzwe. x2
1. Mungu anasema atawainulieni nabii
Katika ndugu zenu
Msikieni yeye katika mambo yote atakayonena nanyi x2
(Chorus)
Na itakuwa ya kwamba kila mtu asiyemsikiliza
Nabii huyo ataangamizwa na kutengwa na watu wake x2
2. Petro na Yohane walishangaza wazee na waandishi
Kwa kuwa na nabii Yesu
Japo walikuwa watu wasio na elimu
Wala pia maarifa x2
Utashangaza shetani kwa vile unavyoyapata mema
Kupona Baraka kwa kumfuata mtumishi wake Mungu x2
3. Shida ulizonazo na uovu ulionao wewe
Ni wazi kutengwa kwako
Heri ughairi usikilize nabii
Upate amani yake x2
Na utakuwa ya kwamba, kila mtu asiyemsikiliza
Nabii huyo ataangamizwa na kutengwa na watu wake.
1. Ni ajabu, (safina sasa imekwisha kamilika)
All:
Sote tunaiona sote tunafuraha
Imepambwa (Jamani kweli safina inapendeza)
All:
Kwani tumetimiza amri ya mwanzilishi. x2
(Chorus)
(Yatupasa tufahamu)
All:
Twapata wokovu sasa
Twasamehewa na dhambi, twapona magonjwa yote
Na twabarikiwa. x2
2. Burudika (wewe uliyejikana kwa hii safina)
All:
Sasa ufurahie, sasa ushangilie
All:
Kazi yako (Si bure Baraka kutoka kwake Mungu)
Zitakujia wewe ukose kwa kueka
Chorus x3
1. Nyakati hizi tunazoishi (ndugu zangu) ni za mwisho
Hakuna mda wa kuchezea (ufalme) umefika *2
Dalili zajionyesha,
ya kwamba kuja kwake Masihi kukaribu,
Maovu yaongezeka, Upendo umepoa *2
Chorus:
Bado kama kufumba na kufumbua (na kufumbua)
Yesu yuwaja upesi siku hiyo je utakuwa wapi. *2
2. Sasa nabii yu kati yetu (yu tayari) kuongoza
Kama Yoshua kutufikisha (nchi ile) ya sayuni *2
Sote Tumsikizeni, maana Mungu wetu ndiye kamchagua kutuelekeza njia, njia ya mbinguni. *2
(Chorus) *2
3.Tujitakase mioyo yetu (tutubie) kwake Mungu
Kwani ni wale watakatifu (watakao) fika huko. *2
Tuziache dhambi zetu, tukatende haki tuifikie ahadi,
ile ya kuingia, Katika raha yake. *2
(Chorus)
1. Njoni kwangu wenye mizigo
Pia magonjwa mpumzike
Mimi niko tayari kuwaokoa
Tena niwasamehe
(Chorus)
Mimi bwana Mungu wako
Nimeyanena haya, sadiki
Nawe upumzike
Kwani wewe uliasi
Ukatekwa na shetani na sasa
Yesu anakuita.
2. Mmedumu katika dhambi
Na kumtumikia shetani
Matunda yake sasa mmeyapata
Magonjwa na mateso
3. Mema haya ni kwake yule
Mwenyekutii neno la Mungu
Na kunyenyekea kufanyika mwana
Kuacha ya shetani
1. Naomba baba yangu unisikie sasa x2
2. Umetuleta hapa kukutukuza wewe x2
3. Bariki watu hawa twaomba utimize x2
4. Tukuka ndani yetu tuinue jina lako x2
5. Ponya magonjwa yao wakakufurahie x2
6. Baraka tunaacha mbarikiwe nyote x2
(Chorus) x2
Tunaimba, Halleluya tunaimba Halleluya x2
Kwa furaha, """"""""""""""""""""""""""""""""x2
Kwa amani, """""""""""""""""""""""""""""""""x2
Kwa vinanda, """""""""""""""""""""""""""""""x2
Tunaimba, """""""""""""""""""""""""""""""""
1. Siku ya leo
All:
Twakushukuru ee Mungu wa Mwanzilishi
Kukamilisha miaka ishirini na mitano
Tangu msingi wa neno hili
Uliloweka na mwanzilishi x2
Tazama kazi yako yatendeka
Nasi sote twaziona
Ni wewe unayejidhihirisha
Ndani yake mjumbe wako
2. Jengo letu safina limeshakamilika
Upanuzi wa injili Afrika mashariki
Uponyaji wa imani magonjwa yaliyoshinda
Basi tuimbe, tucheze sote, Ahadi zetu
Tumezipata, tumsifu Mungu kwa shukurani
Tutamiliki hata milele. x2
Sasa tunaifungua safina hii
Karibuni nyote pamoja
Tabirio la mtumishi wa Mungu latimia
Kupitia kwa maongozi ya mjumbe wake Mungu
Kutolea Mungu ni hakikisho
Kwani sote twaona (tabirio)
Kweli limetimia
Safina yetu sada (twaiona)
Imeshakamilika
Kama nuhu na waliojenga safina
Hawakunyeshewa kabisa
Wewe uliyejitolea kwa moyo furahia
Tarajia amani kutoka kwake Mungu baba
Basi nasi tufurahi kwa kazi hii
Tuliyowezeshwa na Mungu
Hata kama hukuwezeshwa kutoa furahia
Jipe moyo na uingie kwa utumishi huu.
Kama ilivyo ahadi yake muumba
Kazi yako yote si bure
Agiza Mungu chochote utakalo utapata
Hakuna lililogumu kwake Mungu wa mjumbe.
1. Miaka ishirini na tano (haipungui)
Sauti ilitoka kwa Mungu (na ikasema) x2
(Chorus)
Uache baba, uache mama, uache na wajamii yako yote
Uache shamba pia dhahabu, uende kuishi nchi ya ugeni. x2
2. Na huyo mteule wa Mungu (akasafiri)
Mpaka hata ng’ambo ya pili (kwenye kisiwa)
(Chorus)
Ukae hapa, ukangoje nitakutuma kwa mtumishi wangu
Akuombee, nikutumie, uanze kazi kwa ulimwengu wote x2
3. Na kazi ilikua ni ngumu (ya kuhubiri)
Kupingwa waziwazi kabisa (na watu wote)
(Chorus)
Utatangazwa, kwenye radie na magazetini yatakunena pia
Ujipe moyo, ukahubiri, wokovu na uponyaji na Baraka.
4. Na sasa kazi imetimia (ya kuuweka)
Msingi huu wa kuhubiri (kwa ulimwengu)
(Chorus)
Tumefikia mwisho wa mwanzo wa msingi wa kuifanya kazi
Umuhubiri Yesu mwokozi kwa waafrika na ulimwengu wote.
1. Hakuna mtu (ndugu) azifanyaye ishara hizi
Isipokuwa Mungu yuko pamoja naye. x2
2. Na Mungu wetu (sisi) akainua mjumbe wake
Mwenye uwezo wake roho mtakatifu. x2
3. Hata mitume (wote) wazama zile walipokea
Uwezo wake huyu roho mtakatifu. x2
4. Na kila mtu (yule) azifanyaye ishara hizi
Ni kwake yule anayemcha Mwenyezi Mungu. x3
1. Mungu ee Mungu wa mwanzilishi x2
Twakushukuru kumuwezesha mjumbe wako
Kutujengea safina hii
Mungu ee Mungu wa mwanzilishi
2. Safina ya Nuhu uliingia
Wawili wawili kila aina
Nawe ndugu yangu, ujitahidi
Ukawe katika ya waingiao
Kwani neno lake Mungu linapohubiriwa
Linatafuta atakayeingia
Safina ya Mungu ni takatifu
Safina ya Mungu ni nyumba ya maombi.
Kanisa la Mungu ni mwili wako
Kanisa la Mungu nyumba ya maombi
Kanisa safina ni mwili wako
Kanisa safina nyumba ya maombi
Mungu ee Mungu, wa twakushukuru
1. Tukisoma Yohana mlango wa nane
Fungu la thelathini na moja panasema
All:
Yesu kawambia wayahudi waliomuamini
Ninyi mkikaa katika neno langu
Mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli x2
2. Mjumbe leo yu hapa mtumishi wa Mungu
Atufunze yale yote ya Mungu yasemayo
All:
Kweli dhambi zetu mbaya ndizo zatutenga na Mungu
Basi hivi leo tukikaa kwa furaha
Kusikia kutoka kwa Mungu baba yetu x2
3. Tupokee kwa moyo yale yanatoka
Kinywani kwa mtumishi wa Mungu na lolote
All:
Atakalosema tulishike kama yule kipofu
Alivyompokea yule nabii Yesu
Kwenda nawa siloamu alikoagiziwa.x3
1. Chipukizi katika shina la Yesse
Lisimamalo kuwa ishara
Tawi litokalo mizizini mwake
Na litazaa matunda
(Chorus)
Roho ya bwana ijuu yake, hekimaa ufahamu na maarifa
Furaha yake kwao wamchao bwana. x2
2. Tazama huyu ndiye mwokozi wetu
Tushangilie na tufurahi, kwa kuwa ndiye bwana wa mabwana
Tuliye mngojea sana.
(Chorus)
Maana kwa ajili yetu kazaliwa mfalme wa amani
Na uwezo, ni mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu. x2
3. Mamajusi, wachunga walifuata nyota kuu ya mashariki
Ili iwaongoze bethlemhenu alikolazwa mtoto
(Chorus)
Walizobeba ni zawadi zao uvumba Manemane
na pia tunu, wamsujudu Mfalme na mwokozi wao. x3
1. Kuna nchi nzuri kabisa
Nchi hiyo ya kupendeza
Mwangaza ni Yesu amulika x2
(Chorus)
i) Njoo kwake Yesu umulikiwe
Na mavazi yako yawe meupe
ii) Vazi lako wewe ni roho yako
Ukiacha dhambi yawa nyeupe
2. Na walio kwenye nchi hii
Mavazi yao ni meupe
Ni safi na ni watakatifu x2
3. Utafika kwenye nchi hii
ila umwamini mwokozi
Apate samehe dhambi zako x2
1. Enzi ni yake, enzi ni yake
Mungu juu, Mungu juu
Na nchi salama. x2
2. Enzi ni yake aliye juu x2
Enzi ni yake, Mungu juu
Na wanadamu wapate radhi x2
Sasa, na daima, na asifiwe Mungu
1. Kuna nini huko mji wa Daudi
Umati wa watu ni mkubwa sana
Wote wanangoja saa timilifu
Saa yake Bwana yakuzaliwa
(Chorus)
Bwana Yesu amezaliwa, ni mkombozi wa ulimwengu
Tumepokea, mwana wa Mungu
Tupate wokovu wa dhambi zetu x2
2. Mwana gani huyo mwana wa ahadi
ilitabiriwa kuzaliwa kwake
kaja fanya nini kaja kuokoa
Wanadamu wote toka dhambi zao
(Chorus) x3
1. Hebu mtazame Yesu mwokozi
Anasononeka msalabani
Kamwaga damu juu ya mti
Ni kwa ajili yetu.
(Chorus)
Amini damu yake Yesu
Uoshwe dhambi zako zote
Uponywe na magonjwa yote
Upate uzima milele x2
2. Alipokuwa karibu kufa
Aliomba kwa baba yake kwamba
Ee baba yangu wasemehe wote
Hawajui watendalo
3. Hili ndilo pendo lake Mungu wetu
Kamtoa mwana wake wa pekee
Nasisi tuonyeshe pendo letu kwake
Kwa kutii neno lake.
(Chorus) x2
1. Mungu anatembelea kila mmoja wetu
Akikukuta najisi bass (kama watenda dhambi)
Atapita na kando
Basi jitenge na uchafu
Wa aina yoyote Bass (kwani yuko kati yetu kutembelea)
Ili apitapo aweze kukutembelea
(Chorus)
Kati ya vifaa ulivyonavyo, usikose kajeembee
(Utakakokatumia, kuchimba na kuficha uchafu wako
Ili Mungu ajapo atende kazi kwako)×2
2. Chochote unachofanya kinyume chake Mungu
Hicho ndicho najisi bass (hicho ndicho najisi)
Mbele za Mungu wako x2
Dhambi zetu tukiziacha
Ndipo twauzika uchafu bass (kwani yuko kati yetu kututembelea)
Ili apitapo aweze kututembelea.
(Chorus) x2
1. Je humo rohoni mmesafishwa taka
Kutayarishwa kwa kuzaliwa mwana
Kwa kuwa mwana ni mwokozi na mfalme
patakuwa safi
(Chorus)
patakuwa safi, roho iwe safi
2. Yeye alikuja kwa walio wa dhambi
Heri kuwekwa nyasi chakula cha ng’ombe
Hivi leo ziondoe taka rohoni
patakuwa safi.
3. Na wewe mwenzangu hori ni roho yako
Mkaribishe mwana azaliwe humo
Atawale rohoni mwokozi na mfalme
patakuwa safi.
(Chorus) x2
1. Yesu alikwenda kuyaandaa makao
Atarudi tena kuwachukua wakristo. x2
(Chorus)
Sol:
Kubali wokovu, wokovu wake Yesu
All:
Bwana Yesu alikuja, alikuja kuokoa
Wanadamu toka dhambi.
2. Wamwamini Mungu umwamini na mwokozi
Kwake baba Mungu makao ni mengi sana. x2
(Chorus) x2
1. Mwokozi yesu amezaliwa bethlehemu
Malaika wamwimbia shangwe
Wachunga kondeni waziacha kondoo
Ili wakamsujudie
(Chorus)
Shangwe shangwe kuu
Kitoto kimelazwa
Hosianna sana
Ndiye kitoto mkombozi
2. Ni siku njema yenye furaha
Na ya thamani, alama yenye wokovu wetu
Tujitoe sote shughulini mwetu
Ili tukamsujudie
3. Wambebea tunu uvumba na manemane
Zawadi zetu moyo tumpe
Tujitoe sana maishani mwetu
Ilitukamsujudie
4. Nyota kuu ya mashariki ituongoze
Ni mtumishi wa bwana Mungu
Atuangazie tuione njia
Ilitukamsujudie
(Chorus) x2
1. Nautazama uso wake mwana wa Mungu
Akiwa Gethsemani
Anaomba akiugua usiku kucha
(Chorus)
Niokoe bwana na haya majaribu
Niepushe kikombe cha mauti x2
2. Mwili wake mwokozi ulijaa matone mazito sana
Yadondoka kama damu, chini ya ardhi
3. Roho yake mwokozi ulijaa huzuni
Kwa kiasi cha kufa alibeba mzigo wote
Wa dhambi zetu
(Chorus) x 2
1. Kuzaliwa kwa Yesu, huruma za Mungu kwetu sisi
Viumbe wake wote tupate okoka
Yesu amezaliwa ulimwenguni
Ameleta ukombozi kwetu sisi
mwamini usipotee
Bass (Bali uwe na ukombozi maishani)
Ya leo na yajayo. x2
2. Na ukitafakari, Mungu hangeleta mwana wake
Azaliwe horini mahali panyonge
3. Ni kwa ajili yako, upate kutoka matesoni
Hivyo amua sasa kuacha uovu
1. Furaha furaha ni furaha
Ya kuzaliwa kwake Yesu
Ni mtoto mzuri mno
Bass (Hata mbinguni pia kuna furaha)
All: Ya kuzaliwa kwake Yesu
(Chorus)
Hosanna hosanna jeshi kuu la mbinguni
Waimba wakimsifu Mungu
Bass (Anakuja kwa jina la bwana)
All: Wanadamu wapate radhi
2. Habari ni njema tumeletewa ya kuzaliwa
Kwake Yesu
Katika nchi ya uyuda
Bass (wamakondeni sote twendeni kwake)
All: Tusujudie kwake Yesu
3. Chukua zawadi zenye thamani
Tuzipeleke kwake Yesu
Iwekwako shukrani
Bass (Na mamajusi pia walipeleka)
All: Zawadi zao kwake Yesu
4. Karibu mwenzangu amealikwa
Uelekee kwake Yesu
Jiunge nao msafara
Bass (Itamulikwa njia na nyota kuu)
All: Ituongoze kwake Yesu
(Chorus) x2
1. Nashukuru Mungu wangu, nguvu zote ni zako
Nashukuru bwana wangu, umeniokoa x2
(Chorus)
Natumai siku moja
Nitakwimbia mbinguni
Kwa vinanda na mazeze
Milele na milele x2
2. Ingawa nipate tabu, ya kuteswa duniani
Wewe uliteswa sana, zaidi yangu mimi
3. Ingawa nipate tabu, ya kupigwa duniani
Wewe ulipigwa sana zaidi yangu mimi
(Chorus) x3
1. (Sop) Katika rama kuna kilio watoto wengi wamekufa
All : Sababu ya roho mbaya ya Herode
(Chorus)
Adui ni wengi wanao taka kumuua mwokozi
Mlinde mwokozi moyoni, ukayashinde majaribu
2. (Sop) Na hata Musa wa zamani likimbilia Midiani
All : Sababu ya roho mbaya ya Farao
3. (Sop) Nawe mwenzangu sikiliza umpokee Bwana Yesu
All : usifanye roho mbaya ya Kwa Mwokozi
(Chorus) x2
1. Hapo mwanzo kulikuwa na neno
Naye neno aliyetoka kwa Mungu
Akashuhudiwa na Yohana akasema
Yuko mtu ajaye kwa jina la bwana.
(Chorus)
Naye ni Yesu aliyendani ya mjumbe wa Mungu
Basi mpokee sasa kwani amezaliwa horini x2
2. Huyu Yesu alikuwa ni Nuru
Kaleta habari za ufalme wa Mungu
Aliyepokea maneno haya ya Yesu
Alipata ufalme wa haki ya Mungu
3. Mtumishi wake Mungu yu hapa
Ananena habari zake huyu Yesu
Basi mpokee kwani yeye ametumwa
Ili nawe upate ufalme wa Mungu.
(Chorus) x2
1. Hii ni krismas, siku ya kuzaliwa
Aliyetabiriwa, mwokozi wa ulimwengu x2
2. Yesu kazaliwa ili akuokoe
Baada ya wokovu uinie paradiso x2
3. Mpokee Yesu kwa kuwa ndiye njia
Ya kweli na uzima kwenye ufalme wa mungu x2
4. Ufunue moyo azaliwe mwokozi
Upate kiongozi katika maisha yako x2
5. Mungu akupenda kwa utumishi wake
Ili akubariki na kukuponya mateso x2
1. Kumbukeni mji wa ninawi yona alivyotumwa
Kakimbia kwenda tarashishi aepuke uso wa bwana x2
(Chorus)
Yona (katangaza ) siku arobaini ndizo zimebakia
Mji wote ninawi wote uangamizwe x2
2. Kweli sote tukumbuke maelfu ninawi
Waliposikia ya Mungu kavunjika x2
(Watu wote) na wanyama walijivika magunia
Naye bwana wa huruma alibadili nia mbaya x2
1. Bikira Mariamu, umebarikiwa na Mungu baba yetu
(Chorus)
Utamzaa mwana, utamuita imanweli
Maana yake Mungu yuko
Pamoja nasi daima. x2
2. Naye Yusufu, ana hofu kubwa kwa, Hiyo mimba ya Mariamu
(Chorus)
Malaika wa Mungu kamtokea Yusufu
Kumwabia usihofu
Kilicho ndani ni safi.x2
3. Mfalme Herode kaghafilika kuzaliwa a kwake Yesu
(Chorus)
akaamuru kuuwa watoto wote nchini
Ili apate kuangamiza
Yesu mkombozi. x2
4. Ndugu ipo nafasi yake mkombozi azaliwe ndani yako
(Chorus)
Hutakuwa na hofu wala hutagafilika
Maisha yako yote nayatakuwa ni shwari x4
1. Ilikuwa siku ya huzuni mwokozi alipokamatwa x2
Mwokozi Yesu alitufia ili tuokolewe x2
(Chorus)
Mwokozi alikufa msalabani
Na damu takatifu ilimwagika
Ili kuzitakasa dhambi za watu
2. Ilikuwa mbele ya pilato mwokozi alipopelekwa x2
Aliulizwa maswali mengi kisha kahukumiwa x2
3. Ilikuwa ndani ya kaburi mwokozi alopolazwa x2
Siku ya tatu alifufuka sasa yuko mbinguni x2
(Chorus) x2
1. Hebu tuwaeleze x2
All : Hebu tuwaeleze mwana wa Mungu ooh kazaliwa x2
(x2)
2. Natumpokeeni x2
All : Natumpokeeni mwana wa Mungu ooh kazaliwa x2
(x2)
3. Tumshangilieni x2
All : Tumshangilieni mwana wa Mungu ooh kazaliwa x2
(x2)
4. Tumsujudieni x2
All : Tumsujudieni mwana wa Mungu ooh kazaliwa x2
(x2)
1. Wito wa mbinguni kwa baba Mungu
Malaika wanatungoja
Napenda kwenda mbinguni kwa mwokozi
Kumwona bwana Yesu uso wake
kanionyesha makao mema mno
Pale watakatifu watakaa x2
(Chorus)
Malaika wanaimba watangoja kwa furaha x2
2. Wito wa mbinguni kwa baba Mungu
Wale waliomwamini
Ikiwa hujamwamini umwamini
Uwe na uzima wa milele
(Chorus)x4
1. Imanueli ni nani huyo
Mungu yuko pamoja na wanadamu
(Chorus)
Ni mfalme tena na mwokozi wetu
Ndiye mshauri wa ajabu x2
2. Na Herode ni nani huyo
Wivu wa bwana utayatenda hayo
(Chorus)
Amewaongoza na akawakosesha
Walioongozwa wakaangamia x2
3. Nyota kuu iwapi hiyo
Ituongoze vyema kwa Imanweli
(Chorus)
Atawale vyema na kutuokoa
Tusije tukaangamia x2
4. Mamajusi sote twendeni
Tuungane nao hao wachungaji
(Chorus)
Kwani ndiyo nyota ituongozayo
Ili tukaupate uzima x3
1. Bwana Yesu anakuita, uje kwake akuokoe
Na mizigo yako mizito yeye atakupumzisha
2. Duniani unavyoishi, yadunia yatakusonga
Bwana Yesu ni kimbilio, ana uzima wa milele
3. Basi mbona unayoshaka, ikiwa ni muumba wako
Yeye aliyekuumba hashindwi kukurekebisha
4. Yeye Bwana hasaidiwi, hakuna asiloliweza
liwe ni jambo gumu vipi, Bwana Yesu yeye ni mwisho
Sol: Hao washauri husema tumia dawa na shida ikizidi muone daktari
All : Washauri husema yakizidi pata mshauri
Sol: Hiyo ni sawa kabisa, wao husema hivyo maana wanao upungufu
All : Hiyo sawa kabisa kwa sababu uko upungufu
Solo : lakini nakuhakikishia Yesu anaweza kwani yeye hashindwi
All : Lakini ninakuhakikishia Yesu anaweza
Sol : huwezi kusema Yesu ameshindwa hadi ukatafute usaidizi mahali kwengine
All : Hutaweza kusema akishindwa pata mshauri(Amen)
(Chorus)
(Halleluya!!) Amen Yesu ni mwisho ×9
(Oo akuita!!) Amen Yesu ni mwisho ×2
(Aa ni mshindi!!) Amen Yesu ni mwisho ×2
(Halleluyah !!) Amen Yesu ni mwisho× 2
Sol : Yesu ni mwisho kwake hakuna lisilowezekana Bwana Yesu anakuita ukimkimbilia atakupumzisha
Halleluyah.
(Chorus)
(Halleluyah!!) Amen Yesu ni mwisho ×5
(Oo akuita) Amen Yesu ni mwisho ×2
(Oo ni mshindi) Amen Yesu ni mwisho ×2
(Halleluyah!!) Amen Yesu ni mwisho ×3
(Halleluyah!!) Amen Yesu ni mwisho ×3
1. Kamba za mauti zikikuzunguka
Shida za kuzimu zikikupata ×2
(Bass) Ukiona tabu nyingi na huzuni nyingi
Hebu mwite Yesu
(All) Atakuokoa nayo mateso mengi
Maana yeye ndiye bwana
Wa mema yote ×2
2. Yesu huinua mnyonge kutoka
Kwenye mavumbi na kumpandisha×2
(Baas) Masikini toka jaani amketishe
Na walivyonavyo
(All) Huweka nyumbani
Mke aliyetasa, awe
Mama yake, wana wenye furaha ×2
(Bass) Hivyo usifadhaishwe na mateso hayo unayoyaona
(All) Yesu alimwaga damu yenye thamani
Ili uosheke nayo mateso hayo ×2
(Chorus)
Wokovu ni nini ndugu, ni kubadilika
Na kuziacha dhambi kumuamini Yesu
Sol:
1. Watu wengine wanafikiria ya kwamba
Eti kuimba kwaya huko ndiko kuokoka
Hiyo ni kazi Mungu amekupatia
Lakini yakupasa wewe upate kuokoka
2. Pia kuhubiri ni kazi nzuri sana
Mungu amekuita hubiri kwa moyo
Lakini yakupasa upate takasika
Njia ya pekee kwenda juu kwa Mungu baba
3. Pengine una huduma nzuri kanisani
Mungu amekupatia ufanye kwa hiari
Lakini yakupasa upate kuokoka
Ukifa ukaishi na Mungu muumba wako
4. Dini haitaweza, cheo hakitaweza
Sanamu haitaweza, hata nabii hataweza
Ila ni damu ile iliyomwagika
Na jina lake Yesu hili ndilo linaokoa
5. Pengine una mali tena unayo afya
Unavyovitu vyote kwenye dunia hii
Usije ukadhani ati huko ni kuokoka
Huo ni utajiri Mungu baba amekupa
6. Pengine unadhani ati umeokoka
Hata kanisani wewe hukosi kila siku
Ili matendo yako na mawazo yako
Na mapambo yako yote siya kuokoka
7. Mtu hutenda neno moja kwa wakati mmoja
Wokovu na dhambi haviwezi kuwa pamoja
Usibaki na alama za shetani mwilini mwako
Na tena useme ati kuwa umeokoka
(Chorus)
Sol:"""""""""""""""
ALL: """""""""""""""X2
(Chorus)
Dunia yapita, mbingu zinapita
Neno lake bwana linasimama
Sol:
1. Amri za Mungu zinasema wazi
Na kila uovu uko dhahiri
Ikiwa ni dhambi, Mungu haitaki
Kwani yeye bwana hajuti kamwe
2. Ewe mwanadamu, uutende uovu
Ujipendekeze unavyotaka
Lakini ujue haiwezekani
Kulibadilisha neno la bwana
3. Hata mhubiri asiponena kweli
Bado huyo kwei yabaki kweli
Nawe ndugu yangu usipotenda kweli
Hiyo haitoshi kuibadili.
(Chorus) x3
1. (Halleluya! ooh halleluyax3) x2
Halleluya! Halleluya!
2. (Lisifiwe jina la bwana Yesu x3) x2
Lisifiwe milele
3. (Isifiwe damu ya bwana Yesu x3) x2
Isifiwe milele
4. (Usifiwe uwezo wa bwana Yesu x3) x2
Usifiwe milele.
5. (Halleluya! ooh halleluyax3) x2
Halleluya! Halleluya!
(Chorus)
Asante bwana, Asante bwana
Kwa neno lako
Sol:
1. Kuniokoa, Nashukuru x2
2. Kunisamehe, Nashukuru
""""""""""""", Bwana Yesu
3. Kwa kuniponya, Bwana Yesu x2
4. Kunibariki, Ahsante x2
5. Kwa roho wako, Mtakatifu
""""""""""""""""", Nashukuru
(Yesu ndiye hai x2)
Damu yake yaniosha
Nguvu zake zanitosha
Na uzima nalipewa
Kwa Yesu ndiye hai x3
1. Mungu baba katupenda tukiwa wenye dhambi
Kamtoa mwana wake atuokoe
2. Bwana Yesu kajitoa kakubali kuteseka
Sababu ya dhambi zetu tusamehewe
3. Je ndugu una lipi la kumuonyesha Mungu
Dhihirisha pendo lako kwa muumba wako
Sol:
Basi ndugu ziungame dhambi zako si kwa sababu ya shida zako
Bali kulidhihirisha pendo lako kwa muumba wako
Pia mali zako zitoe si kwa kutaka Baraka tu
Bali kulidhihirisha pendo lako kwa Mungu wako
Na utakatifu zingatia sana si kujipendekeza na kujionyesha kwa watu
Bali kulidhihirisha pendo lako kwa Mungu wako
(Chorus)
All:
Basi ndugu jitoe kuungama dhambi zako
Kulidhihirisha pendo lako kwa Mungu wako x2
Mali zako zitoe kwa utumishi wa Mungu
Kulidhihirisha pendo lako kwa Mungu wako x2
Zingatia sana utakatifu moyoni
Kulidhihirisha pendo lako kwa Mungu wako x2
Sol:
Ikuwa Mungu alitangulia kutupenda tukiwa tuwenye dhambi
Akamtoa mwanawe afe kwa ajili yetu apate kutuokoa
Hivyo upendo huo ni wa kweli hauna hila ndani yake
Basi inakupasa uonyeshe upendo huu
Si kwa faida ipatikanayo tuu
Bali kulidhihirisha pendo lake kwa Mungu wako
(Chorus)
Ahadi ya Mungu ni wokovu
""""""""""""""""""""""Kupona
""""""""""""""""""""""Baraka
""""""""""""""""""""""Furaha
""""""""""""""""""""""Amani
""""""""""""""""""""""Mbinguni
x2
(Chorus)
Fata Mungu ndugu yangu kwa sababu unapenda
Sol:
1. Isiwe ni sababu ya kutajirika
2. Isiwe ni sababu ya Kutaka sifa
3. Utumishi wako ndugu na uwe wa hiari
4. Ukitoa mali yako utoe kwa hiari
5. Isiwe ni sababu ya kuonekana
6. Isiwe ni sababu ya Kupata cheo
Sol: Fata Mungu ndugu yangu kwa sababu unapenda
All:"""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""" x4
(Chorus)
Mwenya imani zingatia utakatifu
Bila huo huwezi kufika mbinguni
Kwani wokovu umekua ni kawaida
Kila mkristo asema ameokoka
Sol:
1. Ewe mwenzangu sikiliza nikwambie
Wokovu sio jambo la muhimu sasa
Sasa unahitajiwa utakatifu
Uletao wokovu siku za mwisho
2. Hata walimwengu wameshakuambia
Huezi kuokoka sasa na ni kweli
Utaokoka na hukumu ya jehanamu
Baada ya kujitakasa hivi leo
3. Wokovu ni baada ya utakatifu
Watakaokoka ni watakatifu
Wataingia mbinguni patakatifu
Wakiimba halleluya patakatifu
“Nasoma katika bibilia, kitabu cha Mathayo mlango wa 24:13
Kinasema ya kwamba atakayevumilia hadi siku ya mwisho
Ndiye atakaye okoka
Lakini swali ni kwamba mtu atawezaje kuenenda kitakatifu
Ni apate mtu naye ni mjumbe wa bwana anayeenda
Kitakatifu amfundishe kitakatifu kwa usahihi mpaka aelewe na
Aweze kuingia mbinguni.
(Chorus)
1. (Soprano): Ajikwezaye atashushwa
All: Ajishushaye atakwezwa
Soprano: Neno la Mungu latuonya,
All: Unyenyekevu tujivike
Mungu huwapinga wenye kiburi,
(Tenor): Lakini
Huwapa wanyenyekevu rehema x2
(Chorus)
(Tenor + Bass): Kila aajikwezaye
All: Atadhiliwa
(Tenor + Bass): Naye ajidhiliye,
All: Atakwezwa
Ndungu ondoa kilemba hicho cha ukuu
Vua pia nayo taji hiyo ya kiburi
Ewe Mkristo unyenyekevu ujivike x2
2. (Soprano):Watu wengine wanapenda,
All: Waonekane ni wakubwa
(Soprano): Hupenda sifa za dunia
All: Na kudharau ndungu zao
Tena hujivuna hujitukuza
(Tenor): Lakini
Kiburi cha mwanadamu ni bure. x2
(Chorus) x2
Ewe Mkristo unyenyekevu ujivike x2
(Chorus)
Damu yangu (Munywe x2) x4
Mwili wangu (mle x2) x4
Sol:
Ilipofika siku ya pasaka, Yesu aliketi na wanafunzi wake
Na kuundaa meza na kuiita meza ya agano
Akatoa mkate, akatoa kikombe, akakibariki, akasema
Twaeni mle, mnywe hii ndiyo damu yangu imwagikayo kwa
Ajili ya wengi, Agano hili ninakubaliana na Kristo kwamba asivyo
Mwenye dhambi nawe usitende dhambi kwani ndicho kiapo
Ikiwa agano hili linawezesha kuishinda dhambi, basi nivyema nijihoji nakufanya uamuzi wa busara na kula katika meza ya agano.
(Chorus)
Damu yangu (Munywe x4) x2
Mwili wangu (mle x4) x2
(Chorus)
Ahsante Mungu wangu x3
Kwa neno la uzima
x2
1. Umeandaa neno hitaji la nafsi yangu
Haja ya roho yangu chakula cha uzima x2
(Chorus) x2
2. Sasa naja zako nanyenyekea dua kwako
Nafsi yangu ilihimidi pendo lako kuu. x2
(Chorus) x2
Nasema ndio x2
Ndio bwana ndio bwana
Nasema ndio
x3
(Chorus)
Bwana Yesu aja kutuchukua
Kwenda naye juu mbinguni
Sol:
1. Yesu akwaambia, msifadhaika moyoni mwenu
Nyumbani mwa baba mna makao mengi. Mimi ninaenda kuwaandalia
Na tena nitakuja niwakaribishe.
Na Tomasa akasema uendake Bwana sisi hatukujui.
Chorus
Instruments
Chorus
Sol:
2. Yesu akasema, mimi ndimi njia kweli na uzima
Mtu haji kwa baba ila kwa njia ya mimi
Na Filipo aksema tuonyeshe njia nasi tutatosheka.
(Chorus) x2
1. Halleluya kwa damu ya mkombozi
Halleluya tuimbe daima
Halleluya kwa damu ya mwana wake mungu
Halleluya kwake bwana x2
Tunaishi x2, """"""""""""
Twaokoka x2, """""""""""
Tunapona x2, """"""""""
Tunashinda x2."""""""""
2.Yu bwana x3
Amefufuka kifoni yu bwana
Na kila ulimi ukiri kwanza
Yesu ndiye bwana
Aokoa""""""""""
Bwana Yesu anaweza""""""""""
Bwana Yesu anaponya"""""""""""""
Bwana Yesu atawala"""""""'
Bwana Yesu ameshinda"""""""""
Halleluyah ameshinda"""""""""
Halleluya kwa damu ya mkombozi
Halleluya tuimbe daima
Halleluya kwa damu ya mwana wake mungu
Halleluya kwake bwana
1. Chakutumaini sina,ila damu yake bwana
Sina wema wa kutosha ,dhami zangu kuziosha
(Bass): Kwake yesu nasimama,
All: kwake yesu nasimama
(Bass): Halleluyah
All: Ndiye mwamba
(Bass): Hakika
All: ni salama
Ndiye mwamba ni salama
2. Njia yangu iwe ndefu,yeye hunipa wokovu
Mawimbi yakinipiga,nguvu zake ndio nanga.
3. Damu yake na sadaka,nategemea daima
Yote chini yakiisha,mwokozi atanitosha
4. Nikiitwa hukumuni rohoni nina amani
Nikivikwa haki yake sina hofu mbele zake
Sol:
Nimeuona mkono - mkono wa bwana Yesu
All: """"""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""
x 5
Sol:
Nimeziona Baraka-baraka za bwana Yesu
aLL: """"""""""""""""""""""""""""""""""""""""x5
Sol:
Nimeuona uwezo – uwezo wa bwana Yesu
All: """""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""x5
Sol:
Nimeiona furaha – furaha ya bwana Yesu
All: """"""""""""""""""""""""""""""""""""""""""x5
Sol:
Nimeuona mkono - mkono wa bwana Yesu
All: """"""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""
x 5
Ameniweka huru, kwa damu yake
Amenipa amani
Amenipa uzima
Mbinguni ninaenda
1. Nina haja nawe kila saa,hawezi mwingine kunifaa
(Chorus)
Yesu nakuhitaji,vivyo kila saa
Niwezeshe mwokozi nakujia x2
2. Nina haja nawe kaa nami, na maonjo haya hayaumi
Nina haja nawe kila hali, Maisha ni bure uli mbali
3. Nina haja nawe nifundishe,na ahadi zako zifikishe
Nina haja nawe mweza yote ni wako kabisa siku zote
(Chorus) x2
1. Kumtegemea mwokozi kwangu tamu kabisa
Kukubali neno lake nina raha moyoni x2
(Chorus)
Yesu Yesu namwamini nimemwona thabiti
Yesu Yesu yu thamani ahadi zake kweli x2
2. Kumtegemea mwokozi kwangu tamu kabisa
Kuamini damu yake nimeoshwa kamili x2
3.Kumtegemea mwokozi kwangu tamu kabisa
Kwake daima napata uzima na amani x2
4. Nafurahi kwa sababu nimekutegemea
Yesu mpendwa na rafiki uwe name dawamu. x2
(Chorus) x3
Yesu kristo (habadiliki)x3
Yesu kristo habadiliki, habadiliki sasa na milele
Ooh halleluya (halleluyax3)
Roho wake (habadiliki)x3
Roho wake habadiliki, habadiliki sasa na milele
1. Mimi naifanya kazi yake mungu kwa bidii sana sijui ya kesho x2
(Chorus)
Nachuchumilia kumwona bwana pamoja na wateule wote
Malaika wakiwa tayari kunilaki mimi mawinguni x2
2. Kwa vile sijui ni wakati gani bwana ataniita sichezi na dhambi.
(Chorus)
instruments
(Chorus)
Sol 1 (Gent) Sol 2 (Lady)
1. Sol 1: Utukuzwe
All: Utukuzwe
Sol 1: Yesu
All: Utukuzwe, utukuzwe
Sol 2: Utukuzwe
All: Utukuzwe
x2
2. Sol 2: Aokoa
All: Aokoa
Sol 2: Huyu Yesu
All: Aokoa
Sol 2: Aokoa
All: Aokoa
Sol 2: Aokoa
All: Aokoa
3. Sol 2: Anaponya
All: Anaponya
Sol 2: Bwana Yesu
All: Anaponya
Sol 2: Anaponya
All: Anaponya
Sol 2: Anaponya
All: Anaponya
4. Sol 2: Abariki
All: Abariki
Sol 1: Yesu
All: Abariki
Solo 2: Abariki
All: Abariki
Sol 2: Abariki
All: Abariki
5. Sol 1: Anaweza
All: Anaweza
Sol 1: Yesu
All: Anaweza x2
Sol 2: Anaweza
All: Anaweza
Sol 2: Huyu Yesu
All: Anaweza
Sol 2: Anaweza
All: Anaweza
Sol 2: Anaweza
All: Anaweza
6. Sol 2: Afungua
All: Afungua
Sol 2: Bwana Yesu
All: Afungua
Sol 2: Afungua
All: Afungua
Sol 2: Afungua
All: Afungua
1. Bwana Mungu kaumba Yerusalemu, mji wa amani tena wenye furaha
Waishio Yerusalemu wana furaha x2
Katika mji huo hakuna njaa wala kilio
Mungu pia kawapa maisha mema tena marefu x2
(Chorus)
(Uzima x2 baraka x2, Uwe navyo vyote maishani daima) x2
Ndiyo ahadi aliyowapa watu wa yerusalemu x2
2. Ewe mkristo uliyeokolewa umewekwa yerusalemu mji mpya
Jitahidi usichafue mji huo x2
Acha uovu wako uwe msafi maisha yako, uishi na amani mji mzuri yerusalemu x2
(Chorus) x2
1. Tumaini lako lote liweke kwa kristo Yesu
(Maana yeye ndiye) mkombozi wa ulimwengu
(usichoke kuomba,unapopata shida)amimi kupona
Mkombozi Yesu ndiye mwisho wa mateso yote muamini yeye
(Chorus)
Ewe ndugu yangu sasa usiwe nayo hofu
Mkombozi yesu yuko tayari kukuokoa x2
2. Je una lipi gumu asiloliweza Yesu
(kama ni magonjwa) yeye ni tabibu wa kweli
(usikate tama,katika shida zako) Yesu akuita
Akupe amani yako uliyonyang’anywa naye muovu shetani
3. Kwa kupigwa kwake Yesu twaonywa mateso yetu
(Tunayoyapata) kwa ajili ya dhambi zetu
(Achana na dunia, mkaribie yesu) mshinde shetani
Uzima uko kwa Yesu baraka ziko kwa Yesu muamini yeye
(Chorus)
Instruments
(Chorus)
1. Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe daima
(mapenzi yatimizwe ulimwenguni hata milele)x2
2. Utupe leo riziki yetu, utusamehe na dhambi zetu
(Kama vile sisi tunavyosamehe kila tumuae) x2
3. Usitutie majaribuni, tuokoe a yule mwovu
(Tushinde na hata kila jaribu tunakuomba) x2
4. Utukufu ni wako daima, Hakuna kitokanaco na sisi
(Hatuwezi tukajuna kabisa vyote ni vyako.) x3
1. (Kama dhambi) – ingekua ni bahari
(Watu wengi)- wangekuwa wamechoka kuogelea
2. (Dhambi ya wizi)- ingekuwa ni bahari
(waizi wengi)- wangekuwa wamechoka kuogelea
3. (Dhambi ya kunywa pombe)- ingekuwa ni bahari
(watu wengi)- wangekuwa wamechoka kuogelea
4. (Dhambi ya utapeli)- ingekuwa ni bahari
(watu wengi)- wangekuwa wamechoka kuogelea
5. (Dhambi ya uzinifu) – ingekuwa ni bahari
(watu wengi)- wangekuwa wamechoka kuogelea
6. (Dhambi ya usherati)– ingekuwa ni bahari
(watu wengi)- wangekuwa wamechoka kuogelea
7. (Dhambi ya kudanganya) – ingekuwa ni bahari
(wadanganyao)- wangekuwa wamechoka kuogelea
8. (Dhambi ya kusengenya) – ingekuwa ni bahari
(wasengenyao)- wangekuwa wamechoka kuogelea
(Yesu mwokozi wa maisha yako nyosha mkono atakuokoa
Usife maji na hali mwokozi yuko tayari ili akuokoe) x2
Sol : All
(Wacha wizi) – hiyo ni dhambi
(Wacha kudanganya) – hiyo ni dhambi
(Ukija kwa mungu uache uzinifu) – hiyo ni dhambi
(Ukipenda yesu uache usherati) – hiyo ni dhambi
(Wacha na uongo) – hiyo ni dhambi
(Wacha masengenyo) – hiyo ni dhambi
(Ndugu yangu uache kudanganya) – hiyo ni dhambi
(Ewe mwenzangu uache na sigara) – hiyo ni dhambi
(Wacha na tumbaku) – hiyo ni dhambi
(Wacha na uchawi) – hiyo ni dhambi
1. Sisi tuwateule wateule wa mungu katuchagua tuwe mabalozi
Mungu ndiye ni baba tena ndiye nfalme nasi tu wana wana wateule.
2. Twazijua sheria za kwetu ju nyumbani katueleza nasi twazifata
Nasi twamwakilisha hapa duniani twayaongea yale ya mbinguni.
3. Kama kwetu ni juu hizi ndizo sheria sitende dhambi tumikia mungu
Sawasawa balozi zitetee sheria za kwetu juu hapa duniani.
4. Huo ndio ni wito kwa aliyebalozi inampasa pate takasika
Ndivyo tulivyoitwa tuyatende mema na ndiyo lugha ya kwetu mbinguni.
(Chorus) : Hatukuitiwa hatukuitiwa uchafuu
Sol: Tuliitiwa-tuliitiwa –‘’ wokovu,
"""""""""""""""""""""""""- kupona,
"""""""""""""""""""""""""- Baraka,
""""""""""""""""""""""""""- Amani,
""""""""""""""""""""""""""- Mbinguni
Sol: Hatukuitiwa hatukuitwa uchafuu
(Chorus) x5
(Chorus)
Basi nasema sasa enendeni katika roho wala hamta timiza kamwe tamaa za mwili x2
Zitwae nguvu za roho wake akushindie x2
1. Sol -Enyi wazinzi hata sasa hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni adui wa Mungu x2
2. Sol -Ona upendo wake yesu ulivyo wa ajabu kajitolea mwanadamu upate okolewa x2
3. Sol -Ee mwanadamu yesu aona una thamani jione sasa kama yesu alivyokuona x2
Acha x5
Sol:
(Wizi,uongo,uzinifu ni dhambi acha kabisa)
(Ufidhuli,kutotii,kiburi ni dhambi acha,acha mara moja)
(Masengenyo,manung’uniko,vita vyote ni vyangu acha kabisa)
(Mgeukie Mungu wako,akusamehe akujaze roho wake upate kuwa huru kabisa)
1. Yampasa muongofu (afanyike) kuwa mwana wa Mungu x2
Ili afanyke mwana wa mungu ajizoeshe baba anavyotaka x2
2. Yampasa muongofu (afanyike) kuwa kiumbe kipya x2
ya kale yapita natazameni ni mapya sasa naye atapendeza x2
3. Yampasa muongofu (kua na amani) na watu wote x2
Kuwa na amani ni kutulia katika mema kumpendeza Mungu x2
4. Yampasa muongofu (kushiriki)shwa naye Baba Mungu x2
Awasiliane na baba mungu kwenye maombi akiwa na furaha x2
5. Yampasa muongofu (kuwa nayo) haki ya kupona x2
Hawezi kuteseka na magonjwa kwenye wokovu kama ametakaswa x2
Sol 1 (Gent) ; Sol 2 , Sol 3 (Lady)
(Chorus)
Uwezo-uwezo wa damu yake Bwana Yesu x2
Yaponya- yaponya magonjwa yatakasa dhambi x2
Damu ya Yesu ni ta-takatifu x2
Alizaliwa kwa uwezo wa roho mtakatifu x2
Sol 1: (Bikira kapata mimba kwa uwezo wa roho)
All : Na Yusufu hajamkaribia Mariamu
Sol 2: (Malaika kamtokea yusufu kamwambia)
All : Mimba hiyo ni kwa uwezo wa roho mtakatifu
Sol 3: (Basi Yesu ni mwana wa Mungu na damu yake si ya Yusufu)
All : Ni damu iliyotakatifu ni damu safi isiyo hatia ) x2
(Chorus)
Sol 1: (Kama damu ya Yesu ingekua ya kawaida)
Damu ya Yusufu mwanadamu mwenye hatia
Sol 2: (Isingetakasa dhambi na kuponya magonjwa)
Jamani tungeangamia tungeangamia
Sol 3: (Ona damu hiyo yake Yesu inao uwezo hata sasa)
Ni damu yake aliye hai, Mungu tumwaminiye yupo x2
(Chorus)
Uwezo-uwezo wa damu yake Bwana Yesu x2
Yaponya- yaponya magonjwa yatakasa dhambi x2
Damu ya Yesu ni ta-takatifu x2
Alizaliwa kwa uwezo wa roho mtakatifu x4
1. Neno lake baba mungu haliwezi kukaa na kishetani mahali popote pale x2
Utaliona hilo neno likipigana na kishetani mpaka lilishinde vita x2
2. Sanduku la sheria za mungu halikuweza kukaa naye dagoni mungu wa wafilisti x2
Kulipokucha kumbe dagoni alianguka na kukatika vitangaa vya mikono yake x2
3. Ikiwa nawe ndugu yangu umeshindwa na adhambi au magonjwa kubali nano lake Yesu x2
Ukiliweka moyoni mwako litaziuwa nguvu za dhambi magonjwa nayo yatapona x2
1. Ndugu yangu umeshakata bima ya maisha kwa ajili ya kesho yako usiyoijua yakupasa kuwa tayari kwa shida ya kesho wakati ambapo huwezi kujisaidia x2
2. Mkurugenzi wa kampuni wa bima yako Bwana Yesu aliyemwaga damu ya thamani ili wewe usiteseke na shida yoyote ambayo shetani ataileta huko kwakox2
3. Ukitoa sadaka zaka matoleo yote wajiunga na kampuni yahiyo bima umasikini ujapo kwako magonjwa yote Yesu asimame apige vita hivyo vyote x2
1). Sadaka yako toa sasa uone yesu hivi sasa.
2). Na zaka yako toa sasa uone yesu hivi sasa.
3). Kipawa chako toa sasa uone yesu hivi sasa.
4). Mwana wa Mungu Bwana Yesu sio dhalimu asilipe.
5). Toa kamili kwake mungu shida ijapo hebu muite.
6). Na dhambi zako tubu sasa uone Yesu hivi sasa.
7). Tenda mapenzi yake Mungu shida ijapo hebu muite.
(Utaokoka x3)x2
1. (Ewe mtu wa nungu)- utahubiriwa mpaka lini, (fahamu) hila za mwovu shetani (Utii) maagizo yake muumba.
2. (Shetani huonyesha)- upande mmoja wa maisha, (hawezi) kukuonyesha ubaya (wadhambi) atakayo uitende.
3. (Hebu mpinge pepo)- kama bado yeye yuko mbali, (simruhusu) akusongelee,(na wala) asikukaribie kamwe.
4. (Jizoeshe kudumu)- katika neno la baba mungu, (mazungumzo) machafu uache, (daima) dumu kwa neno la kristo.
(Chrorus)
Utakatifu tudumishe, utakatifu tudumishe
Sol:
1. Utakatifu~
Na kanisani-tuabudupo,
na washirika-tuaminio,
na wanakwaya-tunapoimba,
nawahubiri- tuhubiripo
2. Utakatifu~
kila mahali,
hata sokoni-biasharani,
pia shambani-tunapolima,
hata shuleni- tunaposoma,
nasafarini- ndani ya gari
1. Sol: ( Wapendwa dhambi ilitutenga mbali na Mungu,hatukuweza kuwasiliana naye
Lakini tunayo hati-jina la Yesu lituwezeshayo kupata kila tuombalo.
All: Tunapomaliza maombi tunasema
Katika jina la Yesu mwokozi Amen
(Chorus
Jina hili Yesu lina uwezo,pepo hutoroka,alisikiapo jina la Yesu
2. (Kila tunapokemea shetani twatumia jina hili Yesu
Kwa sababu jina hili Yesu ndilo lenye nguvu na uwezo mwingi kabisa)
All: Tunapokemea shetani twatumia
Jina hili Yesu kwani linazo nguvu
(Chorus
Jina hili Yesu lina uwezo,pepo hutoroka,alisikiapo jina la Yesu
3. Sol: (Bila jina hili Yesu pepo hawezekani kabisa
Ita jina la Yesu kila uwapo mashakani)
All: Bila jina Yesu,pepo hawezekani
Ita jina Yesu uwapo mashakani
(Chorus
Jina hili Yesu lina uwezo,pepo hutoroka,alisikiapo jina la Yesu
Sol 1 (Lady) : Sol 2 (Gent)
1. Sol 1: (Mungu)
All: Wa ibrahimu isaka na yakobo ndiye tunamwabudu hakuna Mungu mwengine x2
(ndiye tunamuabudu hakuna Mungu mwengine).
2. Sol 1: (Ndiye)
All: Wa Shedraki, Meshaki, Abedinego ndiye wa Danieli na nabii Eliya x2
(ndiye tunamwabudu hakuna Mungu mwengine)
3. Sol 1: (Fanya)
All: Maajabu kwa walio jipa majina tena haikutosha na dhambi kaikataa
(ndiye tunamwabudu hakuna Mungu mwengine)
4. Sol 2: “(Shedraki na Meshaki naye Abedinego hata na Danieli walikataa dhambi kusujudu mfalme, kuabudu sanamu mungu kawaokoa na tanuru na simba, nawe unaabudu dhambi unazitenda tena wajivunia maajabu ya Mungu,
Hao ndio miungu wanaruhusu dhambi watenda muijiza nawe wadanganyika, Elisha akatoboa siri akafichua, kaita uko wapi ee mungu wa Eliya, siri ni ya Elisha mungu ndani ya mtu mungu wa uko wapi nawe utaokoka)”
Sol 1 : All
(i) Ni Mungu wa Yakobo –(Chorus)
All: ni Mungu wa Elisha ndani ya mama mwanzilishi kwa mkono wa mjumbe ndiye tunamwabudu
(ii) Ni Mungu wa Danieli"""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""
(iii) Ni Mungu wa Isaka""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""
(iv) Nani asiyejua x2""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""
(v) Nasi tuimbe sana""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""
(vi) Upepo utavuma"""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""
(vii) Hata dunia ipasuke"""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""
(viii) Milele tutaimba"""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""
Ni Mungu wa mjumbe - ndiye tunamuabudu x2
Mungu asiyetaka dhambi - """"""""""""""""""""x2
Mungu wa msamaha -"""""""""""""""""""""""""x2
(Chorus)
Heri wamgojeao Bwana, maana hawatachoka,maana hawatazimia
Watapewa nguvu, nguvu, nguvu mpya. x2
1. Umngojee bwana kwa kupenda watu
2. Umngojee bwana kwa kumtolea
3. Umngojee bwana kwa utakatifu
4. Umngojee bwana katika maombi
Bwana atakupa nguvu kwenya kupenda watu
Bwana atakupa nguvu kwenya kumtolea
Bwana atakupa nguvu kwenya utakatifu
Bwana atakupa nguvu kwenya maombi yako
Sol : ”(Ni makosa kusema unamngojea Bwana na huku una nia mbili moyoni mwako
Unapendezwa na chuki,uzinifu,ulevi, manung’uniko,ibada za sanamu,na huku unadai mambo mengi kutoka kwa kristo Yesu, utachoka,
(Nguvu mpya zakukupa haja za moyo wako hazitakuja ni heri kuamua kuzaliwa upya kaika roho
Na lolote utakaloomba kutoka kwa bwana utapata)”
Bwana atakupa nguvu kwenya kupenda watu
Bwana atakupa nguvu kwenya kumtolea
Bwana atakupa nguvu kwenya utakatifu
Bwana atakupa nguvu kwenya maombi yako
(Chorus)
Ooh shangwe leo,shangwe leo
Ooh shangwe leo, kwa harusi yenu
Ahadi ya mungu mwatimiza(leo) kuwa kitu kimoja kwa pendo
Kuvumilia kwenu si bure(kweli) matokeo yake twayaona
Maisha yenu yawe ni mema(kweli)) ni ushuhuda kwetu sote
Twawaombea Baraka zake (Mungu) mjaliwe amani nyumbani
Dada eeh tunakupa kwaheri ,uendako ukawe na amani
-Wazazi wako wote walikupenda sana na sasa imebidi wakupe kwaheri
-Kaka na dada zako walikupenda sana na sasa imebidi wakupe kwaheri
-Majirani rafiki walikupenda sana na sasa imebidi wakupa kwaheri
Leo ni siku yenye furaha,kwetu na kwako kijana
Kwa kuyavumilia yote,mmetimiza ahadi
-Ni mengi sana umeyaona yenye kuvunja moyo
Nawe kasimame imara katika kuongozwa
-Maisha haya wayaendea ya amani na Baraka
Uutumishi kaudumishe kwa moyo wako wote
1. Heko twawapongeza ninyi mnaoowana, hata kwa wazazi ni heshima kuu x2
2. Heko twawapongeza ninyi mnaoowana, hata kwa kanisa ni heshima kuu x2
3. Heko kwa utiifu ninyi mnaoowana, kwa waongozao ni heshima kuu x2
4. Heko kwa ushindi ninyi mnaoowana, hata na mbinguni ni furaha kuu x2
5. Heko kuvumiliana ninyi mnaoowana, na dunia nzima imewatambua x2
6. Amani hii iwe na nyinyi muendako mkilidumisha neno la muumba
Shangwe shangwe, kwenu jamani,kwa kutimiza ahadi x7
1. Sasa mmefunga ndoa,nasi twashangilia
Mungu ni shahidi wenu,mpendane kwa upendo x2
(Chorus)
Siku ya furaha leo yenye heri na salama
Kwa furaha na amani ni pambo la nyumbani x2
2. Kaka yetu yakumbuke mapatano ya ndoa
umpende na mkeo umlinde daima x2
3. Dada yetu kazi yako heshimu mume wako
Utiifu na maonyo Baraka za nyumbani x2
(Chorus) x3
1. Furaha leo kwa kuitimiza siku ya pili ya maisha x2
(Chorus)
Sasa mmefunga ndoa siku hii ya harusi x2
Yanpasa mjue sasa mkitu kimoja x2
2. Ahadi yenu mmeitimiza siku ya leo ya harusi x2
(Chorus)
Sasa mmefunga ndoa siku hii ya harusi
Yanpasa mjue sasa mkitu kimoja
3. Mungu wetu awaimarishe mkidumisha utakatifu x2
(Chorus)
Sasa mmefunga ndoa siku hii ya harusi x2
Yanpasa mjue sasa mkitu kimoja x3
Mungu mulika vijana hawa, kwani tayari wako mlangoni
Pingu za mikononi wameshika, funguo za maisha yao
Maisha haya ni ya milima, mabonde pia hata majaribu
Uchangamfu ndio ngao yao, ee bwana hilo wajalie
Uvumilivu na kupendana, heshima pia kuaminiana
Mlinde sana haya msiache, unyumba ukawe imara
Eeh Mungu uwabariki, huyu bwana na bibi harusi
Katika maisha yao
1. Tuingojea kwa tumaini siku ya leo,imewaadia
Twamsifu mungu kwa huyu bwana na bini harusi,siku hii ya leo
(Chorus)
Leo ni furaha kuu kuiona harusi yenu
Mungu awabariki mkaishi kwa amani ×2
2. Maisha mema nyumbani mwenu ni ushuhuda,kwa watu wote
Mapenzi yenu yatoka mwanzo yaendelee, kwa wakati wote
3. Baba na mama mpeni kwaheri leo aenda,nyumbani kwake
Msiwe na hofu mtoto wenu leo apata , masikani mapya
Mungu baba ilikupendeza, kuumba mbingu na nchi
Na vitu vyote tunavyoviona katika ulimwengu huu
Hivyo hivyo ilikupendeza kuumba mtu kama wewe
Uliumba Adamu mzuri,ukaumba na Hawa pia
Tena baba ilikupendeza kuumba vijana hawa
Ambao sasa wanaitimiza, ahadi ile ya kwanza
Sasa baba tunakuomba wabariki vijana hawa
Na vitu vyote utakavyowapa katika unyumba wao
-shangwe tufurahi kwa siku hii ya leo
1. Mtu wa kwenu amepatikana Na mabaya aombe
Anao moyo wa kuchangamka Na aimbe zaburi
Amekuwa hawezi na awaite Wazee wa kanisa
Na wamuombee na kumpaka mafuta Kwa jina la Bwana
Na kule kuomba kwa imani kutomuokoa mgonjwa Yule.
(Chorus)
(Na Bwana ataimuinua), - atamuinua, atamuinua
(Na kama amefanya dhambi), - atasamehewa, atasamehewa x2
2. Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi na kuombeana
Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, kiomba kwa bidii.
(Chorus) x2
Sol : All
Atasamehewa baba, Atasamehewa mama - Mmmh x3, atasamehewa
Atasemehwa x2 baba - mmmmh x3, Atasamehewa
Mama atasamehewa - mmmmh x3, Atasamehewa
Atasamehewa ndugu Atasamehewa dada - Mmmh x3, atasamehewa
Atasemehwa x2 ndugu - mmmmh x3, Atasamehewa
Dada atasamehewa - mmmmh x3, Atasamehewa
(Mmmh x3, atasamehewa) x2
1. Shika sana ulichonacho,asije mtu akakupokonya
Imani ile ya kwanza uitunze kama kwanza. x2
(Chorus)
Kwani sasa umefanikiwa usibaki kujivunia
Bali ujilinde ukichunguza kutokaribisha la uchafu
Na shetani ajapo umpinge
2. Mafundisho pia maonyo,linda sana ulivyopokea
Kwani shetani yu macho,ili akuhuzunishe.
(Chorus) x2
1. Neno lake Muumba wetu, alilonena muhubiri
Lidumu ndani yetu nyote. x2
(Chorus)
(i) Neno limehubiriwa, nanyi mmeshasikia
Fundisho la unabii, la maisha yenu mapya x2
(ii) (Mliweke mioyoni mwenu), -liwe ngao ya ushindi
(Liwafae maisha yenu), -siku zote za maisha x2
2. Roho wa Bwana amenena, yote ya maisha yenu
Msipoteze hata neno. x2
(Chorus) x2
1. Dunia inayumbayumba, dunia imetiwa giza, dunia inatingisika, yateleza, haikanyagiki x2
2. Dunia imetekwa nyara, mfaume amekuwa shetani, majeshi yake amemwaga yapigana na watu wa Mungu. x2
3. Kuna vita kati ya ndugu, makanisa kuchukiana na uasi kuhalalishwa, dhihirisho Yesu anakuja x2
4. Ee mkristo mtu wa Mungu shika sana ulichonacho, mwovu asijekupokonya, ufaume umekaribia x2
(Chorus)
Ewe Yesu, nakuomba, nishike mkono nipe nguvu,uniepushe na majaribu yanayosonga imani yangu
Nipe nguvu mpya, nipe nguvu mpya , niwe imara daima x2
1. Nataka nimjue Yesu, na nizidi kumfahamu
Nijue pendo lake na wokovu wake kamili
(Chorus)
Zaidi, zaidi, nimfahamu Yesu
Nijue pendo lake na wokovu wake kamili
2. Nataka nione Yesu, na nizidi kusikia
Anenapo kitabuni kujidhihirisha kwangu
3. Nataka nifahamu na,nizidi kupambanua
Mapenzi yake nifanye yale yanayompendeza
4. Nataka nikae naye,kwa mazungumzo zaidi
Nizidi kuwaonyesha wengine wokovu wake.
(Chorus) x2
1. Yampasa muongofu (afanyike) kuwa mwana wa mungu
Ili afanyke mwana wa mungu ajizoeshe baba anavyotaka
2. Yampasa muongofu (afanyike) kuwa kiumbe kipya
ya kale yapita natazamini ni mapya sasa naye atapendeza
3. Yampasa muongofu (kua na amani) na watu wote
Kuwa na amani ni kutulia katika mema kumpendez mungu
4. Yampasa muongofu (kushiriki)shwa naye baba mungu
Awasiliane na baba mungu kwenye maombi akiwa na furaha.
5. Yampasa muongofu (kuwa nayo) haki ya kupona
Hawezi kuteseka na magonjwa kwenye wokovu kama ametakaswa
1. Neno lake baba Mungu haliwezi kukaa na kishetani mahali popote pale
Utaliona hilo neno likipigana na kishetani mpaka lilishinde vita
2. Sanduku la sheria za Mungu halikuweza kukaa naye dagoni Mungu wa wafilisti
Kulipokucha kumbe dagoni alianguka na kukatika vitangaa vya mikono yake
3. Ikiwa nawe ndugu yangu umeshindwa na adhambi au magonjwa kubali nano lake Yesu
Ukiliweka moyoni mwako litaziuwa nguvu za dhambi magonjwa nayo yatapona.
( Wapendwa dhambi ilitutenga mbali na Mungu,hatukuweza kuwasiliana naye
Lakini tunayo hati-jina la Yesu lituwezeshayo kupata kila tuombalo.
1.Tunapomaliza maombi tunasema
Katika jina la Yesu mwokozi Amen
Jina hili Yesu lina uwezo,pepo hutoroka,alisikiapo jina la Yesu
(kila tunapokemea shetani twatumia jina hili Yesu
Kwa sababu jina hili Yesu ndilo lenye nguvu na uwezo mwingi kabisa)
2. Tunapokemea shetani twatumia
Jina hili Yesu kwani linazo nguvu
(Bila jina hili Yesu pepo hawezekani kabisa
Ita jina la Yesu kila uwapo mashakani)
3. Bila jina Yesu,pepo hawezekani
Ita jina Yesu uwapo mashakani
1. (Hii ndiyo siku yetu) tuliyoingoja kwa raha, (kuwakaribisha nyote) kwa harusi takatifu
(Chorous)
Tulidhani haitafika na leo imewasili
2. (Tazameni kaka yetu) ameshapata mkewe,(Baraka za Mungu wetu) mkaishi kwa amani
3. (Wazazi wa bi harusi) leo mpeni kwaheri,(msipatwe na majonzi) hicho ndicho kimungu
(Chorous)
Dada eeh tunakupa kwaheri ,uendako ukawe na amani
1. -Wazazi wako wote walikupenda sana na sasa imebidi wakupe kwaheri
2. -Kaka na dada zako walikupenda sana na sasa imebidi wakupe kwaheri
3. -Majirani rafiki walikupenda sana na sasa imebidi wakupa kwaheri
1. -Leo ni siku yenye furaha,kwetu na kwako kijana
Kwa kuyavumilia yote,mmetimiza ahadi
2. -Ni mengi sana umeyaona yenye kukuvunja moyo
Nawe kasimame imara katika kuongozwa
3. -Maisha haya wayaendea ya amani na Baraka
Utumishi kaudumishe kwa moyo wako wote
(Chorous)
Sisi sote twakupongeza,sisi sote twakuongeza
Sisi sote twakupongeza,heko kwako kijana
1. -Mungu amechagua siku hii,iwe siku ya ndoa na harusi
Siku ya shangwe na vigelegele,iwe siku ya ndoa na harusi
2. -Ukae ni ua la kupendeza,milele pia hata milele
Ukawe ua zuri la urembo,milele pia hata milele
3. -Ukawe ni faraja kwa mwenzio,milele pia hata milele
Ukawe msaada kwa mwenzio,milele pia hata milele
(Chorous)
Sasa umefikia daraja la maisha, vuka ng’ambo ya pili maisha ya wawili
1. -Twawaona maharusi hawa wamepambika na wapendeza
2. -Ni furaha hata juu mbinguni na duniani twashangilia
3. -Lolote lisiwatenganishe kwani sasa mkitu kimoja
4. -Mambo ya kigeni siwateke neno la mungu linawatosha
(Chorous)
Siku ya leo twawashangilia, Bwana na bibi harusi hongera
1. Eeh mtakatifu, ewe Bwana Mungu wetu
Twahitaji Baraka kwa vijana hawa walio mbele zetu
Watangulie maishani x2
(Chorus)
Mimina amani,mimina upendo
Wabariki, wafanikishe, maishani x2
2. Uwape kudumu katika utakatifu
wape uvumilivu neno baya lolote litakapo kuja
Upendoni mwako wadumu x2
(Choru)
Chorou
Ni shangwe,ooh nishangwe
Heko kwenu maharusi,mungu na awatukuze
Wote waseme amina x2
1. Sol: Sasa mmekwisha timiza yaliyo mapenzi ya mungu
Kwani hii ndiyo ahadi mungu aliyoiweka
All:"""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""
(Chorus) x2
2. Sol: Maishani mwenu mjue,neno lake mungu silaha
Kwa moyo nanyi mlishike,majaribu mtashinda
All:""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""
(Chorus) x2
3. Sol: Heshima pendo mdumishe kutii maonyo mshike
Unyumbani mwenu daima,na furaha mtapata
All: """""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""
(Chorus) x3
1. Mungu mulika vijana hawa, kwani tayari wako mlangoni
Pingu za mikononi wameshika, funguo za maisha yao x2
Chorous
Eeh Mungu uwabariki, huyu Bwana na bibi harusi
Katika maisha yao x2
2. Maisha haya ni ya milima, mabonde pia hata majaribu
Uchangamfu ndio ngao yao, ee Bwana hilo wajalie x2
3. Uvumilivu na kupendana, na pia kuaminiana
Mlinde sana haya msiache, unyumba ukawe imara x2
(Chorus) x2
1. Mungu baba ilikupendeza, kuumba mbingu na nchi
Na vitu vyote tunavyoviona katika ulimwengu huu
2. Hivyo hivyo ilikupendeza kuumba mtu kama wewe
Uliumba Adamu mzuri,ukaumba na Hawa pia
3. Tena baba ilikupendeza kuumba vijana hawa
Ambao sasa wanaitimiza, ahadi ile ya kwanza
4. Sasa baba tunakuomba wabariki vijana hawa
Na vitu vyote utakavyowapa katika unyumba wao
Chorous
-shangwe tufurahi kwa siku hii ya leo
1. Yesu alikwenda mlima wa mizeituni
Kakesha kuomba kwa baba Mungu, kikombe cha mauti kimwepuke
Chorous 1
Yuda mwanafunzi alimsaliti
(Lakini Bwana Yesu alimwamini Mungu)
Kwamba atafufuka, Nasi atufufue ifikapo siku ya mwisho
Ya hukumu kwa ulimwengu
2. Yesu alipofika mbele ya pilato, akawa hata hana hatia
Pilato kasema afunguliwe
3. Yesu kasema kwamba mtasalitiwa majaribu hayana budi
Jipeni moyo nanyi mtashindA
Chorous 2
Yuda mwanafunzi akikusaliti
(Lakini yatupasa kumuamini Mungu)
Ila atufufue toka majaribuni
Ifikapo siku ya mwisho
Ya hukumu kwa ulimwengu
1. Bwana Yesu alikufa kwa dhambi za watu
Alimwaga damu yake kwa dhambi za watu
Chorous
(Amini) baba, mama usamehewe kwa damu ya Yesu
(Amini) ndugu, dada usamehewe kwa damu ya Yesu
2.Yesu aliyaponya magonjwa yote ya watu
Kupigwa kwa bwana Yesu kwayapoya magonjwa
3. Mali zote za dunia ni zake baba Mungu
Utajiri wa ukwasi ni wake baba Mungu
1. Bwana Yesu ameshafufuka, kaburini ametoka
ushindi umeshapatikana, mwokozi amefufuka
Chorous
Furaha kubwa kwetu sisi wanadamu
Kwa kufufuka kwake mwokozi
Kifo mauti navyo vimekwisha shindwa
Kwa kufufuka kwake mwokozi
Twende mbele, tufufuke toka dhambini
2. Walinda, kaburi mashahidi wathibitisha ushindi
Kwa kufufuka kwake mwokozi, tumeupata ushindi
1. (Hebu litazameni kaburi
Bwana Yesu hayumo kaburini)
(Kweli) ameshafufuka
Chorous
Ametoka Bwana kaburini
Kifo mauti vimeshindwa sasa Bwana Yesu
Amekaa juu mbinguni
Kwa baba.
2. (Naye Mariamu Magdalena
Likwenda kulitazama kaburi)
(Kakuta)amefufuka
3. (Kampe nafasi moyoni mwako
Apate kukufufua kabisa)
(Kutoka) katika dhambi.
(Sop) Huzuni kwa mwokozi Yesu
(All) Akisulibishwa
(Sop) Tazama anasononeka,
(All) Pale juu ya mti
Makofi apigwa mbavuni achomwa mkuki
(Tenor) Wakamvika,
(All) Taji yenye miiba
Wayahudi wale walimdhihaki mwokozi
(Tenor) Kweli mwokozi, kapata mateso.
Yote haya ni wewe na mimi tuokolewe
Tuachane na dhambi tusimsulubishe tena
(CHORUS)
Yeye Bwana katoa hakikisho, Kwetu sisi viumbe wake, Maji na damu ilivyomwagika, dhambi zetu kaziondoa. x2
(Sop) Ushindi kwa awaye yote
(All) Anayemwamini
(Sop) Mateso aliyoyapata
(All) Bwana wetu Yesu
Tukimkaribia naye takukaribia
(Tenor) Katika shida
Tunazozipata.
Kwenye msalaba, yeye alimaliza yote
(Tenor) Uhakikishe
Humsulubishi
Ukirudia dhambi unamsulubisha tena
Sifanye hivyo ndugu kosa kubwa kwako wewe.
(chorus)instrumental
(chorus) x2
1. Ni mashindano ya wayahudi
(hawakuamini ya kua Yesu alitumwa na
Mungu kuwaokoa)
Ni mashindano ya wayahudi yaliyomsulibisha Yesu mwokozi
Mashindano, mashindano, mashindano yaliyomsulubisha mwokozi
2. Ni mashindano ya Israeli
(hawakuamini ya kua Musa alitumwa na
Mungu kutuokoa)
Ni mashindano ya Israel yaliyowaangamiza kule jangwani
Mashindano, mashindani, mashindano yaliyowaangamiza jangwani.
3. Ni mashindano yatufanyayo
(hatuamini a kua mjumbe amesimamishwa na
Mungu kutuongoza.)
Ni mashindano yatufanyayo kunena juu ya roho ili tuangamie
Tuyaache mashindano, tuyaache na tutamshinda yule shetani
Chorous
Tuvae, upendo
Tuwe na umoja
Napia heshima
Haya yote yatakua ni yetu
1. Katika mlima ule usiku wa manane(Huo)
Yesu mwana wa Mungu kakesha kuomba
Kesheni kuomba enyi wateule kwaja majaribu
Chorous
Fufuka amefufuka
Yesu mwana wa Mungu ameshafufuka
2. Kama kitambo kidogo usingizi mzito( Huo)
Yesu mwana wa Mungu kasema amkeni
Kesheni kuomba enyi wateule kwaja majaribu
3. Ulifika wakati kaja msalaba(Huo)
Yesu mwana wa Mungu kashinda mauti
Kesheni kuomba enyi wateule kwaja majaribu
4. kilima kando ya mji kaangikwa mtini(Huo)
Yesu mwana wa Mungu kasema imekwisha
Kesheni kuomba enyi wateule kwaja majaribu
1. Bwana Yesu amefufufka
Kaburini ametoka
Yuko hai kwa baba
Juu mbinguni,
Shangilieni
Kwani ni mshindi yu hai kwa baba
2. Tetemeko lilitokea
Na walinzi wote chini
Yuko hai kwa baba
Juu mbinguni
Shangilieni
Hata na mapepo wote waogopa
3. Atokea wanafunzi,
Na Amani,iwe kwenu
Yuko hai kwa bab
Juu mbinguni
Shangilieni
Ndiye mfalme wa Amani yote
Sol: (Mjumbe awaye yote anao ujumbe ametumwa)
All: Basi nasi tumekua naye mjumbe wa Bwana
Sol: (Ni wengi liomsikia na wengine wenu kumuona)
All: Je wote mmekwisha keti na kujiuliza
Sol: (Je ni ujumbe gani huu aliotuachia mjumbe wa Bwana kutoka juu)
(Chorus)
All: Bado hujachelewa sana waweza kuamua,
Sol: (Kuamua)
All: Mungu kamwe hatafanya suluhu na wenye dhambi,
Sol: (Dhambi)
All: Katika ule ufalme wake.
Sol: (Wakati)-wakati ni sasa kwa hakika makao yako tayari x2
Sol: (Kama ilivyokua wakati ule wake Nuhu, alivyotumwa na Mungu ajenge safina, hawakuamini aliyoyasema ni kweli isitoshe pia walimdhihaki, nakatika muda wa miaka mia ishirini, aliweza tu kushawishi wa nyumbani mwake,ijapo watu walikuwa na mioyo migumu, hilo halikubadili kusudi la Mungu)
1. (Hata sasa hujaamini bado,kutokuamini hakutobadili kusudi la Mungu)
Sasa amekusudia kuiadhibu dhambi kwa wote waitendao
2. (Kama siku saba za neema wakati wa Nuhu hazikuweza kuwafaa kitu)
Sasa huu ndio wakati ule wa neema kwako amua usije angamia
(Chorus)
3. (Ndugu yangu jehanamu ipo kama Yule tajiri alivyoomba Lazaro atumwe)
Kwamba akawaonye walioko duniani wasiendee jehanamu
4. (Makaburi haya yatafunguka wafu nao kufufuka ndipo wewe upate amini)
Bali hao manabii pia ndugu kati yenu ndio waliotumwa kwenu
(Chorus)
Sol: (Wakati)-wakati ni sasa kwa hakika makao yako tayari x4
1. (Katika mji wa Daudi)- Mkombozi Yesu kazaliwa
(Amelazwa katika hori) – kama ilivyotabiriwa
Chorous
Twende kwake sote tukamsujudie
Tutoe zawadi kwa mwana wa Mungu uvumba manemane
2. (Amekuja katika mwili)-kuokoa watu wa dunia
(Wasamehewe dhambi zao)- wapate kwenda juu mbinguni
3. (Jina lake ni Emanueli) – Yani Mungu pamoja na watu
(Anaitwa ni wa ajabu) – naye ndiye Bwana wa amani
1. (Limetimia tabirio) la nabii Isaya
Alitabiri kuzaliwa kwake Yesu mwokozi
(Katika shina lake Yesse) mji wa Daudi
Litachipuka tawi zuri tawi safi la kung’ara
(Chorus) 1
(Ooh shangwe tumwimbie)
Amezaliwa mwana wa Mungu
Kaja kimwili kuokoa kutokana na dhambi
(Ooh sote tuabudu) tushangilie tusujudie
Tumepata mpatanishi kati yetu na Mungu
2. (Sote twende Bethilehemu) tukamtazame
Kavikwa nguo za kitoto amelazwa kihorini
(Tazama nyumba imejaa) hamna nafasi
Wamekuja kumsujudu kumlaki mkombozi
(Chorus) 2
(Ooh leo shangwe kuu) juu mbinguni na duniani
Malaika viumbe vyote wahimidi jina lake
(Halleluya tusifuni) natumwimbie nyimbo za shangwe
Sauti pia vyombo vyetu vimfanyie shangwe kuu x2
1. Sol: (Jamani Mungu atupenda) Mungu hakutuacha yatima x2
Ramani ya uinjilisti -(tunayo ooh tunayo)
Tuhubiri ulimwengu wote
Kujenga hayo mahekalu, tuyajenge katika umoja
Katika utumishi wetu tuwatunze wahubiri wote
Sol : All
Uinjilisti - Tuhubiri ulimwengu wote
Mahekalu- tuyajenge katika umoja
Kwa upendo - tuwatunze wahubiri wote
2. Sol (Ni kweli Mungu atupenda) Mungu hakutuacha yatima x2
Ramani ya maendeleo –(tunayo ooh tunayo)
Makanisa yawe nazo shule
Waahubiri wawe imara-tusikose kuwa na semina
Namna ya kusifu Mungu-kwa vinanda magita na ngoma
Sol : All
Maendeleo - makanisa yawe nazo shule
Kuwa imara - tusikose kuwa na semina
Kusifu Mungu - kwa vinanda magita na ngoma
3. (Hakika Mungu atupenda) Mungu hakutuacha yatima x2
Ramani ya usambazaji –(tunayo tilipewa tunayo)
Runinga, redio,majarida
Namna ya uhusiano – afrika na dunia nzima
Kuongoza kazi ya Mungu- huyo roho ndiye kiongozi
Sol : All
Usambazaji - Runinga, redio,majarida
Uganda , Tanzania - afrika na dunia nzima
Kazi ya Mungu - huyo roho ndiye kiongozi
Usambazaji - runinga, redio, majarida
Madagascar - afrika na dunia nzima
Kazi ya Mungu - huyo roho ndiye kiongozi
1. Mungu wetu ni shujaa huinua shujaa,ili adhihirishe ushujaa wake
Katika kazi atakazozifanya mteule wa Mungu ili mtu apate amini yeye yuko hai. x2
Sitishike wewe mpendwa muamini mtu wa Mungu,kwani yeye amepewa mamlaka naye Mungu juu yake yeye ibilisi
2. Ukitaka kushinda iga walioshinda mashujaa wa Bwana kama mjumbe wake, aliyejawa na kuamini la Mungu, hata shida iweje husimama kukiri, Mungu wake anaweza yote. x2
Sivunjike moyo mpendwa liamini neno la Mungu ukiiga msimamo wa walio shinda vita kwa hakika nawe utashinda
Chorus
Sol : All
(i). (Hili ni onyo kwako mpendwa) – siige aliyeshindwa
(ii). (Ni dharau siikubali) – ndani ya moyo wako
(iii). (Ni uchungu siukubali) – ndani ya moyo wako
(iv). (Ni ulevi siukubalii) – ndani ya moyo wako
(v). (Ni uzinzi siukubali) – ndani ya moyo wako
(vi). (Simamia utakatifu) – mwendo wa mashujaa x 2
(Deep river my home is over jordan
Deep river lord, I want to pass over into camp ground) x2
(Chorus)
Lord I want to pass over into camp ground x2
(Oh don’t you want to go to the gospel feast the promised land where all is free)
(Chorus) x2
(Deep river my home is over jordan
Deep river lord, I want to pass over into camp ground) x2
(Chorus) x2
(Oh don’t you want to go to the gospel feast the promised land where all is free)
(Chorus) x2
(Deep river my home is over jordan
Deep river lord, I want to pass over into camp ground)
MAWAZO YA MUNGU
Ma wa a zo, Ma wa a zo ya Mu ngu
m f r m m r d l d r d
d. r t d d t l f s l s
s l f s s f m d m f m
kwe tu Ni me ma x2
m r f t d
d t d s s
l s l r m
Solo:(Bwana asema)
Ma na a na ya ju a
l. s. l. l. t. d' s
f m f f s l m
Solo:(mawazo)
Ni na yo wa wa zi a a x2
d r r r d s r m
s t t t s m t d
Ni ma wa zo ya A ma ni (Na Wala)
f f m f f f m f
Wa la si ma ba ya a ((x2 a)
s s s s d l' d' s
Ku wa pa Ni nyi tu ma i ni i ~
l l l d d r d m r m~
si ku ze nu za mwi sho oohx2
f m r t f t d le
SOLO:Verse 1
Kwanini ukate Tamaa
Huoni kwenda mbele
Umeipoteza dira hujui uendako
Heri umtuma-inie umtumia-inie Mungu pekeex2
ALL: Harmonise
Te ge me o le tu Ni Mu ngu
l l l l l. s f l s
Si ye na u pe nde le o
r r r r s s f m
Ye si ka ma mwa na da mu
l l l l l s f s
E ti a se me u o ngo
s s s s t l t d
1. Krismas siku ya kuzaliwa kwake Yesu
Mwana wake Mungu
Ndiye neno aliyekuwa mwanzo kutoka kwa Mungu
Bass~(Sikia)
~Malaika wanaimba Hosana
Bass~(Amesha)
~zaliwa mfalme wa Amani
Ndiye Immanueli x2
2. Wachunga walipata habari ya kitoto horini mwa ng’ombe
Waliacha kondoo wakaenda alikozaliwa
Bass~(Sikia)
~Malaika wanaimba Hosana
Bass~(Amesha)
~zaliwa mfalme wa Amani
ndiye Immanueli x2
3. Tazama mamajusi wamashariki nao walifata nyota
Walimsujudia wote kwani ndiye mfalme.
Bass~(Tazama )
~walibeba tunu uvumba vyote
Bass~(Napia)
~walibeba manemane zawadi,
zakumtolea
Bass~(Nasisi)
~tujitoe mili na roho zetu
Bass~(Tuweze)
~kutumika kwake mwokozi Yesu
azaliwe kwetu. x2
Chorus
Furaha kubwa mchungaji atakapo horini
Kwenda kuishi horini, Horini mwake ng’ombe
1. (Mbwa mwitu) (simba wakali)
Waniotea kondeni, njia moja ya usalama
Nirudi kule horini
2. (Jua kali) (shida umande)
Yanikondesha mwituni
Njia moja ya kuepuka
Nirudi kule horini
3. (Mwana mchanga) (amezaliwa)
Katika hori ya ng’ombe
Sababu yangu mchungaji
Nirudi kule horini.
SOL: Tufurahi tena tumsifu
All: Tumsifu tuamini kwake, tufurahi tena tumsifu, Mungu wetu wa zamani
SOL: ooh Tufurahi tena tumsifu
All: Tumsifu tuamini kwake, tufurahi tena tumsifu, Mungu wetu wa zamani
SOL: Wapendwa tufurahi tena tumsifu
All: Tumsifu tuamini kwake, tufurahi tena tumsifu, Mungu wetu wa zamani
SOL: kanisa tufurahi tena tumsifu
All: Tumsifu tuamini kwake, tufurahi tena tumsifu, Mungu wetu wa zamani
(pause)
SOL: Tufurahi tena tumsifu
All: Tumsifu tuamini kwake, (tuamini kwake) tufurahi tena tumsifu, Mungu wetu wa zamani
SOL: wadada Tufurahi tena tumsifu
All: Tumsifu tuamini kwake, (tuamini kwake) tufurahi tena tumsifu, Mungu wetu wa zamani
SOL: wandugu tufurahi tena tumsifu
All: Tumsifu tuamini kwake, (tuamini kwake) tufurahi tena tumsifu, Mungu wetu wa zamani
SOL: watu wote tufurahi tena tumsifuuuu
All: Tumsifu tuamini kwake, (tuamini kwake) tufurahi tena tumsifu, Mungu wetu wa zamani
Sol 1:
Mungu wa zamani All: Mungu wetu wa zamani
Yeye yule “ “ “ “
Ooh toka mwanzo “ “ “ “
Hakuna kama yeye “ “ “ “
Mungu wa Ibrahimu “ “ “ “
Bado hajabadilika “ “ “ “
SOL 2:
Chezea Yesu cheza All: cheza x2
Inua Yesu Inua inua x2
Bariki Yesu bariki bariki x2
Shangwe na vigelegele kwa Bwana Yeeeeesu
Sol 1:
Ooh Mungu wa zamani All: Mungu wetu wa zamani
Hakuna kama yeye “ “ “ “
Aliyeponya Bartimayo macho “ “ “ “
Yeye ndiye tunamwabudu “ “ “ “
Hakuna kama yeye “ “ “ “
Mungu aishiye “ “ “ “
SOL 2:
Yesu Yesu Yesu Yesu All: Yesu x2
Yesu anaokoa Yesu x2
Yesu anabariki Yesu x2
Shangwe na vigelegele kwa Bwana Yesu
(pause)
Sol 1:
Ndiye tunamwabudu All: ndiye tunamwambudu
Ndiye tunamwinua ndiye tunamwambudu
Hakuna kama yeye ndiye tunamwambudu
Aliyeponya Bartimayo macho ndiye tunamwambudu
Ndiye tunamwabudu ndiye tunamwambudu
Ainuaye mnyonge toka mavumbini ndiye tunamwambudu
Sol 1:
{Ndiye All: tunamwambudu x2
Aliye Mungu wa Amani tunamwabudu
Na yeye bado ni wa Amani tunamwabudu
Ndiye tunamwabudu x 2
Ainuaye mnyonge toka mavumbini tunamwabudu
Ooh ndiye tunamwabudu x2
Hakuna kama yeye tunamwabudu } x2
1. Shika sana ulicho nacho, asije mwovu, akakupokonya
Imani ile ya kwanza, uitunze kama kwanza x2
Chorus:
kwani sasa umefanikiwa, usibaki kujivunia,
bali ujilinde, ukichunguza, kutokaribisha na uchafu,
na shetani ajapo umpinge x2
2. Mafundisho pia maonyo, vilinde sana ulivyopokea,
kwani shetani yu macho ili akuhuzunishe x2
3. Kesha sana, yaimarishe yalosalia, yatayokufa,
ukumbuke livyopokea, uyashike na udumu x2
All: Yesu akawaita wanafunzi wake, kumi na wawili, akawapa amri juu ya pepo, wachafu, wawatoe na kupoza magonjwa yote na udhaifu, wa kila aina x2
{Solo: Hao thenashara Yesu aliwatuma, akawaagiza akisema akisema
All: Katika njia za mataifa msiende, wala katika mji wowote wa wasamaria msiingie
Solo: Katika njia
All: Katika njia za mataifa msiende, wala katika mji wowote wa wasamaria msiingie} x 2
Solo2 vita, chuki uchungu na hasira hayo ni baadhi ya mengi maovu, kinyume cha maagizo yake Baba Mungu, uwe mwanafunzi nawe utaona amani x 2
{Solo: Hao thenashara Yesu aliwatuma, akawaagiza akisema akisema
All: Katika njia za mataifa msiende, wala katika mji wowote wa wasamaria msiingie
Solo: Katika njia
All: Katika njia za mataifa msiende, wala katika mji wowote wa wasamaria msiingie} x 2
Solo 2: Hakuna amani kwa mtu anayeiga njia za mataifa, iga amani, umoja utakatifu na upendo
Hakuna furaha kwa mtu anayeiga njia za mataifa, iga Imani, umoja utakatifu na upendo
Solo1: nawe ndugu yangu Yesu anakuita leo, anakuagiza, anasema anasema
All: Katika njia za mataifa usiende, wala katika njia zozote za wasioamini usiige
Solo: Katika njia
All: Katika njia za mataifa usiende, wala katika njia zozote za wasioamini usiige
Solo 1 Nawe dada yangu Yesu anakuita leo, anakuagiza anasema anasema
All: Katika njia za mataifa usiende, wala katika njia zozote za wasioamini usiige
Solo: Katika njia
All: Katika njia za mataifa usiende, wala katika njia zozote za wasioamini usiige
Solo: Katika njia
All: Katika njia za mataifa usiende, wala katika njia zozote za wasioamini usiige
Solo: Katika njia
All: Katika njia za mataifa usiende, wala katika njia zozote za wasioamini usiige
Solo: Katika njia
All: Katika njia za mataifa usiende, wala katika njia zozote za wasioamini usiige
Sol: Jamani sio sisi tuliomchagua Mungu, bali ni yeye Mungu aliyetuchagua sisi
Hata akamtoa mwanawe duniani ili kutuokoa sisi wanadamu x2
Tumepata wokovu, wokovu wa ajabu
Tumepata wokovu, (sol: wokovu wa ajabu)
Tumepata wokovu, wokovu wa ajabu
Tumepata wokovu, (sol: wokovu wa ajabu)
All: (Tutunze wokovu huu tutunze wokovu) x2
Tuzimhuzunishe roho, kuyatenda mabaya bali tujifunze kumpendeza Mungu x2
Tumwogope Mungu x4 Tumwogope Mungu x4
Sisi je? tutatapataje kupona tusipojali wokovu namna hii? x2
All: Kama mwanzo ulinenwa na (Bwanaaa), kisha ukadhibitika kwetu (na waliosikia)
Sol: Kwa hakuna jambo asiloliweza Mungu, Mungu ni yeye mwanzo tena ndiye mwisho, lakini wanadamu tumemuasi Mungu tumemkataa Mungu hatutaki wokovu. X2
Tuujali wokovu, wokovu wake Mungu
Tuujali wokovu, (wokovu wake Mungu)
(Tutunze wokovu huu tutunze wokovu) x2
Tuzimhuzunishe roho, kuyatenda mabaya bali tujifunze kumpendeza Mungu x2
Tumqogope Mungu x4 Tumqogope Mungu x4
Sisi je? tutatapataje kupona tusipojali wokovu namna hii?x2
Kama mwanzo ulinenwa na (Bwanaaa), kisha ukadhibitika kwetu (na waliosikia) x3
{sop: angalie utakapokuwa ukikula na kushiba
all: na kujenga nyumba nzuri na kukaa ndani yake
sop: na makundi yako ya ng’ombe na kondoo yatapoongezeka
all: fedha, dhahabu na kila kitu ulicho nacho, kitakapo-ongezeka} x2
(pause)
{sop: angalie utakapo kuwa ukikula na kushiba
all: na kujenga nyumba nzuri na kukaa ndani yake
sop: na makundi yako ya ngombe na kondoo yatapo-ongezeeka
all: fedha, dhahabu na kila kitu ulicho nacho, kitakapo-ongezeka} x2
{sop: basi hapo moyo wako
all: usiinuke
sop ukamsahau Bwana
all Mungu wako
sop Aliyekutoa katika nchi
all Ile ya Misri, katika nyumba ya utumwa} x2
Sol: waisraeli wakiwa jangwani, wakasahau yale mema na mengi makuu Mungu wao aliowafanyia wakaanza kunung’unika na kuigeukia miungu wakaanza kunung’unika na kuigeukia miungu x2
SOL: Ninamwimbia Bwana maana nimepona x4
SOL: Ninamwimbia Bwana maana nimepona x2
all: Ninamwimbia Bwana maana nimepona x2
(pause)
SOL: Ninamwimbia Bwana maana nimepona
all: Ninamwimbia Bwana maana nimepona x2
SOL: Ninamsifu Bwana maana nimepona
all: Ninamsifu Bwana maana nimepona x2
SOL: Ninamchezea Bwana maana nimepona
all: Ninamchezea Bwana maana nimepona x2
break
sol2 ninamwimbia Bwana kwakuwa nimepona x2
all ninamwimbia Bwana kwakuwa nimepona x2
sol2 ninamwimbia Bwana kwakuwa nimepona x2
all ninamwimbia Bwana kwakuwa nimepona x2
sol2 amenipa amani amenipa uzima, ninamwimbia Bwana kwakuwa nimepona
all ninamwimbia Bwana kwakuwa nimepona x2
sol2 amenipa Baraka, amenishindia, ninamwimbia Bwana kwakuwa nimepona
all ninamwimbia Bwana kwakuwa nimepona x2
sol2 shangwe na vigelegele kwa Yesuuuu….
[sol: chezea Yesu cheza All chezaa x4
sol [imbia Yesu all: imba x4
sol [rukia Yesu all ruka] x6
(pause)
Sol2: ewe mama imbia Bwana
all: kwakuwa umepona kwakuwa umepona
so2l: ewe dada chezea Bwana
all: kwakuwa umepona kwakuwa umepona
sol2: ewe kaka rukia Bwana
all: kwakuwa umepona kwakuwa umepona
sol2: ewe baba imbia Bwana
all: kwakuwa umepona kwakuwa umepona
{sol2: haleluya all: aamen ] x10
Sol2: celebrate Jesus …………………..
sol2 ninamwimbia Bwana kwakuwa nimepona x2
all ninamwimbia Bwana kwakuwa nimepona x2
All: Nuhu akamjengea Bwana madhabahu,
Akatwaa kila mnyama na ndege aliye safi
Akavitoa sadaka ya kuteketezwa
Juu ya madhabahu x 2
Sol {Bwana
akasikia harufu ya kumridhirisha akasema moyoni sitailani nchi tena
sol Baada
ya haya yote (Bwana) mawazo ya mwanadamu mabaya tangu ujana wake {x2
all: {Habili nduguye Kaini akaleta wazao, wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizo nona Bwana akamtakabali na hiyo sadaka yake } x2
Sol {Bwana
akasikia harufu ya kumridhirisha akasema moyoni sitailani nchi tena
sol Baada
ya haya yote (Bwana), mawazo ya mwanadamu mabaya tangu ujana wake {x2
2 solos {harufu nzuri ni matendo mema
All harufu nzuri ni kumcha Mungu
2 solos harufu nzuri sadaka shukurani
All mtolee Mungu kwa uaminifu }x2
All Mungu hataruhusu ubaya wowote katika maisha yako kwa huo uaminifu
Solo Mungu hataruhusu – mabaya kwako – ukiwa mwaminifu
All Mungu hataruhusu ubaya wowote katika maisha yako kwa huo uaminifu
Solo Mungu hataruhusu – madeni – ukimtumikia
All Mungu hataruhusu ubaya wowote katika maisha yako kwa huo uaminifu
Solo Mungu hataruhusu – umaskini – ukimtolea
All Mungu hataruhusu ubaya wowote katika maisha yako kwa huo uaminifu
Solo Mungu hataruhusu – magonjwa kwako – ukiungama dhambi
All Mungu hataruhusu ubaya wowote katika maisha yako kwa huo uaminifu
(pause)
(Bwana) akisikia harufu yakumridhisha, atasema moyoni sitakulaani wewe tena
All: (sheria sheria humfunga mwanadamu
sheria sheria kizuizi cha mema) x2
All: (sheria sheria humfunga mwanadamu
sheria sheria kizuizi cha mema) x2
Solo: Palikuwepo mwanamke ,mmoja msamaria.
Alikwenda kisimani, ili kuyateka maji,
Lipofika kisimani, kamkuta Bwana Yesu,
Naye Yesu kamwambia nipe maji ninywe
Naye Yesu kamwambia nipe maji ninywe
Huyu mwanamke kamwambia Yesu
2 solo Haiwezekani kamwe haiwezekani
Sopr ; (Wewe ni myahudi
Alt ; Na mimi ni msamaria
Tenr ; Kwani hatuchangamani
Bass ; Kwani hatuchangamani)×2
Solo: Ndipo Yesu kamwambia, mwanamke msamaria,
Kama ungaliijua hiyo karama ya Mungu,
Naye ni nani akuambiaye nipe maji,
Ungalimuomba yeye maji yaliyo hai
Ungalimuomba yeye maji yaliyo hai
Yule mwanamke kamjibu Yesu
2 solos: Ni maji gani hayo ni maji gani
Sopr : ( Unipe maji hayo
Alt : Maji hayo ya uzima
Tenr : Nisiione kiu tena
Bass: Nisione kiu tena)×2
Solo: Kama yule mwanamke, aliondoa sheria,
Kakubali Bwana Yesu, naye akawekwa huru,
Kakimbia vijijini, kutangaza neno lake,
Naye Yesu atwambia, tuondoe sheria,
Naye Yesu atwambia, tuondoe sheria,
Sheria imetufunga sisi saasa,
2 solos :Tuiondoe hiyo sheria yetu.
Sprn : (kwani sheria ni yale
Alt : Yaliyo mapenzi yako.
Tenr : Tujifunze kuishi
Bass : Kwa sheria yake Mungu)×2
Solo: Ili upate Amani All: Uindoe sheria x2
Ili upate kupona Uiondoe sheria x2
Ili upate Baraka Uiondoe sharia x2
Nawe utawekwa huru Ukiondoa sharia x3
1. Tuwe nayo nia moja, katika Bwana,
Wenye kupendana kama ndugu, hehehee,
wasikitivu watu wenye unyenyekevu x2
Chorous
Hapo ndipo, hakuna adui atakayetutoa
Pendoni mwa Mungu, tukisimama
kwenye zamu zetu, ushindi wa kweli unapatikana x2
2. Tu viungo vya mwili mmoja, katika Kristo
Kila kiungo kwa zamu yake,
tujenge mwili wa Kristo ili kanisa lisimame x2
3. Basi nani atatudhuru, tukitenda mema
Mioyoni tuwe tumejazwa dhamiri njema
Adui ajaposema uongo atahayari x2
Solo1: Sikiliza habari za Paulo na Sila watumishi wa Mungu walofungwa gerezani x2
ni sababu gani? Ni sababu gani? Paulo na Sila kujikuta gerezani x2
All: kwa sababu ya injili ya Yesu, Paulo na Sila walifungwa gerezani x2
Solo1: Wakiwa gerezani Paulo na Sila, walipata mateso ooh mengi sanaX2
All: walivuliwa nguo na kupigwa viboko, walipata mateso oh gerezanix2
solo2: Lakini panapo usiku wa manane, Paulo na Sila walikuwa wakimwomba Mungu,
wakimwimbia nyimbo za kumsifu, wafungwa wengine nao waliwasikiliza x2
All: ghafla tetemeko la nchi, likaitikisa milango ya gereza x2
Solo1: na milango ya gereza ikafunguka, na vifungo vya wote vikalegezwa x2
Solo 3: [sasa usiishi kwa gereza la umasikini..
All: sifu Mungu nawe utafunguliwa]x2
Solo 3: [sasa usiishi kwa gereza la magonjwa
All: sifu Mungu nawe utafunguliwa]x2
Solo 3: [sasa usiishi kwa gereza la dhiki, shida
All: sifu Mungu nawe utafunguliwa]x2
All: sifu Mungu, nawe utafunguliwa
Solo 3: Wakati wa shida
All: sifu Mungu, nawe utafunguliwa
Solo 3: Wakati wa raha
All: sifu Mungu, nawe utafunguliwa
All: sifu Mungu, nawe utafunguliwa
Solo: {Neema neema aah
All: Neema ya Mungu yanitosha} x2
All: Naye akaniambia neema yangu yakutosha
Maana uweza wangu hutimilika kwa udhaifu
Solo: Basi nitajifia udhaifu wangu kwa furaha
Ili uweza wa Kristo ukae juu yangu x2
Napendendezwa na udhafu mimi
All: Kwa ajili ya Kristo
Solo: Ufidhuli misiba hata shida
All: Kwa ajili kwa ya Kristo
All: {Maana niwapo dhaifu
Ndipo nilipo na nguvu } x2
Solo: {Neema neema aah
All: Neema ya Mungu yanitosha} x2
All: {Hata sasa atuambia neema yake yatutosha
maana uweza wake hutimilika kwa udhaifu} x2
Solo: basi ndugu jisifie udhaifu wako kwa furaha
ili uweza wa Kristo ukae juu yako
basi dada jisifie udhaifu wako kwa furaha
ili uweza wa Kristo ukae juu yako
Upendezwe na udhaifu wewe
All: kwa ajili ya Kristo
Solo: Upendezwe na udhaifu dada
All: kwa ajili ya Kristo
Solo: Upendezwe na udhaifu ndugu
All: kwa ajili ya Kristo
Solo: Upendezwe na udhaifu dada
All: kwa ajili ya Kristo
{maana uwapo dhaifu
ndipo ulipo na nguvu }x2
Solo: Napendezwa na udhaifu mimi
All: Kwa ajili ya Kristo
Solo: Napendezwa na hayo matatizo
All: Kwa ajili ya Kristo
Solo: Napendezwa na maneno manyonge
All: Kwa ajili ya Kristo
Solo: Napendezwa na huo upungufu
Kwa ajili kwa ya Kristo
All: [maana niwapo dhaifu
ndipo nilipo na nguvu ]x4
All: Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo,
maana ndiko zitokako chemichemi za uzima
maana ndiko zitokako chemichemi za uzima x2
Solo: sikurudi nyuma kuiacha amri ya midomo yake eeh,
nimeyatunza maneno ya kinywa chake zaidi ya riziki yangu x2
All: Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo,
maana ndiko zitokako chemichemi za uzima
maana ndiko zitokako chemichemi za uzima x2
Solo: usirudi nyuma kuiacha amri ya midomo yake eeh,
utunze kumtolea zaka, sadaka, zaidi ya hitaji lako x2
All: Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo,
maana ndiko zitokako chemichemi za uzima
maana ndiko zitokako chemichemi za uzima x2
Solo: usirudi nyuma kuiacha amri ya midomo yake eeh,
utunze sana upendo kwa watu wote zaidi ya chuki yako x2
All: Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo,
maana ndiko zitokako chemichemi za uzima
maana ndiko zitokako chemichemi za uzima x2
solo: Linda moyo
All: Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo,
maana ndiko zitokako chemichemi za uzima
solo: maana ndiko
maana ndiko zitokako chemichemi za uzima x4
Let every creature, (creature) that has breath, praise the Lord, praise the Lord x2
Let every creature, (creature) that has breath, praise the Lord, praise the Lord x2
His name is Jesus, Jesus, Jesus, Jesus King of Kings, his name is Jesus Christ, Lord of Lords x2
Haleluya praise the Lord, praise the Lord, haleluya praise the Lord, oh oh praise the Lord x2
Let every creature, (creature) that has breath, praise the Lord, praise the Lord x2
His name is Jesus, Jesus, Jesus, Jesus King of Kings, his name is Jesus Christ, Lord of Lords x2
Haleluya praise the Lord, praise the Lord, haleluya praise the Lord, oh oh praise the Lord x2
Haleluyah praise the Lord, praise the Lord, haleluyah praise the Lord, oh oh praise the Lord
Haleluyah praise the Lord, praise the Lord, haleluyah praise the Lord, oh oh praise the Lord
Haleluyah praise the Lord, praise the Lord, haleluyah praise the Lord, oh oh praise the Lord
Haleluyah praise the Lord, praise the Lord, haleluyah praise the Lord, oh oh praise the Lord
His name is Jesus Jesus, Jesus, Jesus King of Kings, his name is Jesus Christ, Lord of Lords
( Melody)
Kwa ma a na twa ju a
d. d. d s r. r l
(All)
I ma ni bi la ma te ndo i me ku fa
m s s s s m f f. f. m. r. d
d m m. m m d. r. r. r. d. t. s
s t. t. t. t. s. l. l. l. s. f. m
d. s. s. s. s s. r. r. r. s. t. d
(Melody)
Mwa na da mu hu he sa bi wa ha a ki
d. l. d. m. d. r. r. r. r. r. r. r
(All)
Kwa ma te ndo Ba li si kwa I ma ni ya ke pe e ke
m. f. s. s. s. s. m. f. f. f. f. m. r d. t. d
d. r m. m. m.m.d . r. r. r. r d. t. s. si. s
s. t. d. d. d. d. s. l. l. l. l. s. f. m. r. m
d. t. d. d. d. d d. r. r. r. r s. f. d. t. d
I we e e ni wa te nda ji wa ne no, wa a a la si wa
d m r. r. d. m m. m.m m. f l l. t d. t. t. t
s. d. t t .s. d d. d. d. d. d f. f. s. l. s. s. s
m s. f. f m s. s. s. s. s. l. d d r m r. r. r
d. d. t. d.d. d. d. d. d. d. f. f. f. s. l s. s. s
si ki a ji tu x2
t t. t. l s
s s. s f m
r. r. r d d
s s. s f. d
I we e e ni wa te nda ji wa ne no, wa a a la si wa
s d s. s s d. d. r. r. r. f. l m. f f. l. d. d
m s m m m s. s. l. l. l. d. f. d. r. r f. s. s
d m. d. d. d. m. m. f. f. f. l. r. s. l. l r m m
d. d. d. d d. d d r. r. r. f f. d l. l. l. d. d
si ki a ji tu x2
d d. r m d
s s. t. d. s
m m f. s. m
d. d. t d. d
Ra ha bu~ yu le ka ha ba~a a li he e sa bi wa
d. r. m mi d. d. r. m . r m l. t. d t. l l. l
s. t. d. si s .s. t. d. t. d. f. s. l. s. f f. f
m. f. s. m.m. f. s. f. s. d. r. m r. d. d. d
f s. l. s. f. f. f
ha a ki A li po wa fi cha wa le wa ju u u u u mbe
l. li l l t. d. l l. r. d. l. l. s. d. t.d t. l
f. si f f. s. l. f. f. t. l. f. f m l s. l s m
d r d. d r. m. d. d. f. m. d. d. t. m r m r d
f. t f. f s. l. f. f. s. d. f f. s l. s. l. s. d
( Rahabu Solfas👇)
Abraham naye pia alihesabiwa haki
Alipomtoa mwanawe kama Sadaka
U na po si ki a ku hu su ku tu bu na u te nde
m m m. m m m. f. m. r. r. r. r ~ r. r. d. d
# # #. #. #. #. #. #. #. #. # #. #. # #. #
t t t t. t.( l...................................................
U ta. he sa bi wa ku po na
d. d. d. d. t. t t. t. l~
#. #. #. #. #. #. #. #. #
l. s*..................................)
(Unaposikia Solfas 👇)
Unaposikia kuhusu kutoa na utende
Utahesabiwa baraka
(Unaposikia Solfas 👇)
Unaposikia kuhusu kusamehe na utende Utahesabiwa msamaha
A na he ri. a i ta za ma she ri a ka mi li fu
d t. d. s. d d t. l. l. l. l. l. l. l. t. d
l. s. l m. s s s. f. f. f. f. f. f. f. s..s
m r. m. d. m m m r. r. r. r. r .r. r. m m
ya u hu ru na ku ka a hu mo a si we msi ki a ji
l. t. d. s. s. s. d. d. s. s. d .d. t. l. l. l. l
f. s l. m m. m. s s m. m. s. s. s. f. f. f. f
r. m f. d. d. d. m.m d. d. m m m. r. r. r. r
msa ha u li fu Ba li mte nda ji
l. l. l t. t. d. d. f. r. d
f. f. f. s s. m. m. d. t. s
r. r. r m m d. d. s. f. m
(Ana heri Solfas 👇)
Hivyo wewe Utahesabiwa haki si kwa Imani Bali matendo utayapata mema nayo mafanikio ambayo Mungu aliahidi.
Kwa maana mumeokolewa, kwa neema
kwa njia ya imani,ambayo hiyo haitokani na nafsi zenu
Ni kipawa cha mungu *2
Wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.
Maana tu kazi yake tuliumbwa katika kristo Yesu *2
(Solowist)
Hali tukijuwa mwanadamu hahesabiwi haki
Kwa matendo ya sheria kwa imani ya kristo Yesu
Ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu
( All) Kwa ajili yetu kwa ajili yetu
(Solowist)
Ili atuokoe katika maasi yote,
Na kujisafishia watu wawe milki yake mwenyewe mwenyewe.
Wale walio na juhudi katika kuyatenda mema.
( All) Kuyatenda mema kuyatenda mema.
Chorous
Basi tuyatende matendo mema
Ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza
Ili tuenende nayo,nayo nayo
(Solowist)
-Heshima alitengeneza tangu mwanzo
-Upendo alitengeneza tangu mwanzo
-Amani alitengeneza tangu mwanzo
Wasiokubali (niwatawale) waleteni mbele zangu muwachinje
(Ewe ndugu mwongofu umo kanisani,lakini huoni uponyaji,Baraka,amani na mengine mengi kutoka kwa Mungu,huko ndiko kuchinjwa kunakotokana na kutokubali kutawaliwa na Yesu kristo)
Kukubali kutawaliwa ni kuacha vyote, ni kwenda kinyume cha mapenzi yako,mara unaposikia sauti ya bwana atakavyokuagiza.
(katika mambo yote bwana ananitawala,nisiseme liko moja gumunisiloweza kufuata)
Nisemapo bwana anitawala yanipasa kuacha yaliyo mapenzi yangu nifuate kama apendavyo yeye.
(Atawalikaye hana mambo yake mwenyewe isipokuwa yale ya bwana wake ayapendayo yeye)
(Katika mambo yote bwana unitawale) – nakubali bwana tawala
(katika kutii bwana unitawale) – nakubali bwana tawala
(pia kutakasika bwana unitawale) – nakubali bwana tawala
(kuishi kwa imani bwana unitawale) – nakubali bwana tawala
(nijaze roho wako bwana unitawale) – nakubali bwana tawala
1. Natamani mji ule mzuri
Makao mazuri ya furaha
Ni Yerusalemu mbinguni x2
(Chorus)
Nimwone, mwokozi
Na wale waliotutangulia mbingunix2
2. Nyimbo nzuri tutaziimba kule
Tukimsifu Yesu mwokozi
Tukirukaruka mbinguni
(Chorus)
Tutashangilia, tutakapoonana
Na wateule wote x2
3. Tunaoamini tufurahie
Kwa kuwa tutaonana nao
Wale waliotangulia x2
(Chorus)
Tutashangilia
Tutakapoonana na wateule wote. x2
Yona akamezwa na samaki,kwa kukataa kutii sauti ya Mungu,akapelekwa asikotaka
(Umemezwa na samaki wa uzinifu sasa wapelekwa usikotaka)
(Umemezwa na samaki wa chuki sasa wapelekwa usikotaka)
(Umemezwa na samaki wa uongo sasa wapelekwa usikotaka)
(Umemezwa na samaki wa fitina sasa wapelekwa usikotaka)
(Umemezwa na samaki wa kupinga sasa wapelekwa usikotaka)
(Umemezwa na samaki wa dharau sasa wapelekwa usikotaka)
(Umemezwa na samaki wa ukaidi sasa wapelekwa usikotaka)
(Ondoa nadhiri kwa sauti),sauti ya shukurani
(Ukatapikwe na uzinifu ) samaki wa uzinifu
(Ukatapikwe na chuki) samaki wa chuki
(Ukatapikwe na uongo) samaki wa uongo
(Ukatapikwe na fitina ) samaki wa fitina
(Ukatapikwe na kupinga ) samaki wa kupinga
(Ukatapikwe na dharau ) samaki wa dharau
(Ukatapikwe ukaidi ) samaki wa ukaidi
1. Mji wa Daudi (Mji wa Daudi) Leo ametoka (Leo ametoka)
Aliyemkuu (ni mkuu tumshangilie), Tumshangilie
Ndiye Bwana Yesu (Ndiye Bwana Yesu), aliyezaliwa (aliyezaliwa)
Ni ishara kuu (ni ishara kwetu sisi sote), kwetu sisi sote. x2
(Chorus)
(Njoni nyote) Tumshangilie, (Njoni nyote) Tumsujudie, (Njoni nyote) Tumsifu kwani leo yuko horini.. x2
2. Tazama Herode (Tazama Herode), kwa uchungu mwingi (kwa uchungu mwingi)
Katumana watu (katumana walete habari), walete habari
Kauwa watoto (kauwa watoto), wote wa kiume (wote wa kiume)
Lakini kashindwa (akashindwa kumuuwa Yesu), kumuuwa Yesu.
3. Leo duniani (leo duniani), Hata na mbinguni (hata na mbinguni)
Wote wanaimba (wanaimba utukufu wake), utukufu wake
Tumepata njia (tumepata njia), tena ukombozi (tena ukombozi)
Msamaha dhambi (msamaha ukimuamini), ukimuamini.
Mungu mtukufu aliye bwana wa mabwana
Akamtoa mwanawe Yesu mpendwa
Sifuni msifuni nchi yote
Njoni kwake Yesu
Mpeni heshima aliye
Bwana wetu
Yesu ulikuja kutuletea nuru kuu
Nasi twakusifu wewe nakushukuru
Roho kiongozi, roho wa mapenzi ongoza
tia nuru tunaomba tumulikie
1. Usiku wa manane
Yesu alipozaliwa Bethlehemu
Mariamu na Yusufu
Walifuraha kumpata mtoto
(Chorus)
(Sote) twendeni (tuka)mwimbie
(Nyimbo) za shangwe, (kule) horini
(Kaza)liwa kwa (aji)li yangu
(Mimi) na wewe, (Tuo)kolewe x2
2. Mamajusi wachunga
Wafurahia habari
Yakuzaliwa kwake mwokozi Yesu
Mfalme wa watu wote ulimwenguni
3. Mfalme Herode kafadhaika
Alipopata habari
Kaamua kuangamiza mwokozi
Kwa kuwauwa watoto.
1. (Amekuja kwetu, aliyemtakatifu) ~ Soprano
(Malaika ndiye kaleta habari njema.) ~Tenor
All: Leo kazaliwa na bikira Mariamu
Ndiye Yesu kristo mwokozi wa ulimwengu
(Amekuja kwetu, aliyemtakatifu) ~Alto
(Malaika ndiye kaleta habari njema.) ~Bass
All: x2
2. (Mji wa Daudi umetukuka kwa sifa) ~Soprano
(Wenye sifa zote na amani duniani) ~Tenor
All: Yesu kazaliwa mwana mpendwa wa Mungu
Tumshangilie Hosana tumwimbieni
(Mji wa Daudi umetukuka kwa sifa) ~ Alto
(Wenye sifa zote na amani duniani) ~Bass
All: x2
3. (Tujiunge sote tumsifu mwana huyu) ~Soprano
(Tupate wokovu na uzima wa milele) ~Tenor
All: Natumtolee sehemu iliyonono
Azaliwe kwetu atukuke ndani yetu.
(Tujiunge sote tumsifu mwana huyu) ~Alto
(Tupate wokovu na uzima wa milele) ~Bass
All: x3
Mungu atupenda, katoa mwana
Wake wapekee Yesu Kristo
Ili kwa kila anayemwamini
Apate uzima wa milele
(Twakushukuru) Mungu twakusifu twakutukuza
(Pendo lako kwetu) kweli ni la ajabu
Halina kifani
Ndugu usipompenda ndugu
Umwonaye kwa macho yako
Utawezaje kumpenda Mungu
Ambaye haujamwona
Ndungu nasema natupendane
Kama alivyotupenda Mungu
Tuonyeshane pendo la kindungu
Na tutamshinda shetani.
Ni wakati mgumu, Yesu alipokuwa kizaliwa
Tabirio kuwa ni mwokozi, mfalme wa wanadamu
Hakuna mwingine azaliwe badala yake
Ila huyo tu mwana pekee wa Mungu
Mariamu ana mimba watembea toka Galilaya
Waelekea Bethlehemu, ili kujiandikisha
Uchungu kwa Mariamu, mara ndipo mjini mwa Daudi
Wapangaji tele wamejaa, nafasi hori ya ng’ombe
Kitoto o ni kichanga, pamoja na hila za Herode
Ndoto tahadharisha Yusufu, wajisalimisha Misri
Mamajusi waelekea wapi
(Bethlehemu) nieleze ni kitu gani wanaeliokifata
(Mwokozi) wa ulimwengu, amezaliwa Bethelehemu
Katika ki hori
Twendeni sote horini, Tukamsujudu mwana.
Wachungaji waelekea wapi
(Bethelemu) nieleze ni kitu gani wanachukifata.
Ameshazaliwa mwana wake Mungu
Kama ilivyokuwa tabirio
Ndiye Imanueli, Mpendwa wa Mungu
Yuko tayari kihorini
Tushangilieni, tufurahieni
Ameshazaliwa mwana wa Mungu
Tuimbeni sote tusujudieni
Ukombozi umeshafika
Hila za Herode, kataka kuuwa
Watoto wote, Bethlehemu
Lakini Yusufu kaenda usiku
Kujisalimisha Miisri
Tumshangilie, Tumsujudie
Tumtolee zawadi zetu
Ameshazaliwa kuokoa wate
Kutokana na dhambi zao
Bethilehemu ya Uyahudi
(Kazaliwa mwana kihorini x 2)
Ni furaha gani kwa yeyote anayemwamini
Mwana kama mwokozi wa dunia
Mamajusi nao wapeleka
(Manemane pia na uvumba x2)
Wachungaji wale wa kondeni
(Waenda kumsujudia mwana)
Mtoto mchanga amezaliwa
Bethilehemu horini
(Ajaye)( kwa jina) la baba Mungu wetu
Malaika wamwimbia shangwe
Hosanna, Hosana, mbarikiwa
Alitabiriwa mwokozi Yesu
Naye nabii Isaya
Ukampokee mwokozi Yesu
Akawe mwokozi wako.
1. Mateso ya Yesu aliyopata
Ni kwa ajili yangu mimi nawe
Alipigiliwa msalabani
ataka tuokoke x2
(Chorus)
(Ni kweli) Yesu aliteswa
(Na damu) yake alimwaga
(Juu yetu na sisi) Ili tuosheke (tuosheke)
Tufutiliwe dhambi zetu x2
2. Mnafiki Yuda kapenda fedha
Kamsaliti mwana wake Mungu
Kapokea tonge nakambusu
akakamatwa
3. Njoo kwake Yesu Yesu uokolewe
Damu yake Yesu inatakasa
weka imani yako kwake Yesu
Nawe utaokoka.
1. (Bwana) Yesu ni yeye yule
(Jana) leo na milele x2
Habadiliki kamwe, yeye alfa na omega
Mwanzo na mwisho x2
(Basi kitu gani kitatutenga naye) ~Soprano
All: Twampenda kwani alishatupenda
Kifo chake bwana pendo la ajabu
(Bwana Yesu amaliza yote) ~Bass
All: msalabani
(Kwa kupigwa kwake) ~Tenor
All: twaokolewa
2. (Basi) tunapopata jaribu
(Tue)puke kutenda dhambi x2
Kwani hayana budi kutokea kwetu sisi
Tusiyumbishwe. x2
(Tudumu katika imani ile ile) ~Soprano
Tukidumisha utakatifu
Alioanzisha mtumishi wake
(Tuyaache matengano yote) ~Bass
All: tuyaacheni
(Tuyaacheni ndugu) ~Tenor
All: tutashinda dhambi x2
1. Ni furaha mbingni Na hata duniani
Amefufuka yeye ndiye Yesu mwokozi
Shujaa ni Yesu Kristo. x2
(Chorus)
Tuimbe kwa furaha leo amefufuka
Amekaa mkono wa kuume wa Mungu
Naye atwombee sote. x2
2. Na alipofufuka, kawambia wanafunzi
Msifadhaike niko pamoja nanyi
Amani na iwe kwenu. x2
3. Nasi tuwe hodari, katika majaribu
tusiwe na hofu, wala tusiogope
Na yote tutayashinda. x2
Harusi duniani ni tatu
Ya kwanza kuzaliwa ya pili ni ndoa
Ya tatu ni muhimu japo ni ya huzuni kwetu
Hivyo kwa harusi hii takasa roho yako
Ukapokee Yesu katika roho Yako.
Nawe utafika kwa Mungu muumba wako
Niongoze bwana popote
Niendapo bwana uwe nani
Nisijepotea dhambini,
Kaa nami bwana wangu
Nihurumie bwana, nikikosa naomba msamaha
Roho wako anitawale
Nienende kama upendavyo
Atawale maisha yangu
Niwe mkamilifu
Nihurumie bwana, nikikosa naomba msamaha
Maombi ni silaha, ya watu wa Mungu
Nao wanaomba bila kuchoka
Hata Yesu akiwa na wanafunzi wake
Aliwaagiza ombeni kwamba
Msiingie majaribuni, kwa kuwa hayana budi
Hata yakiwepo yakuzidi, Bwana atafanya
Mlango wa kutokea
Ikiwa haja zenu Bwana azijua, msiache kuwaombea
Wengine, hasa asimamaye kwa ajili yenu
Ajazwe nguvu awafundishe nyinyi
Kufunga na kuomba bwana apendezwa
Silaha msiache kupanda mlima, Nanyi mkiomba bwana
Atawasikia vita vya shetani na mtawashinda.
Ndugu yangu usichoke, kumcha bwana Mungu
Mwambie yale yote unayataka kwake,Yeye takusikia
Omba usiku, omba pia na mchana
Imani yako idumu.
Muumba wetu asema, uwezo wake tutukuze
Jinsi alivyomleta bwana Yesu kwetu apate kuokoa.
Ee Bwana mwokozi wangu
Nakuomba nisikie
Maombi kilio changu, Ewe Yesu wa rehema
Bwana, ooh Yesu naomba niponye
Nikinge na majaribu, yanijiapo
Niyashinde bwana
Sitachoka kukuomba bwana wangu
Bwana Yesu nakusihi nisikie
Sina mwingine yote wakuniponya magonjwa
Wala wa kunifariji, ila wewe mwokozi wangu
Rehema fadhili zako zanitunza kila siku
Nipe kutubu dhambi nikayashinde maovu.
Roho mtakatifu wa Mungu
Teremka kwetu wana wako
(Utusaidie kila siku katika maisha) x2
Huyu roho ndiye mwenye nguvu
Zakumshinda yule mwovu
Siku zote
Yesu akiwa na wanafunzi
Aliwapa nguvu kufanyika (wana wake Mungu
kwa kujazwa roho mtakatifu)x2
Mpenzi mkristo nakuomba
Usichelewe kumpokea (roho wake
Mungu ndiye kiongozi maishani)x2
Huyu roho atakuongoza
Kwa lolote unalotenda
Siku zote.
Yesu akwita ewe ndugu yangu
ataka uje kwake, anakungojea umkubali
Naye akupokee.
Njoo kwake leo mletee matatizo
Nawe ukimwamini atakuweka huru.
Na usifanye moyo mgumu anapoita Yesu
Ujapokosa wewe umwendee
Naye akupokee
Yesu anao wokovu kamili wa mwili na wa roho
Ni mfariji na huruma nyingi
Naye akupokee
Ewe baba wetu wa mbunguni
Twaja kwako wewe twaacha yote
Utupe pendo na neema yako
Ututawale tukujue wewe x2
Asante baba kwa kuwa ahadi zako ni za kweli
Kwetu wana wako utatimiza
Twaja mbele zako utumishi
Kwa kuwa ni wewe uliyesema
Tukujaribu kwa njia hiyo kweli
Utatimiza tunalokuomba x2
Nasi tuwanyonge bila nguvu
Tunayo imani iliyo haba
Utawezeshe kuifahamu kweli
Tukayashinde yaliyo ya mwovu.
(Shetani ameshindwa)
Hololo lolo shetani ameshindwa - Hololo lolo
(Na Yesu juu juu)
Halleluya na yesu juu juu – haleluya
1. Mtazame Maria ana mimba kwa uwezo wa Mungu
Alipashwa habari hizo naye malaika.
(Chorus)
Shangwe na furaha, yesu amezaliwa
Wachungaji mamajusi wapeleka zawadi x2
2. Ni usiku nchi yote ikimya malaika waimba
Sauti ya mwana horini yesu kazaliwa
3. Bwana Yesu mwenye upendo mwingi akatuhurumia
Tungepataje mema haya rehema za Mungu.
(Chorus) x3
1. Ni mamajusi na wachungaji waliopewa habari hii (ya kuza)liwa kwa mwokozi, Yesu katika nchi ya Uyuda.
(Chorus)
Amezaliwa Yesu, amezaliwa Yesu, (oo) amezaliwa Yesu, katika nchi ya uyuda
2. Ni malaika toka mbinguni aliyeleta habari hii (ya kuza)liwa kwa mwokozi Yesu katika nchi ya Uyuda.
3. Ni Herode aliyewaua watoto wote na sababu ni (ya kuza)liwa mwokozi Yesu katika nchi ya Uyuda.
4. Ni yako ndugu habari hii, ungeamini habari njema (ya kuza)liwa wa mwokozi Yesu katika nchi ya Uyuda.
(Chorus) x3
-(Bethilehemu amezaliwa mwana) mwokozi Yesu mwana wake ee Mungu
(Furaha kubwa kote ulimwenguni) mkombozi wa dunia kaja
(Tumpokeeni mkombozi wetu) katika mioyo yetu siku zote daima
-(Na wachungaji pia na mamajusi) wanafuraha kuzaliwa kwa mwana
(Waifuata nyota kuu mashariki) iwaongoze kule alikozawa
-(Nasi tujiunge nao wachungaji) tumsujudu tumfanyie shangwe
(Tumtolee mioyo yetu zawadi) ili tupate ukombozi wa kweli
-Bethilehemu (ya uyahudi) Amezaliwa mtoto ndiye mwana wa Mungu
(Wachungaji makondeni wapata habari)(ya kwamba) Amezaliwa amezaliwa ooh amezaliwa mwokozi.
-Na mamajusi (wamashariki) walipata habari ya kuzaliwa mwana
(nyota kuu iling’aa ikiwaongoza) (katika) zizi la ng’ombe,alikolazwa ooh katika hori la ng’ombe.
-Naye Herode (wa ufaume) alishikwa na hofu ya kuzaliwa mwana
(Aliwauwa watoto bila ya huruma)(Yusufu) Alimficha mtoto Yesu ooh katika nchi ya Misri.
-Nawe mwenzangu (umesikia) habari ya kuzaliwa kwa mwokozi wa roho
(Usiufanya mgumu huo moyo wako)(pokea) mwana wa Mungu rohoni mwako ooh upate uzima daima.
-Amezaliwa mkombozi katika nchi ya uyuda, amelazwa kihorini mahali waliamo ng’ombe
-Anazo njama amepanga huyo Herode mfaume,kuwatumia mamajusi aangamize mkombozi
-Ni wako ndugu huu wakati mkaribishe mkombozi, isitafutwe na shetani roho yako iangamie
Ni shangwe mwokozi amezaliwa ,kusudi la shetani limeshindwa
Sujudu abudu uzieneze, habari za utukufu wa Mungu
-Ni usiku wa manane anga nyeupe nyota zang’aa
(Wachungaji makondeni waona ishara)
Mbingu iwazi jeshi ni kubwa, malaika wake Mungu wanaimba wimbo huu
Utukufu una Mungu juu na nchi salama,wanadamu nao radhi kuu sasa na daima
-Mamajusi mashariki waelekea Bethilehemu
(nyota kuu inang’aa inawaongoza)
-Huyo mwana amelazwa katika hori la kulia ng’ombe
(Mariamu na Yusufu wapata mtoto)
-(Masia Yesu amezaliwa katika nchi ya uyahudi)
(Ndiye mwokozi wa ulimwengu amekuja kwetu sote)
(haleluya) haleluya amekuja kwa jina la bwana
Haleluya ndiye kristo mwana wake Mungu
-(Na mamajusi wa mashariki wakiongozwa na hiyo nyota)
(wambebea mwokozi Yesu tunu uvumba na manemane)
-(Wale wachungaji makondeni pia waacha kondoo zao)
(waenda kumsujudu mwana mle hori la kulia ng’ombe)
-Mtoto mchanga Bethilehemu amelazwa kwenye hori
Twende kwake na vipawa twende tukamsujudie
-Ishara yetu tutamwona amelazwa kwenye hori
Na Maria amemvika bwana nguo za kitoto
-Beba tunu na uvumba pamoja na manemane
Tusujudu tuabudu kwake bwana wa mabwana
Amezaliwa Yesu mwana wa Mungu, mwokozi mponya bwana wa amani
(Nasikia sauti inayonipendeza)- sauti ya kitoto kichanga horini mwa ng’ombe
Twe-ndeni tukamsujudu pamoja sote
(Mtazame Maria pamoja na Yusufu)- wanafurahia kuzaliwa kwake bwana Yesu
Wazipokea zawadi zake huyo mwana
(Njoni nyote tukamzawadie) – kama walivyofanya mamajusi nao wachunga
Tu-mzawadie na tumsujudu mwana
-(Ee bikira) Mariamu umebarikiwa,utamzaa mtoto utamuita Imanueli
Ndiye atakuwa mwangaza mkuu katika nchi ya mataifa
Atawahubiri watu toba,jina lake mtalitumai
-(Nawewe Yusufu) wa Yakobo kaa na Maria,ndani yake Maria chaitwa kitakatifu
Ndiye atakuwa mwangaza mkuu katika nchi ya mataifa
Atawahubiri watu toba,jina lake mtalitumai
- Zakaria usihofu utapata mwana utamuita Yohana amtangulie bwana
Ndiye atakuwa Eliya nyikani ,atengeneze njia ya bwana
Atawahubiri watu toba,na kutangaza mwaka wa bwana
1. Je waijua njia ile iendayo kule Bwana alikozaliwa
(fuata nyota fuata wachungaji wakuongoze nawe utafika) x2
2. Pia mamajusi mashariki wameshika njia kwenda Bethilehemu
(wamebeba vipande vya dhahabu wavipeleke kwa mtoto Yesu)x2
3. Naye malaika wake Mungu amekwishaleta kwetu habari njema,
(amesema tutamwona mwokozi ameshalala katika kihori)x2
4. Nawe ndugu yangu kipeleke kipande cha dhahabu huo moyo wako
(ukiweke mbele za muhubiri akuogoze umuone Yesu.)x3
Furaha moyoni, furaha ulimwengu wote,bwana mkombozi wetu amezaliwa
Tuitanga azeni habari njema tutangaze, habari ya kupendeza ya kuzaliwa
Na tukamtolee bwana chururu za uvumba pamoja na manemane kama zawadi
(Dunia) dunia, (yote sasa) fahamu
(Kazaliwa) mwana shangilieni pigeni vigelegele
Kuna nini Bethilehemu mji wa Daudi
Watu wengi waelekea Bethilehemu mji wa Daudi
(Mkombozi) – bwana Yesu (Amelazwa) kwenye hori waliamo ng’ombe
Mamajusi wa mashariki waiona nyota
Wachungaji wa makondeni wapata habari
(Mungu asema) itengezeni njia ya bwana nyosheni mapito
(Na mkombozi) Atakuja sayuni kwa wote waachao dhambi
(Ewe ndugu) mwokozi bwana Yesu, (ufungue) ataka ufungue, (uamini) moyo na uamini
(Siku ya leo) ni siku ya wokovu (wa roho) kwa wenye imani (Kwani mwokozi) wa ulimwengu wote (horini) ameshazaliwa
(Nitafurahi) katika bwana wangu na pia nitashangilia, (nimevalishwa) mavazi ya wokovu (na vazi ) la haki ya bwana
Yesu kazaliwa kuwaokoa watu kutoka kwa mizigo ya dhambi zao wapate uzima
Sasa tumepata furaha, kwakua kazaliwa mkombozi
Amelazwa katika hori, lakulia ng’ombe Bethilehemu
Mamajusi wa mashariki wapata habari ya kuzaliwa mwana mkombozi wa wanadamu
Wachungaji wa makondeni waacha kondoo wakaenda horini kumsujudia mkombozi
(Mahali) mahali pachafu kabisa pa mkombozi
(Ni nyota kuu ya mashariki iliyowaongoza Bethilehemu kwa mwokozi)
(Na wewe ndugu ongozwa leo na nyota ya pekee mashariki mhubiri)
Utaona kubarikiwa ndani ya moyo wako
(Amani) Amani furaha kamili na kupona
Bwana harusi leo umepata kitu chema likupasalo kufanya niwewe ukilinde.
Bwana harusi leo umepata chombo chema likupasalo kufanya ni wewe ukilinde
Chombo chema kikufae ni wewe ukilinde sikiachie jamaa ndugu au marafiki
Dunia yetu ya leo imekwishaharibika wakulinda vya wengine wako wapi siwaoni
Hivi leo chombo hiki kinameremeta sana hata wewe ni shahidi vilevile hata sisi
Chombo hiki twakisifu ila tena ni ufahamu hakikosi udhaifu ngao yako iwe pendo
Kazi kwako kazi
-Dada yetu leo Mungu amekutukuza,jilinde na kila vikwazo vitakavyovuruga ndoa yenu,Maishani hakukosi vikwazo kutii neno la Mungu ni bora
-Tena vivyo hivyo dada uwe macho sana,kutii na kuyaheshimu maongozi ya mumeo ee dada, maishani hakukosi vikwazo kutii neno la Mungu ni bora
Shangwe leo, shangwe leo
Shangwe leo shetani ameshindwa
(Nderemo zipigwe shetani ameshindwa)
(Kelele zipigwe)
(Kuruka turuke)
(Kucheza tucheze)
(Magita yapigwe)
(Zo ngoma zipigwe)
(Kelele zipigwe ye ndugu amepata)
(Kuruka turuke wapendwa wameshinda)
(Kuruka turuke shetani yuko chini)
Dada yetu hivi ,leo (wavuka hilo daraja leo)
Shangwe vigelegele vifijo kwa harusi yako nzuri x2
Shikamana na mumeo leo,( kwa kila kitu ee dada leo)
Umeambatanishwa naye leo, (na huyu bwana harusi leo)
Sasa mkitu kimoja leo,( msije mkatenganishwa leo)
Maharusi mnaoendea maisha mapya,tunawapongeza kwa uvumilivu na utulivu
Muendapo maisha mapya msisahau mliyofundishwa naye baba yetu mchungaji wa bwana
Utakatifu mkaudumishe mashauri msiyaache na maombi msiyasahau maishani mwenu
Twawapongeza maharusi, twawapongeza ,twawapongeza maharusi kwa ndoa yenu.
Twawapongeza maharusi twawaongeza,twawapongeza maharusi kwa ndoa yenu.
Twafurahia maharusi twafurahia,twafurahia maharusi kwa ndoa yenu
Ooh twashangilia maharusi twashangilia,twashangilia maharusi kwa ndoa yenu
Ooh vigelegele maharusi vigelegele ,vegelegele maharusi kwa ndoa yenu.
Kama Mungu wa Ibrahimu alivyompa Isaka mke,kutoka nchi ya babake,ndivyo wewe ndugu yangu,malaika wa bwana amekutangulia na kukupa mke kutoka nchi ya jamaa ya baba yako.
Wakala wakanywa bi harusi na wote aliokuwa nao,sasa yuaja bi harusi mradi Mungu ameifanikisha njia yake.
Ametwaa shela yake amejifunika,kando yake ni vijakazi wanamsindikiza.
Haya inuka moyoni mwako we bwana harusi ukamlaki bi harusi.
Haya inuka we bwana harusi ukamlaki bi harusi
Haya inuka we bwana harusi ukamlaki moyoni mwako
Ukamlaki maana ni mke wako umepewa na bwana
Umkubali maana ni msaidizi kapewa na bwana
Ukamlaki moyoni kwa pendo lenye kusuluhisha yote
Kwa uvumilivu uwe mwalimu kwake kumfundisha yote
Shida zake zote ni jukumu lako ujue kumsitiri
Umfundishe kumuabudu huyu Mungu wa baba zako
Haya inuka we bwana harusi ukamlaki bi harusi
Heko kwako bi harusi kwa kutimiza ahadi,Mungu akuajalie maisha mema wendako
Heshima hiyo hiyo,kaidumishe wendako,amani uendako iwe nawe daima.
Hongera ewe dada yetu kwa uvumilivu wako,uvumulivu ulonyesha ni heshima kubwa sana - heko
Uliheshimu wazazi pamoja nalo kanisa,pamoja naye kiongozi nasi waumini wote-heko
Heshima ulioonyesha kaidumishe uendako,ili amani ya nyumbani iwe nawe daima-heko
Ukawe wewe msaada kwa mume wako ee dada,ukamlinde na mabaya ya dunia hii dada-heko
Ukawe wewe mtiifu kwa mume wako ee dada,ili Baraka za nyumbani ziwe nawe daima-heko
Mfano mwema umeacha ili kwamba ukaigwe,wanaotaka ushindi huo wazifuate nyayo zako.-heko
Twakuombea ufanisi wa nyumbani mwako dada,Mungu wake mwanzilishi akupe Baraka zake.-heko
Maisha mapa unayaendea dada yetu hilo kumbuka
Ukawe mtulivu nyumbani kila neno weka maombi
Mashauri uwe mharaka hapo ndipo utafaulu
Furahia kuwa na mumeo dada tunakupa pongezi
Weka Mungu wa mwanzilishi mbele katika shida katika raha.
Mke mwema ni nani awezaye kumuona,maana kima chake chapita kima cha marijani.
Ndoa hii inafungwa(kama)ilivyo desturi ya ndoa,basi ili iwe takatifu mkaudumishe utakatifu kama roho alivyonena (nanyi)msipotoshe hata neno.
Nyumba yenu mtaijenga (vyema) panapo mapatano mema, matengano chuki na vita huondosha pendo lenu,mnaporuhusu haya yote ndio mwanzo wa kuanguka.
Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye, bali mke mwenye busara mtu hupewa na bwana,bali mke mwenye busara mtu hupewa na bwana.
Siku uu baada ya siku, siku zaenda mbele mwanadamu usisahau mausia ya Mungu wako.
Siku baada ya siku ulimwengu wabadilika mwanadamu usisahau mausia ya Mungu wako nakuonya mi mwenzangu ee.
Ndoa sio mchezo wa kuoa na kuachana mwanadamu ujihadhari ulimwengu umefika hapo hivi sasa nakwambia ee.
Ulimwengu umeharibika zo anasa za kila aina zaenea ulimwenguni mwanadamu ujihadhari hivi sasa nakwambia ee
Yo mapambo ya kila aina na mavazi ya kila aina yenye kuchukiza Mungu yaenea ulimwenguni tabu gani hivi sasa ee.
Wo ulevi na uzinifu vinaenda sambamba sana starehe zipendezazo mwanadamu ila chukizo kwake Mungu baba yetu ee.
Yo magonjwa ya kugofya yaenea ulimwenguni mwanadamu si ughairi urudie muumba wako bwana Yesu akusihi ee.
Hiyo ndoa kutoka mwanzo si kuoa na kuachana lo kaburi peke yake ndilo lenye uwezo huo wa kutenganisha wawili ee.
Ye shetani mlaaniwa kongozi wa maasi yote joka kubwa liharibifu kimbieni mje kwake Yesu wanadamu nawambia ee.
(Tazama bwana harusi aliyekando yako,mkono wa kushoto,amekuwa wako,mkamate mkono,mkono huo uwe wa moyoni.
Mkamate mkono kwa kila jambo ajapoghafilika ni kipenzi tu mkamate zaidi umuonyeshe njia katika maisha)
Pongezi kwenu ndugu mpendwa na dada yetu mu kitu kimoja.
(Mmekuwa mashahidi)-(Tumekuwa mashahidi)-(Pongezi kwa ushindi)-(Twawaona mmeng’ara)-(Twafurahi sisi sote)-(Twawaombea Baraka)-(Shangwe na vigelegele)
-Tazama dada yetu tumekuja tumashahidi,hiyo heshima yako kwani imetuvutia
Uliwaheshimu wazazi wako kweli kweli,ulichokipanda sasa ndicho unachovuna
-Kwa tamaa za mwili ulipanda utulivu ndipo,twashuhudia ndoa takatifu wavuna
Uliyaheshimu maongozi ya kanisa,hakika lawapa moyo waliokuongoza
-Umetuheshimu sisi wenzio waimbaji,mfano umetupa ili kwamba tukuige
Tunakuombea Mungu wetu wa mwanzilishi,akujaze Baraka zake maishani
-Heshima hiyo hiyo kaidumishe uendako,ili matunda mema yapate kuendelea
Mungu sidhalimu aisahau kazi yako,pendo hilo likadhihirike kwa jina lake.
Wakala wakanywa yeye na watu waliokuwa pamoja naye,nao wakakaa usiku nao,wakakaa usiku.x2
Wakaondoka aa asubuhi naye akasema nipeni ruhusa niende kwa bwana wangu,niendee kwa bwana wangux2
Ndugu zake na mama yake wakasema, msichana na akae kwetu, kama siku kumi zisipungue baadaye aende.x2
Naye akawaambia msinikawishe, mradi bwana amefanikisha njia yangu,nipeni ruhusa niende kwa bwana wangux2
Dada akoshinda mtieni moyox3
Mtieni moyo azidi kwenda mbele kwa bwana Yesu
Dada akishinda mtieni moyo, dada akishinda mtieni moyo,dada akishinda mtieni moyo,Dada akishinda mtieni moyo wapendwa.
Si neno jema kumvunja moyo aliyeshindiwa vita vikali na bwana,si neno jema a kumvunja moyo aliyeshindiwa vita vikali na bwana
Mtieni moyo apate amani,mtieni moyo apate furaha ya bwana,mtieni moyo oo mtieni moyo azidi kwenda kwa bwana
Dada akishinda mtieni moyo,dada akishinda wapendwa mtieni moyo oo dada akishinda mtieni moyo, mtieni moyo azidi kwenda mbele kwa bwana
Mtieni moyo apate furaha,mtieni moyo apate Baraka mtieni moyo wapendwa mtieni moyo,mtieni moyo azidi kwenda mbele kwa bwana Yesu.
Tukuza jina lake bwana wa majeshi-tukuza (tukuza-tukuza)x4
Himidi jina lake bwana wa majeshi,-abudu jina lake bwana wa majeshi,- chezea jina lake bwana wa majeshi,-inua jina lake bwana wa majeshi,-bariki jina lake bwana wa majeshi,-imbia jina lake bwana wa majeshi
-Deni yangu ya dhambi,Yesu amelipa
Kwake msalabani,nilipewa uzima
deni ya dhambi,msalabani,ilimalizikia, ni huru kabisa
-Bwana Yesu asema,mwanangu dhaifu
Uwezo na ushindi,hupaikana kwangu
- Bwana kweli naona, nguvu zako pekee
Huondoa ukoma niwe kipya kiumbe
-Sina wema moyoni,nidai neema
Nakubali kabisa,kwa damu kusafiwa
-Hata huko mbinguni,miguuni pake
Yesu alinifia, nitaimba milele
Ni ujumbe wa bwana, aleluya,wa maisha ya daima
Amenena mwenyewe,aleluya,utaishi ukitazama
-Tazama, ishi sasa, kumtazama Yesu
Amenena mwenyewe aleluya, utaishi ukitazama.
Ni ujumbe wa wema,aleluya,nawe shika rafiki yangu
Ni habari ya raha,aleluya,mwenye kuinena ni Mungu
Uzima wa daima,aleluya, kwake Yesu utauona
Ukimtazama tu,aleluya, wokovu upweke wa bwana.
Huyo ndiye anashuka aliye tufilia,wengi waliookoka wakimfurahia
Aleluya,Aleluya, Yesu aturudia
Sote tutamtazama amekaa kitini,nao waliomchoma kumkaza mtini
Na kilio, na kilio wamuone enzini
Alama za kifo chake hata sasa anazo, na waaminifu wake wapendezewa nazo
Alipata,alipata kwetu alama hizo
Wokovu utakiwao sasa wapatikana,na watakatifu hao mbinguni wakutana
Kumlaki,kumlaki ndiyo siku ya bwana
Wakusujudie wote mbele ya kiti chako,zako bwana nguvu zote itwae milki yako
Njoo bwana,njoo bwana sisi tu watu wako.
- Waitwa mwovu na bwana,umwendee hima sana
Usafiwe dhambi zako,humwoni ni mwema wako
-Unaitwa itika tu,umwendee bwana Yesu
Sifiche makosa yako,uungame dhambi zako,kristo tu umwamini ndiyo njia ya mbinguni.
- Alilipa damu yake ili kukukweza kwake
Alikufa yeye bwana mimi nawe tuwe wema
-Ukifanywa kuwa mwema mwishoni utasimama
Utaingia rahani na wapenzi wa zamani
-Ni manga tu nchi ile uovu hauko kule
Kama wataka ufike sharti huku uosheke
-Anipenda ni kweli,Mungu anena hili
Sisi wake watoto,kutulinda sizito
-yesu anipenda,Yesu anipenda
Kweli anipenda, Mungu amesema
-Kwa kupenda akafa,niokoke na kufa
Atazisafi taka,sana ataniweka
-Anipenda kabisa,niuguapo sasa
Anitunza mbinguni,niliyelala chini
-Kunipenda haachi,tu sote hapa chini
Baada ya mashaka,kwake tanipeleka
- Yesu kwetu ni rafiki,huambiwa haja pia
Tukiomba kwa babaye,maombi asikia
Lakini twajikosesha,twajitweka vibaya
Kwamba tulimwomba Mungu – dua angesiki
-Una dhiki na maonjo, una mashaka pia
Haifai kufa moyo,dua atasikia
Hakuna mwengine mwema,wakutuhurumia
Atujua tudhaifu – maombi asikia
-Je hunayo hata nguvu,huwezi kuendelea
Ujapodharauliwa, ujaporushwa pia
Watu wangekudharau wapendao dunia
Hukwambata mikononi – dua atasikia
Ninamwimbia bwana maana nimepona
Nitamchezea –Nitamtolea-Ninamsifu-Ninamwabudu-Ninamrukia-Ninamuinua
-imba imba
-cheza cheza
-sifu sifu
-ruka ruka
- toa toa
(Tufurahi tena tumsifu, tuamini kwake
Tufurahi tena tumsifu, Mungu wetu wa zamani)x2
-Ni yeye Yule Mungu wetu wa zamani
(Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka,Mungu wa Danieli,Mungu wa Yakobo)
-Waliokombolewa na damu ya Yesu hupewa maarifa ya kumshinda shetani.
-Waliojazwa roho mtakatifu hupewa maarifa ya kumshinda shetani.
(Hupewa maarifa) ya kumshinda shetani
(Yesu ni bwana anastahili sifa) Yesu ni bwana anastahili sifa
Anastahili sifax4
Piga kelele usiache,paza sauti kama tarumbeta
Uwahubiri watu wa Mungu kosa lao,Na dhambi zao piga kelele usiache
Piga kelele dunia imeharibika,na ulimwengu umejaa fujo,uwahubiri waje kwa bwana Yesu, kuna amani, kuna furaha na uzima.
Piga kelele wote waache dhambi, kwa kuwa dhambi yaleta magonjwa,uwaeleze wabaya hawana amani,piga kelele mchungaji wasikie
Piga kelele uzinifu dhambi mbaya na wazinifu hawana akili,wasipoacha dunia itawameza na jehanamu inawangoja kwa hamu sana
Piga kelele wote wajue kutubu na kuungama ndiyo silah ya kuingia mbinguni kwa baba Mungu,piga kelele mchungaji usichoke.
Piga kelele kazi ya Mungu mbele na makanisa yataka kujengwa,uwaeleze watoe kwa kazi ya Mungu wasilegee Baraka ziko zinawangoja.
Paza sauti wote wawe na umoja na upendo wa ndugu udumu kusudi moja amani na watu wote ndo lengo letu tujitahidi tusiliache.
Piga kelele usiache paza sauti kama tarumbeta uwahubiri watu wa Mungu kosa lao ukinyamaza nani mwengine atasema.
Wala tusiache kukusanyika pamoja,kama ilivyo desturi ya wengine
Bali tuonyane na kuzidi kufanya hivyo,kwa kadiri muonavyo siku ile kuwa ina karibia
Basi kuonywa na kurudiwa ni fungu la wote,akubaliye atafanywa kuwa mwana.
-(basi tunapokusanyika kanisani huyu Mungu, hutuonya kupitia kwa muhubiri)
-(hata unapoona magonjwa yamesimama ni mojawapo ya njia mungu hutumia kukuonya)
-(kiongozi wako anaweza kukukemea ni mojawapo ya njia Mungu hutumia kukuonya.)
-(basi ee ndugu unapoona shida yoyote imesimama ni kurudiwa kubali nawe utakua mwana.)
Basi chagua kuwa mwana,chagua kuwa mwana,usiwe mwana wa haramu
Ndugu,dada basi chagua kuwa mwana nawe kweli utafunguliwa.
(Tukisoma mathayo kumi na tano msitari wa kwanza hadi kumi na nne,mafarisayo walichukizwa na mambo waliyoyafahamu vyema katika torati.)
-unaimba na kuchukizwa ni yale uyaimbayo maana huyapendi
(Ukipofu basi) waongozaje mwengine njia usiyoiona
-kila pando, asilolipanda baba wa mbinguni,ooh litang’olewa,ooh litang’olewa
Na kipofu, kiongoza kipofu mwenzake watatumbukia shimoni wote wawili.
-Wahubiri na kuchukizwa ni yale uhubiriyo maana huyapendi
(ukipofu basi) waongozaje mwengine njia usiyoiona
-Wasikiza na kuchukizwa ni yale usikizayo maana huyapendi
(ukipofu basi) waongozaje mwengine njia usiyoiona
Fungu jema ni kukaa miguuni pa Yesu x3
-Martha kahangaika sana akawa na shughuli nyingi fungu lililobaya
(nawewe ujue) fungu jema ni kukaa miguuni pa Yesu
-Kuwa miguuni pa Yesu ni kujinyenyekeza kwa bwana,kuachana na dhambi kabisa shetani hatakukaribia.
(Na jamii ya walio amini walikuwa na moyo mmoja walikuwa na roho moja na pia vitu vyote shirika.)
(Walipouza viwanja) walileta kwa umoja
(Walipouza mashamba) walileta kwa umoja
(Walipouza wanyama) walileta kwa umoja
(Walipouza mazao) walileta kwa umoja
Kwa sababu walikuwa na umoja,roho zao zilikuwa pamoja,kazi zao walifanya kwa umoja, na pia kila kitu shirika
(Nasi sote tujiunge na umoja roho zetu tuziweke pamoja kazi zetu tuzifanye kwa umoja, hakika tutaona Baraka)
(Wakati wa mikutano) tuifanya kwa umoja
(Na kujenga makanisa) tuyajenge kwa umoja
(Na kueneza injili) tueneze kwa umoja
Kama vile mitume wa zamani walikaa kwa umoja naye Yesu,waliomba pamoja naye Yesu wakaona uzima wa milele.
6.DEMA (VOL 19)
Deema, Deema, Deema
Alimkataa mtu wa Mungu (muhubiri Paulo) (kwa kufuata) dunia ya sasa.
Kiupenda ulimwengu wa sasa tamuacha Muhubiri anayetumiwa na Mungu
Imani huja kwa kusikia muhubiri
(Ndipo) utashida dhambi
(Ndipo) utashida shetani
(Ndipo) utashida dunia
Jitahidi upesi kuwa na muhubiri
Ni askari ni gani aendaye vitani,kwa wakati wowote kwa garama zake mwenyewe
Ni nani apandaye mizabibu asiyekula katika matunda yake
Au nani achungaye kundi asiyekunywa katika maziwa ya kundi
(Ewe ndugu jitoe) -Ewe ndugu jitoe kwa mali zako kugaramikia injili
(Seheemu ya mapato)-Sehemu ya mapato katika kazi zetu iwe ya injili
(Na tuuze tulivyo)-Natuuze tulivyonavyo kwa ajili ya kazi ya injili
(Kama zakayo nawe)-Kama zakayo nawe ndugu jitoe na nusu ya mali yako
(Tujitoe kusima)-Tujitoe kusimamia nyumba za waendao kwa injili
(Atakaye kaazi)-Atakaye kaazi ni lazima akubali kugaramika
(Atakaye wokovu)-Atakaye wokovu ni lazima akubali kugaramika
-Mwenye kuangalia upepo hatapanda naye ayatazamaye mawingu hatavuna
Asubuhi panda mbegu, panda mbegu,mbegu zako
Wala jioni sizuie mkono wako,mkono wako.
Kwa maana wewe hujui, wewe hujui, ni zipi zitakazo fanikiwa.
Kama ni hii au hii au kama ni zote zitafaa sawasawa.
-Wapeni, wapeni watu vitu nanyi mtapewa
(mtapewa) kipimo cha kujaa nakushindiliwa
(shindiliwa) na kusukwasukwa hata kumwagika.
Tafuteni sana kwa bidii kuwa na amani na watu wote na huo utakatifu,ambao bila huo hutamuona Mungu.
Je una amani na wazazi wako- Je una amani na wanyumbani mwako-Je una amani na wahubiri wako-Je una amani na wakuomgozao
Ikiwa hakuna tafuta,Ikiwa hakuna tafuta.
Lakini pasipo, pasipo imani, haiwezekani kumpendeza
Kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yupo.
Na kwamba huwapa thawabu wote wamtafutao.
(Mtazame abeli alivyokuwa nayo imani yakumtolea Mungu dhabihu iliyo bora)
Alimtolea Mungu dhabihu iliyo bora kuliko kaini
(Kwa imani nuhu akishakuonywa na Mungu kwa habari za mambo yale yasiyoonekana)
Hivyo alimcha Mungu kajenga safina aokoe nyumba yake
(Hata sara naye alipokea uwezo wa kuwa anayo mimba kwa ajili ya imani)
Maana alimuhesabu yeye aliyeahidi kuwa mwaminifu.
(Ibrahimu alimtoa huyo Isaka kwa imani na isaka kabariki yakobo na Esau)
Yakobo hata Yusufu waliweka ahadi ya kufa kwa imani
(Muone Musa naye kuwatoa waisraeli kwa utumwa wa misri kulihitajika imani)
Nao walivuka shamu kwa imani wakavunja kuta za Yeriko
(Basi sasa jamani wakati singenitosha kuwaleteni habari za wote wenye imani)
Bali uwe na imani ukawe nayo hakika ukitarajia.
Sol: Ndugu zangu, kuna njia mbili za mwanadamu achague mwenyewe, njia nyembamba ni ya watakatifu, walio na matendo, na mawazo safi mbele za Mungu.
All: Hapo patakuwa na, njia kuu na njia, nayo itaitwa ni njia ya utakatifu
(Instruments)
Sol: Na njia pana ni ya watu wenye kiburi, wasiotaka kuziacha njia zao chafu, nao wataangamia.
All: Hapo patakuwa na, njia kuu na njia, nayo itaitwa ni njia ya utakatifu.
Sol: Ijapokuwa waendao katika njia ya utakatifu, waonekana kuwa wajinga, lakini hakuna hata siku moja watapotea kamwe
All: Hapo patakuwa na njia kuu na njia, nayo itaitwa ni njia ya utakatifu
(Instruments break)
{
(Instruments)
All: Wasio safi hawatapita juu yake njia hii kamwe.
(Instruments)
All: Bali itakuwa kwa ajili ya watu wale wasafirio.
}x2
Japo kuwa wajinga hawatapotea njia hiyo x3
Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, yatafakari maneno yake mchana na usiku.
Ukatende sawa na maneno yote yaliyoandikwa humo,ndipo utafanikisha njia yako na kusitawi sana.
Vitabu vingi vimejaa vyapotosha watu wa dunia,wavipenda kuvitafakari mchana na usiku.
Wanatenda sawa na maneno yote yaliyoandikwa humo,navyovimepumbaza fahamu zao na kuchafua sana.
Vitabu hivyo vya zinaa ujambazi na ushirikina,vyafunza maendeleo kinyume cha maadili yake Mungu.
Vimewapotosha wengi sana na kupagawa na mashetani,hata wamesahau kitabu hiki, hwakitaki kabisa
Kitabu hiki cha torati ndicho Bibilia takatifu, maneno yake yanaokoa yanaponya yanabariki.
Yanatuunganisha na Mungu,yanatupa haki mbele za Mungu wayafuatao wapata uzima,duniani na mbinguni.
Siku hizo Hezikia akaugua,akawa katika hatari ya kufa
Naye akamlilia mungu sana sana, Mungu akayasikia maombi yake.
(Isaya nabii mwana wa Amozi, akamjia akamwambia)
Bwana asema hivi, Tengeneza mambo ya nyumba yako, maana utakufa wala hutapona.
Moyo mgumu ukatae, tangu hivi sasa, jibidishe kuyafata maonyo ya roho
Maana kunayo hatari ya kuangamia, na neno la kukuponya likaribu nawe.
(Muhubiri anatumiwa na Mungu kukuonya uiache dhambi)
Mbona usikubali, ni huzuni kubwa kwa mtu Yule asiyekubali,kutii maonyo, ambayo nabii, mteule wake Mungu baba yetu huyasisitiza.
Kama vile Hezekia livyo lia sana, Mungu akamuongeza siku za kuishi.
Basi nawe jichunguze uko hatarini,huna amani uzima sababu ya dhambi.
(hatua ambayo imebaki sasa ni ile ya kumwendea)
Mungu kwa machozi,ukiomba sana,tena kwa majuto,juu ya maovu uliyoyatenda
Ukitubu sana Mungu wa rehema atakusamehe nawe utapona.
(Huyu Mungu wetu hazeeki),Huyu Mungu wetu hachakai, habadiliki ni wa milele.
Aliweza kusamehe dhambi, hata sasa bado asamehe
Aliweza kupomya magonjwa, hata sasa bado anaponya
Aliweza kubariki watu, hata sasa bado abariki
(Nisisi) nisisi twabadilika,(yeye Mungu) yeye Mungu habadiliki
(Alosema) Alosema hatajuta,(tugeuke) tugeuke kwake yeye
(Ye ni Mungu) Ye ni Mungu ,wakaribu,(tukimwita) tukimwita taitika
(Katwaa mkate kaumega kawapa wanafunzi)x2
(Akawaambia) mwili wangu huu ninautoa ni kwa ajili yenu, Fanyeni hivi kwa ukumbusho, bila kuacha kamwe.
(Katwaa kikombee kakinywea kawapa wanafunzi)x2
(Akawaambia) kikombe hiki agano jipya katika damu yangu, damu hii inayomwagika kwa ajili yenu.
Kwa kuwa kila atakayeliita jina la bwana (huyo)-Huyo ndiye ataokoka
Basi wamwiteje yeye wasiyemuamini, Tena wamwaminije yeye wasiyemsikia,
Tena wamsikieje pasipo muhubiri, Tena wahubirije wao wasipopelekwa
Kama ilivyoandikwa ni mizuri kama nini, miguu yao wahubirio habari ya mema
(Wewe u miguu yao wahubirio mema,umewasafirisha sababu ya injili)
(Wewe u miguu yao wahubirio mema,umewapa mavazi sababu ya injili)
(Wewe u miguu yao wahubirio mema,umewalisha mema sababu ya injili)
(Wewe ni miguu yao wahubirio mema,umewavisha nguo kwa sababu ya injili)
(Wewe u miguu yao wahubirio mema,kama bado anza leo sababu ya injili)
Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa
Afanya jambo litakalo mwangamiza nafsi yake
Hizo ni habari kwa ulimwengu aliyeyasema ni Mungu baba yeye alisema tena hajuti ataadhibu atadhibu.
Hata mkihalalisha zinaa kwa kusema eti tumia kinga bado unabaki ni uzinifu vita ni zinaa wala sio kinga
Magonjwa ni hayo ya zinaa ndiyo adhabu kwa wazinio mwatafuta dawa hamtapata dawa ni kuacha hizo zinaa
Watendao dhambi duniani hukumu yao ni jehanamu haijalishi watumia kinga haitakukinga na jehanamu
Mnapohubiri semeni kweli hubirini neno hili waziwazi hata mkiomba maombi mengi dawa ni kutii neno lake Mungu
Tulihubiripo neno la Mungu na tusome kitabu cha Mariko sura ni ya nane thelathini na nane tusiionee haya injili.
Muongofu aliyevuguvugu ni makao ya shetani,
Ubaya wote uwe najisi kwako ewe mtu wa Mungu
Jihadhari na wale watendao mabaya na wale wanaojikataa
Kwanini uishi kama popo humnyama wala ndege
Hueleweki ulikosimamia ewe mtu mwongofu
Jihadhari bwana Yesu asikutapike ni neno lililo la hatari
Ni heri ngekuwa moto sana au baridi kabisa
Bwana Yesu alionya siku zile bado anakuonya
Jihadhari kushikilia vyote viwili maana takuwa wa shetani.
Naamani mtu wa heshima akaugua ukoma,(ooh) akamwendea muhubiri Elisha,
Elisha akamuagiza aoge mto Yordani. Mara saba atapona kabisa.
Kinyume cha alivyotarajia Naamani kakasirika (ooh) akarudi na ukoma wake.
(Mimi nalidhani ataomba kwa Mungu wake na kuniponya mimi mwenye ukoma, je mto rabana pia na mto Faripari sibora kuloko mito yote ya Israeli)
Je siwezi kujiosha ndani yake( na kuwa safi),kageuka akaondoka kwa hasira
Baadaye Naamani kakubali (kanyenyekea), akapona mwili wake ukawa safi
Wewe unazoshidanyingi mwenzangu (mateso mengi) ukishika la muhubiri utapona
(Panda mbegu) asubuhi, (panda mbegu) na jioni
(Hujui ni ipi) (ipi) itakayofanikiwa
Kupanda mbegu ni kumtolea Mungu (uwe mtumishi) kila mara kila saa
Kupanda mbegu ni kumtolea Mungu (kila mara toa) sadaka zaka kamili
-(Mtolee) baba Mungu, (dhabihu za) kushukuru
(na mtimizie)(zie) muumba nadhiri zako
Ukaniite siku ya mateso nitakuikoa na wewe tanitukuza
-(Muheshimu) baba Mungu (kwa mali) yako yote
(Na kwamalimbuko)(mbuko) ya mazao yako yote
Ndipo ghala zako zitajazwa kwa wingi, mashinikizo yafurike divai mpya
(Agano la utajiri wa Yakobo lilitokana na) – kumtumikia baba Mungu
(Agano la mali ya Ibrahimu lilitokana na) – kumtumikia baba Mungu
(Kufufuliwa kwa Thabitha sababu ni) – kuntumikia baba Mungu
(Uwezo juu ya shida uponyaji takupa) – ukimtumikia Mungu
(Imani ya kukemea pepo pia takupa) – ukimtumikia Mungu
(Baraka ya pesa, uzima pia takupa) – ukimtumikia Mungu
Upendo, upendo, Upendo, upendo.
Upendo wa kwanza umekwenda wapi.
Mwanzo wa wokovu wako ulishangaa,ukasema hakika huyu Yesu anipenda
Hatimaye wokovu ukauzoea,ona sasa kushangaa kumetoweka.
(Yatafakari maisha ya baba yetu Ibrahimu)
Alihamishwahamishwa na kua mgeni aendako
(Hata yakobo ndugu yetu na waisraeli wote)
Walihamishwahamishwa na kuwa wageni waendako
(Ili wasipate uenyeji wamtafute Mungu wao)
Walihamishwahamishwa na kuwa wageni waendako
(Kwani mgeni siku zote mambo yote kwake ni mapya)
Yeye huyo hujifunza na kumpendeza bwana wake.
Sasa wokovu wako ni wa kawaida hakuna jambo tena sasa likushangazalo
Wokovu ni kujifunza kila wakati, jilinde sana na uenyeji wokovoni.
(Hata hivyo maandiko yasemaje kwa habari za siku za mwisho,upendo wa wengi utapoa nayo maasi yataongezeka)
Bali ninakushauri wokovu wako takuwa imara kwa hali ya ugeni
Wokovu wa kwanza umekwenda wapi
Imani ya kwanza imekwenda wapi
Upendo wa kwanza umekwenda wapi.
Watulizeni mioyo watulizeni watu wangu
Asema Mungu asema,asema Mungu wetu
Semeni na mioyo ya watu wangu kawambieni kwa sauti kuu ya kwamba vita vimekwisha, hizo dhambi zao wamesamehewa kwa kuwa wameshaopokea adhabu yao maradufu kwa dhanbi walizozitenda.
Warudisheni kwa upole mkiwafahamisha hayo maovu yao ndiyo yawaelekezayo kuangamizwa, sibure, sibure mwanadamu ahangaikavyo bali anapotubu maovu yake Mungu baba atamrehemu.
Watulizeni watu katika kutubu,watulie katika kuendelea kutubu
Watulizeni watu katika kutoa,watulie katika kuendelea kutoa
Watulizeni watu katika kuomba,watulie katika kuendelea kuomba
Watulizeni watu kwa kutakasika,watulie katika kuendelea kutakaswa
Watulizeni..watulizeni
Ikiwa mtawafundisha watu wa Mungu jinsi ya kutubu dhambi na kisha muwafanye waendelee kudumu kutubu,hapo mmewatuliza watu wa Mungu.
Ikiwa mtawafundisha watu wa Mungu jinsi ya kuomba na kisha muwafanye wadumu kuendelea kuomba,hakika mmewatuliza watu wa Mungu.
Ikiw a mtawafundisha watu wa Mungu jinsi ya kumtolea na kisha muwafanye wadumu kuendelea kumtolea Mungu, hapo mmewatuliza watu wa Mungu.
Ikiwa mtawafundisha watu wa Mungu jinsi ya kutakasika na kisha muwafanye wadumu kuendelea kutakasika.
Ahsanteni,mumewatuliza watu wa Mungu
Watulizeni, watulizeni watu wa Mungu.
Wote wawe na umoja kama baba ulivyo ndani yangu, name ndani yako nao wawe ndani yetu.
Wote wawe na umoja,ulimwengu usadiki ya kwamba ni wewe uliyenituma.
Wote wawe na umoja wa kuziacha dhambi
Wote wawe na umoja wa kuungama maovu
-Wote wawe na umoja kuishi kitakatifu
Wote wawe na umoja kujenga makanisa
Wote wawe na umoja wa kuenea injili
-Wote wawe na umoja kutii maongozi
Yesu hachukui dhambi ya mtu kwa nguvu (hakika)
Maana huo wokovu ni wa hiari ya mtu
Peleka dhambi yako mwenyewe na Yesu ataichukua haraka(haraka haraka)
Mtazame mtazame mwana kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi
(Ya ulimwengu) Ya ulimwengu
(Aichukuaye) dhambi ya ulimwengu huu
Wewe wateseka maana yo dhambi yako (hakika)
Haijachukuliwa nay eye bwana Yesu.
Kwa hivyo hizo kazi za dhambi (lazima) utaziona dhahiri
(dhahiri dhahiri) mtazame mtazame mwana kondoo wa mungu aichukuaye dhambi
(Mbona unaishi muongo) – hiyo ni dhahiri dhambi hiyo bado haijachukuliwa
(Mbona unaishi mzinzi) – hiyo ni dhahiri dhambi hiyo bado haijachukuliwa
(Mbona unaishi mwizi) – hiyo ni dhahiri dhambi hiyo bado haijachukuliwa
(Mbona unaishi mpingaji) – hiyo ni dhahiri dhambi hiyo bado haijachukuliwa
(Mbona unaishi na chuki) – hiyo ni dhahiri dhambi hiyo bado haijachukuliwa
(Mbona unaishi na dharau) – hiyo ni dhahiri dhambi hiyo bado haijachukuliwa
(Mbona unaishi na kiburi) – hiyo ni dhahiri dhambi hiyo bado haijachukuliwa
(ukitaka kuishi mwongofu) – leta dhambi yako, kwake bwana Yesu upate msamaha.
Nimefunguliwa mlango mkubwa wa kufaa sana, Na wako wengi wanipingao
Wakijifunza siku zote ila wasiweze kabisa,kuufikia ujuzi wa kweli.
(Kupona kwa imani)- mlango mkubwa wa kufaa sana lakini wako wengi wapingao
(Kumtolea Mungu)- mlango mkubwa wa kufaa sana lakini wako wengi wapingao
(Kuziungama dhambi)- mlango mkubwa wa kufaa sana lakini wako wengi wapingao
(Kuwa nao umoja)- mlango mkubwa wa kufaa sana lakini wako wengi wapingao
Nawe utakusudia neno maishani,nalolitathibitika kwako siku zote
Na mwanga utaziangazia njia zako
Ukikusudia wokovu,si kama hakuna la kukufanya usiende mbele
(Aa vikwazo viko ndugu yangu wenye kupinga wako wengi na wenye matatizo wako)
(Aa wasiotaka mema wako,wasiotaka umoja wako,wasiotaka amani wako)
Ndugu usilegee kupenda Mungu,zidi kukusudia kutenda mema
(Wewe)- kusudia utakatifu, (wewe) kusudia kutubu dhambi
Utumike kwa Mungu wako (ndipo) mwanga utaziangazia njia zako.
(Siku zile za ujinga Mungu alijifanyax2, kana kwamba haoni kwa dhambi zetu tunazofanya)
(Na sasa) aagiza watubu, watu wa mataifa x2 (kwa kweli) kwa ajili ya dhambi hakika mungu anachukizwa.
(Siku zile zake Nuhu wengi walipotezwax2, kama sodoma na gomora ilichomwa kwa moto.
(kwao) walionywa na dhambi wao wakakataa (Na ndipo oo) bwana Mungu akawaangamiza kwa garika na moto x2
(Mungu hatendi jambo wapendwa bila ya tahadharix2, hukuonya na dhambi kabla yeye akupoteze)
(Na sasa) mtumishi wa Mungu yeye anatuonya (wapendwa) tuachane na dhambi ili tuepukane na mapigo.
Sote tufurahi kwa kuwa Mungu ameshatimiza (ahadi yake)
Yakutuinulia nabii, atakaye tueleza kweli yote Mungu atakayo.
(Watu wote) njoni natumkaribishe mwetu moyoni
Elimu zetu tuache, pia na kujua kwetu, tuone uwezo wa Yesu
Hivyo uko hapa na utaraji jambo jipya leo, (bila kukosa)
Na ukauone uwezo atakao kupa bwana, hivi sasa Mungu atukuzwe.
Kila mtu ajue kuuweza mwiili wake mwenyewe,si katika hali ya tama mbaya (kama mataifa) wale wasiomjua Mungu.
Kila mtu ajue kuuweza mwili wake mwenyewe,katika utakatifu na heshima
(Heshimu mwili wako) nawe utakaa salama
Kuheshimu mwili katika mavazi ya kujisitiri ni kuuweza mwili
Kuheshimu mwili kutoyabadili hayo maumbile ni kuuweza mwili
Kuheshimu mwili katika kuacha dhambi za zinaa ni kuuweza mwili
Kuheshimu mwili kwa kuutiisha kiutakatifu ni kuuweza mwili
Kuheshimu mwili kuyazingatia maadili ya Mungu ni kuuweza mwili
Yesu uu Yesu, ni yeye Yule, habadiliku kamwe ni yeye mwanzo na mwisho
Yesu ndiye njia ya kweli na uzima yeye amwaminiye atapata pumzishwa
Damu ya thamani inayomwagika ni kwa ajili yako upate kutakasika
(Muite bwana Yesu uwapo matesoni au mashakani,hata kama umefungwa na mashetani wa aina gani,muite Yesu sasa nawe utapata pumziko la milele)
Muite bwana matesoni, mashakani, kifungoni, yote bwana alitwaa,ili tupate uzima
Heri wamngojeao bwana maana hawatachoka, maana hawatazimia, watapewa nguvu, nguvu, nguvu mpya.
Umngojee bwana kwa kupenda watu
Umngojee bwana kwa kumtolea
Umngojee bwana kwa utakatifu
Umngojee bwana katika maombi
Bwana atakupa nguvu kwenye kupenda watu
Bwana atakupa nguvu kwenye kumtolea
Bwana atakupa nguvu kwenye utakatifu
Bwana atakupa nguvu kwenye maombi yako
(Ni makosa kusema unamngojea bwana na huku una nia mbili moyoni mwako,
Unapendezwa na chuki,uzinzi,ulevi,manung’uniko,masengenyo,ibada za sanamu, na huku unadai mambo mengi kutoka kwa kristo Yesu,utachoka.
Nguvu mpya za kukupa haja za moyo wako hazitakuja, ni heri kuamua kuzaliwa upya katika roho, upate kuenda kitakatifu, na lolote utakaloomba kutoka kwa bwana utapata)
Mimi ni Mungu wa wote wenye mwilix3
Kuna neno gani gumu nisiloliweza
Nilimtokea Musa kwenye kijiti, kikiwaka moto kule mlimani
Nikamjulisha mimi ndiye Mungu,niliyekuwako nipo na nitakuwepo
Niliokoa wana wa Israeli,wakapasua bahari wakavuka
Nikawapa maji na chakula jangwani,kuna neno gani gumu nisiloliweza
Danieli alitupwa tunduni mwa simba, nikawazuia simba wasimle
Hata asubuhi Danieli ni mzima,kuna neno gani gumu nisiloliweza
(Ndipo neno likamjia Yeremia likisema “mimi ni bwana Mungu wa wote wenye mwili,je kuna neno gani gumu nisiloliweza)
Shadiraki, Meshaki na Abedinego,waliponiita nikawatokea
Nikawaokoa na tanuru ya moto,kuna neno gani gumu nisiloliweza
Nilikuwako niko na nitakuweko,nilikuumba wewe mwanadamu
Jambo gani gumu nisiloliweza,mimi ni Mungu wa wote wenye mwili.
Najifunza kufuata Bibilia, si Bibilia kunifuata mimi.
(Kuunganma dhambi) nikufata Bibilia -(Kupenda watu) nikufata Bibilia
(Kumtolea Mungu) nikufata Bibilia -(Kuwa na umoja) nikufata Bibilia
(Kuuweza mwili) nikufata Bibilia -(Kuomba Mungu) nikufata Bibilia
Ndugu fuata Bibilia - utasamehewa,,-Ndugu fuata Bibilia - upate kupona,,
Ndugu fuata Bibilia - upate baraka,,-Ndugu fuata Bibilia - upate furaha,,-Ndugu fata Bibilia - upate amani
Ewe mwenangu umeshatambua, pendo la Yesu lilivyo kuu kwako,katoa uhai wake msalabani (kwa ajili yako) upate okoka
(Basi sasa) ni wakati uonyeshe pendo lako
(kwani yeye) alishakupenda na akajitoa
Basi hii ndiyo ni siku yako,achana na anasa za ulimwengu,na urithi mema yaliyotayari,pia na uzima ule wa milele.
Wasiokubali (niwatawale) waleteni mbele zangu muwachinje
(Ewe ndugu mwongofu umo kanisani,lakini huoni uponyaji,Baraka,amani na mengine mengi kutoka kwa Mungu,huko ndiko kuchinjwa kunakotokana na kutokubali kutawaliwa na Yesu kristo)
Kukubali kutawaliwa ni kuacha vyote, ni kwenda kinyume cha mapenzi yako,mara unaposikia sauti ya bwana atakavyokuagiza.
(katika mambo yote bwana ananitawala,nisiseme liko moja gumunisiloweza kufuata)
Nisemapo bwana anitawala yanipasa kuacha yaliyo mapenzi yangu nifuate kama apendavyo yeye.
(Atawalikaye hana mambo yake mwenyewe isipokuwa yale ya bwana wake ayapendayo yeye)
(Katika mambo yote bwana unitawale) – nakubali bwana tawala
(katika kutii bwana unitawale) – nakubali bwana tawala
(pia kutakasika bwana unitawale) – nakubali bwana tawala
(kuishi kwa imani bwana unitawale) – nakubali bwana tawala
(nijaze roho wako bwana unitawale) – nakubali bwana tawala
Baada ya kuumba vitu hivi vyote,Mungu katuumba kwa mfano wake
Katupa uwezo juu ya vyote, ili turithi mema yote kwake
(kwanini) waviogopa, wanyama kulia usiku ni kawaida, na ndege kulia usiku ni kawaida, wewe wasema umerogwa, sivunje safari yako ukimkuta kobe njiani, sivunje safari yako ukimkuta mbwa njiani.
Mungu yuko katika neno lake, ukimuamini na atakuponya
Na imani mbaya ulizonazo, naye atakuweka huru kabisa
Yakobo akashindana na mtu mmoja mweleka,naye alipoona ya kuwa hamshindi
Akamgusa panapo uvungu wa paja lake.
Yakobo akateguka uvungu wa paja lake Yule mtu kasema uniache niende, yakobo kasema sikuachi usiponibariki.
(Akamwuliza jina lako nani), akamwambia jina langu Yakobo, (Yule mtu kasema hutaitwa yakobo) na utaitwa jina Israeli.
(Si neno rahisi tu kubarikiwa na Mungu ati “Mungu mwenyewe akipenda atanibariki” la hasha,kumtolea Mungu kwa njia mbali mbali ni kushindana mweleka, utoe kiasi cha kuteguka,katika hazina yako,ndipo utakapo barikiwa,nawe utabadilishwa,jina lako hutaitwa aliyelaaniwa bali utaitwa m’barikiwa)
Shindana mweleka, upate Baraka
(Shindana mweleka,teguka katika mshahara wako,utoe zaka, sadaka,shukrani,nawe utabarikiwa, shindana mweleka,teguka na shambani mwako, toa mazao,lisha wahubiri,nawe utabarikiwa.Shindana mweleka,teguka ujitakase,ungama dhambi za aibu nafsini mwako,nawe utaitwa mtakatifu. Aleluya.)
Angalieni siku inakuja inawaka kama tanuru,wenye kiburi watendao uovu watakuwa kama makapi.
Sol (part 1):
(Lakini kwenu ninyi mnaolicha jina la Bwana jua la haki litawazukia).
All (part 1):
Lenye kuponya katika mbawa zake, asema Bwana wa majeshi
Sol (part 1): """"""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""'
All (part 1): """""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""
Sol (part 2):
(Ufunuo wa Bwana kwa kinywa cha malaki, umefunguliwa ndani ya Mchungaji wa Bwana, ya kwamba kizuizi cha mema ya mtu ni laana kutoka kwa wazazi, Dunia nzima tumsikilize mchungaji wa Bwana maana Mungu amemdhihirisha kuwa Eliya nabii)
All (part 2):
Nitawapelekea Eliya nabii, haijaja siku ile yenye kuogofya.
Ataigeuza mioyo ya baba zao, iwaelekee hao watoto wao.
Na mioyo ya watoto kwa baba zao, nisije nikaipiga dunia kwa laana.
Sol (part 2):"""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""
All (part 2):""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""
Nao walipofika kwake yesu walimsihi sana,wakisema anastahili huyu umtendee neno hili,maana analipenda taifa letu naye alitujengea aa sinagogi.
Anastahili ,Anastahili
Sasa mtumishi wa Mungu yuko pamoja na Yesu,naye atamsihi sana ikiwa utastahili, jambo gani ulilofanya lenya kupenda taifa,acha dhambi tolea Mungu na ndipo utastahili.
Utastahili, utastahili
Ukipenda taifa, utapata mema
Ukitolea Mungu, kupata Baraka
Ukiungama dhambi, kupata wokovu
Nastaajabu kwa kuwa mnamwacha upesi, hivi yeye aliye waita katika neema ya kristo, na kugeukia injili ya namna nyingine.
(Wala si nyingine) – lakini wako watu wawataabishao na kutaka kugeuza injili ya kristo
Lakini iwapo sisi au malaika pia wa mbinguni wakiwahubiria injili yoyote isipokua hiyo niliyowahubiri chasema na alaniwe.
Na kama tulivyo tangulia kusema sasa nasema tena mtu awaye yote akiwahubiria injili yoyote isipokuwa hiyo chasema na alaniwe
Mtu awaye yote siyempenda bwana na awe amelaaniwa mara natha
Hapo mwanzo tuliipokea injili hii kwa machozi mengi,lakini sasa tumekuwa nayo mazoea hata hatushangai,kukusanyika tulikuwa wepesi,kutii Mungu huko kukusanyika,Tulihubiriwa kutoa tukawa,wepesi mno katika kutoa,tulihubiriwa kuacha dhambi,ulevi chuki na zingine nyingi,Na uzinifu,kumwibia Mungu,zaka kamili,sadaka shukurani .hatumwamini liyesimamishwa, tumeongeza dhambi juu ya uovu, Tumetengwa na hayo mema ambayo mwenyezi Mungu alituahidia.Nani aliye waloga hata mbio zile za kwanza hamnazo tena.
Mlikuwa mkipiga mbio vizuri ni nani aliyewazuia msiitii, kweli kushawishi huku hakukutoka kwake yeye anayewaita ninyi watu wa Mungu.
Nikupe nini muumba wangu kwa rehema ulizonitendeax2
-nitakipokea kikombe cha wokovu na kulitangaza jina la bwana
Uovu niliokuwa nao ulistahili dhiki kuu,lakini baada ya dhiki umeniokoa nikupe nini
Hakika ya Mungu yatimia lakini ya shetani hayatimii,alilosema,Mungu baba,hata likikawia litatimia
Nimengi sana Mungu baba aliyokufanyia kwa rehema unawaza nini zaidi ya kuyafuata mapenzi yake.
(Bwana Mungu alimtuma Musa kuwakomboa wana wa Israeli
Walipofika jangwani walianza kumnung’unika Mungu na Musa)x2.
(Bwana akatuma nyoka za moto zikawauma wengi wakafa)x2
Wakamwendea Musa wakasema tumefanya dhambi(tumefanya dhambi) tumemnung’unika Mungu na wewe.x2
(Kwa amri ya Mungu Musa kajifanyia) nyoka ya shaba)x2
(Na kila) aliyeumwa (aitazamapo) ataishix2
Leo mchungaji Musa tunaye tumekombolewa kutoka Misri tumefika kiwango tumeanza kumnung’unika Mungu naye Musa.x2
Magonjwa mengi sisi tunayo matatizo yamekuwa mengix2
(Tumwendee muhubiri tuungame) dhambi zetu zotex2
Haswa manung’uniko kwa watuongozao katika rohox2
( kwa wakati huu nyoka ile ya shaba) ni bwana Yesux2
Na tunapomtazama alipoangikwa tutaishi
Amlaniye babaye au mamaye taa yake itazimika katika giza kuu.
-(kuwawazia mabaya,baba yako na mama yako,baada ya kukutendea,jambo usililipenda,wazazi wajapokosa,hata wawe na hali gani,wewe u mwana huna haki,kurekebisha wazazi)
-(kutoweza lolote,hapa duniani mwenzangu,huwa taa yako imezima,kwa kulani wazazi, taa yako ikizimika,katika hilo giza kuu, huezi kuona chochote,wala kufanya lolote)
-(Jinyenyekeze kwa Mungu,utubu dhambi hii ya laana,utaona mwangaza ndugu,katika maisha yako)
- (Enyi watoto watiini wazazi wenu) katika bwana maana ni haki
(waheshimu baba yako na mama yako) amri hii ndiyo amri ya kwanza
Yenye ahadi upate heri ukae siku nyingi katika duniax2
(atukanaye baba au mama yake) kufa na afe
-(umekufa kiroho ew ndugu yangu) kwa kukosa heshima kwa wazazi
(Huna heri popote uendapo) Tafakari maisha na wazazi wako
Ulipoanza kuwadharau,ukatupa heri ukaokota laana
(Tubu dhambi ya dharau kwa wazazi) utaokoka
-(Tafuta amani na wazazi wako) Tafuta heshima kwa wazazi
(Ukae siku nyingi hapa duniani) uone heri tena hapa duniani
Nyumbani mwako kazini mwako utaona Baraka maishani mwako
(Waheshimu baba yako na mama yakox2) utaokoka
Yatupasa kutii mamlaka kuu,maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu
Natujihadhari, Tusinene juu ya roho mtakatifu
Kwa kuwa ni mtumishi wetu anayetuhudumia
Hutakuwa na uhuru,unenapo juu ya roho
Tenda na udumu kwa la Mungu,uwe mwanafunzi
Tenda na udumu kwa la Mungu uwe mwanafunzi
Mwanadamu hateseki bure,aishipo hapa ulimwenguni
Mwanadamu hateseki bure, dhambi zake ndizo zinazomtesa
Ungama na kutubu upate msamahax3
Kwa dhambi zako ulizozitenda mwenyewe
Mateso hayo uliyonayo,ni adhabu kutoka kwake Mungu
Si uchawi wala maonevu,silaumu bali ujichunguze
Mwenye haki hateseki kamwe,maana yeye ni mtakatifu
Mungu humuepusha na yote,yaliyo kinyume na haki zake
Ni vigumu sana tena sana, mwenye dhambi kuwa kuamini ya kwamba
Masumbufu aliyonayo,dhambi zake ndizo zinazomtesa
Lakini ukweli ni kwamba dhambi ndiyo chanzo cha masumbufu
ya wanadamu wote ili asipotee ni mtu akubali,asishindane kusema yeye hana dhambi
(Aliye na akili moyoni mwake atapokea agizo)
Bali mpumbavu mwenye maneno mengi ataanguka
(Uwapo mbele za muhubiri yapaswa kupoke agizo lile Mungu akuagizavyo leo)
Mungu akuagizapo umtolee,usiwe mpumbavu kusema mahitaji ni mengi maneno mengi yatakuangusha wee,kwa umasikini pokea agizo.
Mungu akuagizapo acha zinaa usiwe mpumbavu kusema haitawezekana maneno mengi yatakuangusha wee,wenye magonjwa pokea agizo tu.
Mungu akuagizapo ujitakase usiwe mpumbavu kusema hilo ni neno gumu, maneno mengi yatakuangusha wee,kwa moto wa milele pokea agizo tu.
Mungu akuagizapo jambo lolote usiwe mpumbavu kutoa hizo sababu zako,maneno mengi yata kuangusha wee, takosa imani pokea agizo
Maneno mengi acha uwe mwenye akili
Usipotoa si agizo agizika kutoa
Usipoomba si agizo agizika kuomba
Kutenda dhambi si agizo agizika kuacha
Kupiga pinga si agizo agizika ukubali
Dhambi ni nini x4
Walimwengu nauliza,walimwengu nauliza jamani dhambi ni nini.
(Kizazi cha leo kuitambua dhambi si rahisi)x2,(kwani dhambi zimehalalishwa zimefanywa kuwa maumbile)x2
(Ni la kushangaza maumbile kufanyiwa sirini)x2,(maumbile ni maumbile kwa wote si haja kuyaficha)x2.
(Je waweza kuwaaga wazazi wako unapoenda kuzini,au umuarifu asikari unapoenda kuiba,kamwambie imsengenyaye naenda kukusengenya,uiambie serikali utafanya ufisadi)x2
Yote ufanyayo na hutaki mwingine ajue,basi jua leo hiyo ndiyo dhambi Mungu haitakix2
(Yesu mwokozi mkaribishe awe shahidi,kwa matendo unayofanya,ndipo ujue kuwa si dhambi)x2
Kama hamuwezi kuwa wazi kwa matendo yenu,basi dhambi sasa ni dhahiri kwenu mwaifanya kwa siri,na matendo mema haya ndiyo huwekwa hadharani,yawe ni mfano yapate kuigwa wala si mabayax3
Makutano makubwax2
Wamo katika bonde la kukata maneno - Wamo katika bonde
Waenda kanisani waenda fanya nini, jee ni kuchunguza au ni kulaumu au kunung’unika hivyo wajisumbua
Mbele za muhubiri huko ni kwenye bonde acha maneno mengi,sikiza kwa makini upate neno lako upasalo kukata.
Ewe mpendwa kata – kata – kata uwe huru
Hasira zako – na vita vyako
Na chuki zako – huo uchungu
Huo uongo – na huo wizi
Ulevi wako – hizo zinaa
Mungu kamwambia Aburahamu toka wewe katika nchi yako na jamaa zako,na nyumba ya baba yako uende katika nchi nitakayo kuonyesha.
Nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa kukubariki na kulikuza jina lako nawe uwe Baraka
Mungu anakuagiza leo toka wew katika nchi yako iliyo na ukabila,nchi iliyo na laana,iliyo na matenagano ooh,yenye chuki na vita
Toka katika nchi hiyo isiyotakatifu,nchi isiyo na umoja na upendo,isiyoungama dhambi,isiyotolea Mungu, nawe utafanikiwa.
NamI nitawabarki wakubarikio naye akulaaniye tamlani,katika wewe jamaa zote za dunia tabarikiwa zote watabarikiwa.
Ninyi mkikaa ndani yangu na maneno yangu yakikaa ndani yenu
Ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa hivyo hutukuzwa baba yangu.
(Kwa vile mzaavyo saana nanyi mtakuwa wanafunzi wangu)
(Ni muhimu ukaa katika neno la Mungu siku zote maana ukiomba Mungu atakusikia)
(waonekana unaomba sana lakini Mungu hakusikii,je unakaa katika maneno ya naniewe mpendwa)
(Kwa kuacha zinaa dharau chuki uongo na fitina ndivyo utakuwa ndani ya Yesu)
(Yesu akusihii uwe ndani yake kwa njia hizi za utiifu,unyenyekevu,upole kiasi,uvumilivu na utumishi)
Tahadhari ndugu yangu usiwe kanisani na sifa mbaya
(wayahudi walio na wivu),watakutwaa wewe mtu ovyo usiye na sifa njema
(wakutumie kulivuruga),na kulitatiza kuchafua kanisa la baba Mungu
Wayahudi kanisani ni wenye wivu na watenda mabaya
Wapenda kunung’unika kulaumu fitina pia dhihaka
(uishipo vuguvugu wewe), watakutia chuki wakukate na hao watu wa Mungu
(nawe dhambi zitakushinda we),aibu utakazoleta zitachafua kanisa zuri
We mwongofu vuguvugu Yesu nataka leo uwe imara, ili wasioamini sikutumie kuvuruga kanisa
(utakuwa ukifatwafatwa), na walio imara wokovuni ili wakutie nguvu
(jitahidi kukaa kwa Mungu), kujifunza la Mungu siku zote katika maisha yako
Tazama katika mji huu kuna mtu wa Mungu ni mtu wa kuheshimiwa asemayo hutokea kweli kweli.
(twende huko) twende huko (labda aweza)labda aweza kutuambia habari ya safari yetu-tunayoedea
Tazama maisha yako ndugu unayo mateso huoni amani ndugu waona kushindwa maishani
(mtu yupi)mtu yupi (akuongozaye) akuongozaye hata maisha yako yanaenda kombo siku zako zote
Tazama siku zako nyingi umepata hasara kukosa kutafuta mtu muonaji wa maisha yako
(anza leo) anza leo (tafuta mtu) tafuta mtu muheshimiwa wa Mungu maishani mwako(ya aweza) ya aweza ( kukuambia) habari ya safari ya maisha yako unayoendea
Mmoja hufa katika nguvu zake kamili,mwenye kukaa salama na kustarehe
Vyombo vyake vimejaa maziwa na mafuta ya mifupani mwake ni laini
Mwengine hufa katika uchungu a roho asione mema kamwe
Wapendwa jilindeni sana na uchungu wa roho, uchugu wauwa ni kitu hatari si uruhusu ukutawale.
Uchungu na mkeo ndugu - siuruhusu ukutawale
Uchungu na mumeo dada - siuruhusu ukutawale
Uchungu na jirani zako - siuruhusu ukutawale
Wengi wamejinyonga,wengi wameacha kazi, wengine wametoroka familia zao kwa uchungu wa roho
(Tahadhari) uchungu na wazazi wako – siuruhusu ukutawale
(Tahadhari) uchungu na watoto wako – siuruhusu ukutawale
(Tahadhari) uchungu na kiongozi wako – siuruhusu ukutawale
(Tahadhari) uchungu na muhubiri wako – siuruhusu ukutawale
(Tahadhari) uchungu na jamaa zako – siuruhusu ukutawale
(Tahadhari) uchungu na mume dada – siuruhusu ukutawale
(Tahadhari) uchungu na mkeo ndugu – siuruhusu ukutawale
(Tahadhari) uchungu na jirani zako – siuruhusu ukutawale
(Tahadhari) uchungu na kiongozi wako – siuruhusu ukutawale
(Tahadhari) uchungu na wazazi wako – siuruhusu ukutawale
(Yesu kawambia wanafunzi amini nawambieni)
Ni rahisi zaidi (ngamia) kupenya tundu la sindano (kuliko) tajiri kuingia (katika)ufaume wa Mungu.
(basi ndugu mpendwa unajua tajiri ni nani,ni Yule mtu asiyetaka kuikana nafsi yake,kuacha maovu yote na dhambi zote za dunia hii ili aenende kitakatifu, mtu kama huyu ni vigumu sana kwake kuurithi ufalme wa Mungu)
(ndipo Petro kamwambia sisi tumeacha vyote tutakufuata basi tutapata nini)
Tutapata nini x3 tutapata nini basi Petro akamuuliza
(Yesu akawajibu akawaambia yeye aliyeacha vyote kwa ajili yangu atapokea mara mia na kuurithi uzima wa milele)
(basi ndugu dada kubali kuacha yote hayo uliyonayo ambayo ni ya kidunia na maovu mbele mbele zake Mungu wako ili uweze kurithi uzima ,uzima wa milele)
(ukiacha dhambi baba)-utapokea mara mia,na kurithi uzima ,uzima wa milele
(ukiacha dhambi mama)-utapokea mara mia,na kurithi uzima ,uzima wa milele
(acha dhambi ndugu)-ukapokee mara mia,na kurithi uzima ,uzima wa milele
(acha dhambi dada)-ukapokee mara mia,na kurithi uzima ,uzima wa milele
Awapokeaye ninyi anipokea mimi, naye anipokeaye mimi, ampokea yeye aliyenituma
Ampokeaye nabii kwa kuwa ni nabii, atapata thawabu ya nabii
Naye ampokeaye mwenye haki kwa kuwa ni mwenye haki atapata thawbu ya mwenye haki
Wewe una mateso ya kushangaza watu wampokea nani hapa ulimwenguni jee ni mtu wa Mungu
Ampokeaye yeyote anaye pinga kweli, utamwona daima anapinga,nayo matunda yake ni mateso vilio visiyokuwa na mlango wowote wakutokea.
Heri siku ya leo ukatee shauri,umpokee Yule mtu aliye tumwa naye mkombozi Yesu
Kila upandacho utavunax2
Ukipanda mabaya utavuna mabaya,ukipanda yo mema utavuna yo mema
Ukiwa na heshima utavuna heshima,ukiwa na dharau sitafute heshima
Ukitaka kupinga endelea kupinga lakini ufahamu hutapata amani yako
Ni heri kuamua kushikamana naye aliyesimamishwa kwa ajili ya wema wako
Mchungaji wa bwana nena kweli usichoke apingaye apinge ila kweli inenwe yote
Bali utamkumbuka bwana Mungu wako maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri
Ili lifanye imara agano lake alilowapa baba zako kama hivi leo
Unayo mengi ya kukumbuka lakini si ya bwana,aanza leo kumkumbika bwana mungu wako sasa,ulimwacha wapi huyu Mungu na kushiriki giza.
Rudi leo na uanze sasa kumtumikia bwana, nguvu zake ziko zakungoja wewe umkumbuke,uwezo wake wakungojea wee umkumbuke
Tapewa nguvu za kupata yale unayotafuta kwa akili zako
Tapewa nguvu za kutosheka na kile ulichonacho mwenzangu
Tapewa nguvu za kutokuwa na tamaa ya vitu vingi mwenzangu
Tapewa nguvu za amani ndugu kuridhika na hali yoyote ile
(Wana wa manabii wakaenda kukata miti,wakamchukua nabii Elisha pamoja naye,katika kukata boriti mmoja wao chuma cha shoka lake kikaanguka majini)
Bwana wetu ni mkuu na mwingi ii wa nguvu, akili zake hazina mpaka,akili zake hazina mpaka
(Naye nabii kauliza kilikoangukia akamuonyesha nabii Elisha mahali pale nabii kakata kijiti katupa pale,chuma cha shoka lake kikaelea majini)
(wanasayansi wanajua chuma hakiwezi elea juu ya maji-akili zao zina mpaka)
(madakitari wanajua saratani inahitaji upasuaji-akili zao zina mpaka)
(Watu wajua utasa hauna dawa ila kuvunjika a kwa ndoa - akili zao zina mpaka)
(masikini wanasema umasikini ni kazazi cha aina yake-akili zao zina mpaka)
Alimwokoa Danieli na simba ni mwokozi
Alimwokoa Meshaki na moto ni mwokozi
Alifufua fufua Lazaro – anaweza
Hata shida iwe ngumu – anaweza
Hata uwe na magonjwa – ni mponya
Hata kama huna kazi – ni mpaji
Na tushangilie sote - vigelegele
(akili zake hazina mpaka)
Tazama,halleluya , tazama,tazama aa upate ishi
Mtazame aliyeangikwa juu hivi sasa aa upate ishi
-Mtazame huyo aliyeangikwa juu,hivi sasa upate ishi
Mwenye dhambi dhaifu mtazame tuu,wala usifanye tashwishi
-kama mwana kondoo hakuondoa dhambi na makosa yako maovu
Kama deni zetu zote hakulipa mbona imemwagika damu
-Si kutubu na sala ikomboayo ila damu ndiyi salama
na aliyeiwwaga aweza sasa dhambi zako kukufutia
-Usiwe na shaka Mungu amesema hakuna alilolisaza
Hapo alipokuja alitimiza kazi zote alizoanza
-Basi twae uzima kwa kufurahi upokee kwa bwana sasa
Ujijue hakika kwake kuishi Yesu aishie kabisa.
Watakatifu waioko duniani ndio walio bora hao ndio niliopendezwa nao asema bwana wetu.
-si waimbaji waliopo duniani eti ndio bora wamejiinua na kujigamba wameyaacha mapenzi yangu.
- si waongofu waliopo duniani eti ndio bora hao wamejawa na ukaidi wameyaacha mapenzi yangu
- si wenye dini waliopo duniani eti ndio bora wanatenda anasa za dunia wameyaacha mapenzi yangu
- si wahubiri waliopo duniani eti ndio bora wamewapoteza kondoo wangu wameyaacha mapenzi yangu
(watakuwa mbele ya kiti sha enzi wwakumtumikia Mungu wao hawataona njaa wala kiu jua wala ari)
(Mungu atayafuta machozi yote katika hayo macho yao wataimba wataimba wataimba aleluya.
Wataimba x3
(Watu wote mtiini Mungu sote twendeni tukaa..) Tukaimbe x3
Na ishara hizi zitafatana na hao waaminio
(kwa jina langu,jina langu watatoa pepo)
(watanena kwa lugha mpya,kwa lugha mpya)
(watashika nyoka,watashika nyoka)
( wakila kitu cha kutisha hakitawadhuru)
(wataweka mikono yao juu ya wagonjwa na watapata afya)
(Mimi nimepewa kuamini kutoa, ishara ya Baraka yafuatana nami)
(Mimi nimepewa kuamini kutubu, msamaha wa dhambi wafuatana name)
(Mimi nimepewa kwenda kitakatifu,ishara ya wokovu yafuatana nami)
Amini neno la Mungu ishara utaziona
(Ukitolea Mungu – utapata Baraka)
(Ukiungama dhambi – utasamehewa)
(Ukitakasa roho – ishara utaziona)
Wala msinung’unike, wala msinung’unike mkaharibiwa naye mharabu enyi ndugu
Roho ya kunung’unika haiwezi fanya kitu,tena anung’unikaye azidi kuharibika
Unaowanung’unika wanazidi kwenda mbele, nawe unung’unikaye wazidi kuharibika
Amani taharibika,Baraka taharibika,uzima taharibika,mwishowe ni jehanamu
Hata ukaona nini, hata usikie nini,wewe furahia lile, Mungu alikufanyia
Ukiwa na hali hii,utaenda mbele sana,utaishi na amani utaishi na Baraka
Moyo,moyo uliochangamka ni dawa nzuri dawa nzura sana
bali roho iliyopondeka huikausha kausha mifupa
Moyo changamka kuzitubu dhambi ndiyo dawa nzuri ya uzima wako
Moyo changamka kutolea Mungu ndiyo dawa nzuri ya kubarikiwa
Moyo changamka kuomba kwa Mungu ndiyo dawa nzuri ya majibu yako
Moyo changamka kwa utakatifu dawa nzuri ya kumwona Mungu.
Ewe moyo wangu, uuchangamke ndiyo dawa nzuri ya mambo yote
Ewe roho yangu na usipondeke utaikausha kausha mifupa
Moyo changamkia kutubu dawa nzuri ya uzima wako
Moyo changamkia kutoa dawa nzuri ya kubarikiwa
Moyo changamkia kuomba dawa nzuri ya majibu yako
Changamka kwenye utakaso dawa nzuri ya kumwona Mungu
Hapo mwanzo Mungu aliziumba ziumba mbingu na nchi,nayo nchi ilikuwa ukiwa tena utupu,tena utupu
Na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji.
Mungu akasema iwe nuru,nuru ikawa nuru,hata ilipofika siku ya sita kaumba ntu kwa mfano wake.
Kwa mfano wa Mungu limuumba mwanamume na mwanamke.
Mungu kaona kila alichofanya tazama ni chema sana,kwa mfano wa Mungu tumeumbwa inatupasa tujue hilo.
Ni kwanini basi tunateseka na magonjwa umasikini
Mwanangu shika maagizo ya baba yako,wala usiiache sheria ya mama yako.
Yafunge hayo katika moyo wako daima,jivike hayo shingoni mwako.
Uendako yatakuongoza,ulalapo yatakulinda,uamkapo yatazungumza nawe.
(Maana maagizo hayo ni taa,na sheria hiyo ni nuru,na maonyo ya kuadilisha mtu ni njia,njia ya uzima).x2
(Ndugu zangu mtu akigafilika katika kosa lolote,ninyi mlio kwa roho mregezeni upya,mtu kama huyo kwa roho ya upole,(ukiangalia nafsi yako isije,ukajaribiwa wewe mwenyewe)x2, tuzitubie dhambi zetu mbele zake Mungu kama Daudi anayesema,nalikujulisha dhambi yangu wala sikuficha upotofu wangu,nalisema nitayakiri makosa yangu kwa bwana,nawe utanisamehe upotovu wa dhambi zangu Basi ndugu zangu nawasihi kwa huruma zake Mungu,itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai,takatifu ya kumpendeza Mungu ndiyo ibada yenu yenye maana)
Ukaidi jamani, ukaidi roho mbaya
Wakristo wengi wanaenda jehanamu,(kwa ukaidi, kwa ukaidi)
Wamlilia Mungu waungama dhambi na baadaye warudia dhambi zao
(Nguvu hii ya ukaidi) yatoka wapi ndugu jiulize (ni katika kuikaidi) hiyo amri ya wazazi wako.
Maana kwa wazazi ndiko kwenye msingi wa maisha.
Ukaidi jamani,ukaidi roho mbaya
(Ukaidi, ni roho mbaya, nguvu hii yatoka wapi,je sikatika kuikaidi amri ya wazazi wako,tafakari ni wapi wazazi walikuagiza kisha ukakaidi,tubu kwa Mungu wako,ili nguvu hii ya ukaidi ikapate kukuacha kabisa)
(Je wajua kizuizi cha mema yako), ee baba - ee mama
,ee ndugu - ee dada
(Sikiliza upate kufahamu) (wewe) x2
Dhambi ndiyo chanzo cha mabaya pale edeni nayo ilipata nafasi kwake Adamu alipokosa kutii maagizo ya Mungu.
(kizuizi cha mema yako ni dhambi yako uliyoitenda mwenyewe ewe baba yangu)
Ewe mama yangu)
Ewe ndugu yangu)
Ewe dada yangu)
(tazama sasa Mungu anakuagiza kutii wazazi na kuwaheshimu,kwani ni amri iliyo ya ahadi,upate heri ukae siku nyingi)
(uachapo kutii na kuheshimu) wazazi
(uachapo kutii na kuheshimu) muhubiri
(uachapo kutii na kuheshimu) mwalimu
(uachapo kutii na kuheshimu) mamlaka
(tapata nafasi kutenda dhambi) (wewe)
Kutotii kukosa heshima huleta dhambi, hapo ndipo huja kizuizi cha mema yako,kukosa heri kutokaa siku nyingi kwa mema.
(tafakari uliishije na wazazi wako Yesu aita kwa upole wewe umwendee)
(Akusihi uziungame hizo dhambi zako nawe upate kuombewa hivyo utapona, wawili wenu duniani wakipatana,watakapoomba lolote watatendewa)
Amina amina- Aa amina aa
Nimeokolea – Aa amina aa
Aleluya-aleluya
Baba ninakupa wewe maisha yangu yote
Uyalinde baba uyatawale baba,uyalinde baba uyatawale baba x2
Baba ninakupa wewe na kazi zangu zote
Baba ninakupa wewe na nyumba yangu yote
Baba ninakupenda asante sana bwa mwokozi wangu
(kwani mimi) mimi sitaona haya kusema wewe wangu na mimi wako.
(katika maisha yangu baba naomba) nisaidie,nisaide baba aa..
Utumishi wangu - Kuhubiri kwangu - Kazi zangu - Kuimba kwangu - Ushuhuda
Mashauri yangu
Mungu tuajalie,Mungu tuajalie
(Kuyatenda mapenzi yako), Mungu tuajalie
(Katika kazi zetu)- (Katika kuimba kwetu)- (Katika kuhubiri kwetu)- (Katika Utumishi wetu) - (Katika Maombi yetu)- (Katika Ushuhuda wetu)
(Aleluya,Aleluya),- Aleluya Aleluya
(Jina la Yesu linaponya magonjwa)
(Jina la Yesu lina laleta uzima)
(Jina la Yesu lina laleta wokovu)
(Watu wote wajue) watu wote wajue x2 (Yesu nnani) Yesu nnani
Mwokozi wa ulimwengu,mponyaji wa ajabu, Rafiki na mfariji – watu watu wote wajue
(Na wazee wajue) na wazee wajue - yesu nani
(Na vijana wajue) na vijana wajue - yesu nani
(Tangazeni kwa wote) tangazeni kwa wote – yesu nani
(hubirini kwa wote) hubirini kwa wote – yesu nani
(Bwana nimetambua unanipenda) bwana nimetambua unanipenda
(Jehova nimetambua unanipenda)
(Shama nimetambua unanipenda)
(Jire nimetambua unanipenda)
(Hakuna Mungu kama wewe) hakuna Mungu kama wewe
Hakuna Mungu kama wewe, hakuna na hatakuweko.
Nilitembea kote-kote,nilizunguka kote-kote,nilitafuta kote-kote
Hakuna na hatakuweko
Wote anipao baba sitawatupa nje kamwe x2
Yeyote ajaye kwangu sitamtupa nje x2
(baba amenipa wewe mimi sitamtupa nje) baba amenipa wewe sitamtupa nje
Ukiwa ndani yake Mungu wa mama mwanzilishi
Ukiwa nazo dhambi mimi Yesu nitazifuta
Ukiwa una magonjwa mimi Yesu nitakuponya
Ukiwa umasikini mimi Yesu ni wa baraka
Mungu wa mwanzilishi ni Mungu wa kazi x2
(Ukiwa unazo shida muite Mungu wa Mwanzilishi)
(Ukiwa una magonjwa muite Mungu wa Mwanzilishi)
(Ukiwa una mashaka muite Mungu wa Mwanzilishi)
(Ukiwa umasikini muite Mungu wa Mwanzilishi)
Shangwe, shangwe,Shangwe aleluya
(Sifu shangwe) aleluya
(Cheza shangwe) aleluya
(Imba shangwe) aleluya
(Baba wa upendo ameniokoa) Nitamtukuza kwa upendo wake
(Ameniokoa kutoka dhambini) nitamtukuza kwa upend wake
(Amenisamehe sasa niko huru) nitamtukuza kwa upendo wake
(Nitamtukuza kwa fadhili zake)nitamtukuza kwa upendo wake
(Nilikua gizani kaniangazia) nitamtukuza kwa upendo wake
(Nilipougua akanituliza) nitamtukuza kwa upendo wake
(Nilihuzunishwa akanifariji) nitamtukuza kwa upendo wake
(Nitamuinua na kumtangaza)
(Kaniinulia mtumishi wake)-(Ameniongoza kwa njia ya kweli)-(Kama si upendo wake ningekuwa wapi)
(Nitamuabudu nani kama yeye)-(Nitalihimidi jina lake kuu)
(Baba wa upendo) wa upendo,wa upendo, (ni wewe baba) (hakuna mwingine)
(Nilikuwa gizani kaniangazia,nilikuwa dhambini ukaniokoa tena haikutosha ukanisamehe,nilipougua ukanituliza,nilihuzunishwa ukanifariji tena kaniinulua mtumishi wako,aniongoze kwa njia ya kweli,kama si wee baba mimi ningekuwa wapi)
(Baba ninakupenda ulivyonipenda,baba ninakuimbia ulivyonipenda,baba ninikutukuza ulivyonipenda)
(Baba wa upendo,wa upendo) wa upendo,wa upendo
Mungu wetu huyu wa mwanzilishi ni mzizi mororo katika nchi kavu, hugeuza mwamba ukawa chemichemi ni Mungu wa miujiza Mungu wa mwanzilishi.
Mungu wetu huyu ni Mungu wa miujiza ni Mungu wa matendo ni Mungu wa umoja, amesambaa kote Afrika mashariki Kenya na Uganda hata Tanzania.
Kuanzia Giriama Duruma na Taita,Ukambani na Kikuyu ameenea kote chi yote ya Kenya na sasa mpaka Lodwar,Mungu wa mwanzilishi katika nchi kavu.
Kuanzia koo la mti injili yahubiriwa hata barabarani injili ikaenea na sasa yahubiriwa ndani ya safina,ni Mungu yupi huyu wewe sema mwenyewe.
Alimponya Sara akapata Isaka akamponya Hana akapata Samweli atakuponya wewe usiye na mtoto,Mungu wa mwanzilishi ni Mungu wa maajabu.
Ni Mungu ainuaye ni Mungu afufuaye ni Mungu wa amani ni Mungu asiyeshindwa amefufua wengi na kuinua wengi,kutoka mavumbini ni Mungu wa miujiza.
Ni Mungu abarikiye ni Mungu aponyaye ni Mungu wa msamaha,ni Mungu wa majeshi,lete shida zako kwa Mungu wa mwanzilishi,Mungu wa mwanzilishi ni Mungu wa watu wote.
Ungama dhambi zako Mungu wetu atakuponya mtolee Mungu wetu naye atakubariki,muite Mungu huyu wakati wa matatizo,naye atakuponya ni Mungu wa kuponya.
(Itakuwa utakaposikia sauti ya bwana Mungu wako kwa bidii kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo)
(ndipo bwana Mungu wako atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani, na Baraka hizi zote zitakujia usikiapo)
Utabarikiwa kote mjini,utabarikiwa na mashambani
Utabarikiwa uzao wa tumbo lako,utabarikiwa uzao wa nchi yako
Utabarikiwa kote uingiapo,utabarikiwa na utokako
(Bwana atakufanya kuwa kichwa wala si mkia,nawe utakuwa juu tu wala huwi chini)
Mtafuteni bwana madamu anapatikana muiteni maadamu yukaribu
Mtu m’baya aache njia yake na mtu asiye haki aache mawazo yake
Na amrudie bwana naye ataamrehemu
Na arejee kwa Mungu wetu naye atasamehewa
Acha njia yako acha mawazo yako, urudi kwa bwana wako upate msamahaX2
(Acha njia yako acha mawazo yako urudi kwa bwana wako upate msamaha)
(Acha njia yako acha fitina zako acha na hiyo chuki upate funguliwa)
(Acha njia yako acha kiburi chako acha hiyo dharau imekufanya husikiwi na Mungu)
(Acha njia yako acha ufisadi wako acha na huo wizi upate barikiwa)
(Acha njia yako acha hasira yako acha huo uchungu upate funguliwa)
(Mtafuteni bwana maadamu apatikana muiteni yeye maadamu yukaribu)
(Maisha yangu yote nimpe nani ii )-Maisha yangu yote nampa bwana ayatawale
(Na mali yangu yote nimpe nani ii )-Na mali yangu yote nampa bwana ayatawale
(Na kazi zangu zote nimpe nani ii )-Na kazi zangu zote nampa bwana anyatawale
Maisha yangu yote – nampa bwana ayatawale
Na mali yangu yote – nampa bwana ayatawale
Na kazi zangu zote – nampa bwana ayatawale
(Ee baba Mungu wa Mwanzilishi nakusihi unitawale bwana maisha yangu,
Mimi peke yangu bwana siwezi kitu chochote,ninakusihi ewe Mungu uyatawale maisha yangu,tawala bwana. Asante Yesu)
(Furaha yangu yote nimpe nani ii) furaha yangu yote nampa bwana anitawale
(Elimu yangu yote nimpe nani ii) elimu yangu yote nampa bwana aitawale
(Maisha yangu yote nimpe nani mimi) maisha yangu yote nampa baba ayatawale
Furaha yangu yote-nampa bwana aitawale,Elimu yangu yote- nampa bwana aitawale, Maisha yangu yote – nampa bwana ayatawale.
Maana Mungu si dhalimu hata aisahau kazi yenu na pendo lile mlilolidhihirisha kwa jina lake, kwa kuwa mmewahudumia watakatifu, na hata hivi sasa mngali mkiwahudumiax2
(Nasi twataka sana kila mmoja wenu aidhihirishe bidii ileile kwa utimilifu wa matumaini hata mwisho)
Kwa utimilifu wa matumaini hata mwisho
kila mmoja wenu aidhihirishe bidii ileile
Muwajengee muwalishe muwavike na pia mavazi
Waeneze injili kwa garama zetu katika matoleo
Mahitaji yao yasiwasumbue wenyewe bali sisi
Wanakesha kwa ajili yetu yastahili tuwahudumie
Tuyatende yote kwa utimilifu wa matumaini hata mwisho
kazi yako si bure uwe na matumaini hata mwisho
Mungu si dalimu hata aisahau kazi yako
Baba mama ndugu nawe dada yangu
Tenda kwa utimilifu mwisho utapokea thawabu
Acha kuzimia rohojipe moyo inuka Baraka zakungoja ukazinyakue
Uwe baraka za kungoja-ukazinyakue
Peke yangu la,peke yangu la
Ndivyo alivyoniambia, haniachi pweke
Haniachi, haniachi pweke
Ndivyo alivyonambia haniachi pweke
(Haniachi pweke) Haniachi pweke
(Mungu wa mwanzilishi ooh) Haniachi pweke
Ombeni ombeni nanyi mtapewa
Bisheni bisheni nanyi mtafunguliwa
Ombemi ombeni nanyi mtapewa
Tafuteni tafuteni nanyi mtaona
Msifadhaike mioyoni mwenu baba wa mbinguni ajua haja zenu, nanyi mkiomba kwa mapenzi yake yote mnayotaka atawatimizia.
Muiteni yeye maana yu karibu, muombeni yeye maana asikia
- (Yesu alijitoa afe msalabani jili ya dhambi zetu ili tupate wokovu)
(Yesu alijitoa akapigwa sana jili ya dhambi zetu ili tupate kupona)
(Yesu alijitoa damu ikamwagika jili ya dhambi zetu ili tupate takaswa)
(Sasa tufurahi kwa kuwa tumeokolewa) Tufurahi kwa kuwa tumeokolewa
(kifo chake Yesu kimetupa wokovu)
(Mapigo yake Yesu yametupa kupona)
(Damu yake Yesu imetutakasa)
(Sasa tufurahi kwa kuwa tumeokolewa)
(Sasa tufurahi kwa kuwa tumepona)
(Sasa tufurahi kwa kuwa tumetakaswa)
(Wema wako kwetu Mungu tumeuona) wema wako kwetu Mungu tumeuona
(Furaha tunayoiona ni kwa ajili ya wema wako)
(Amani tunayoiona ni kwa ajili ya wema wako)
(Baraka tunazoziona ni kwa ajili ya wema wako)
Wema wako ooh wema wako -(Una furaha, una uzima, una baraka, una amani)
Yesu, Yesu, Yesu amezaliwa
(Amezaliwa duniani ili tupate wokovu)
(Amezaliwa duniani ili tuwe na uzima)
(Amezaliwa duniani ili tupate baraka)
(Amezaliwa duniani ili tuwe na furaha)
Tuimbe Yesu
(Amezaliwa duniani ili tuwe na amani)
(Amezaliwa duniani yeye ni mwana wa Mungu)
(Tusifu Yesu,Tuimbe Yesu)
(Shangilieni,shangilieni,shangilieni Yesu amezaliwa)
(Mwimbieni bwana wimbo mpya msifuni kwa wema wake,sifa zake zivume katika kusanyiko,kwa kuwa leo kazaliwa mwana,mkombozi wa ulimwengu, mpigieni Mungu kelele za shangwe)
Furahini katika bwana siku zote tena nasema furahini
Upole wenu ujulikane na watu wote bwana yu karibu
Na amani ya Mungu ipitayo akili zote itawahifadhi mioyo na nia zenu katika kristo Yesu
Msijisumbue kwa neno lolote bali katika kila neno kwa kusali na kuomba pamoja na kushukuru haja zenu nazijulikane na Mungu.
(Mjue sana) (mjue sana Mungu) ili uwe na amani, ndivyo mema yatakavyo kujia.
(Tazama Ayubu alivyopata mateso) badala yake hakujua tabu zake sana
(Hivyo yeye alimjua Mungu wake sana) kwa kumjua amani kaingia ndani yake
(Hivyo mema yakamjia mteule Ayubu) mateso yote yakamuishia Ayubu
( Kupata tabu nyingi katika kanisa,humfanya mkristo kumjua Mungu kwake kukamtoka,lakini sivyo,wakati mkristo anapoingia katika dhiki,huwa ndio wakati way eye kumjua Mungu zaidi,Huwa sio wakati wa kuvunjika moyo na kukata tama,bali ndio wakati mwafaka wa kumuiga mtumishi wa Mungu Ayubu,jinsi alivyovumilia mateso mengi na kuingiakatika mema,Nami nina hakika mema yatakujilia pasipo kizuizi)
Wamjuao Mungu wao watakuwa hodari na kutenda makuu
(Watamtolea,watamtumikia,watatubu dhambi,wata takasika)
Wamjuao Mungu wao watakuwa hodari na kutenda makuu
(Katika biashara yako mtolee Mungu atakubariki,katika mshahara wako mtolee Mungu atakubariki,katika mapato yako muheshimu Mungu atakuinua,katika mazao yako mkumbuke Mungu atakuinua)
(Tanzania, Kenya, Uganda mtoleeni Mungu wetu atawabariki,katika mishahara yenu mtoleeni Mungu atawabariki,akina mama mtakuwa hodari,akina baba mtakuwa hodari-mnapomtolea Mungu mtakuwa hodari-mnapomtumikia Mungu mtakuwa hodari)
Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote,Mungu hufanya kazi (pamoja na wale wampendao) katika kuwapatia mema,yani wale walioitwa kwa kusudi lake.
Tumekubali tunakupenda tufanye kazi kama ulivyosema
(Ee bwana Yesu) tumekubali (sote twasema) tunakupenda (hivyo twaomba) tufanye kazi (pamoja nasi) kama ulivyosema.
Usiloweza , usiloweza (maana hakuna gumu,maana hakuna zito,Jehova Shama, Jehova Jire,Jehova Nisi.
( Ama kwa kweli hakuna zito mbele za Mungu wa Mwanzilishi,Mungu aliyeziumba mbingu na nchi,aliyemtoa mwanawe pekee ili atuokoe,Mungu asiyeshindwa,bwana mwenye nguvu,aliye mwanzo na mwisho- shangwe na vigelegele)
Wewe waweza, wewe waweza
(Atakubariki,atakusamehe dhambi,atakupatanisha na watu wote,wewe waweza bwana)
-Sote tushangilie kwa kuwa ,Yesu bwana kazaliwa
Baraka tumepata kwa kuwa,Yesu mkombozi kazaliwa
-Kama bwana usingelizaliwa tungeoko-olewaje,
Pendo lako kwetu wanadamu ni kuu halikadiriki
Basi leo tunakuhitaji uzaliwe mioyoni
Utuokoe katika dhambi tulizozitenda duniani
(Ooh Yesu amezaliwa) Yesu amezaliwa
(wa baraka amezaliwa) - (wa ushindi amezaliwa) - (tuimbe Yesu amezaliwa)
(tushangilie amezaliwa)
(Sikiliza ndugu mpendwa,Yesu amezaliwa mkombozi wa ulimwengu,haijalishi una shida gani,kubali Yesu azaliwe moyoni mwako,akusamehe na dhambi,akuponye na magonjwa, nawe utabarikiwa-shangwe na vigelegele kwa Yesu)
(Ooh sasa azaliwe) azaliwe mioyoni mwetu
(sote tumpokee) - (sote tumkubali) - (atusamehe na dhambi) -(atuponye na magonjwa)
Petro kwa niaba ya wanafunzi wote,akamuuliza Yesu uu
(Tutapata nini) tulioacha vyote kukufata wewe ee
(Mara mia mtapokea Yesu kawajibu)
Shangilia, furahia, mtumikie Mungu kwa mali yako
Kilichonona mtolee Mungu wako naye Mungu atakubariki.
(Ooh ndugu zangu wapendwa nawaomba mnisikie, ee maneno haya ninayowaambia ni kweli, hakuna mafanikio kazini nyumbani hata shuleni mbona twamuibia Mungu kama asemavyo mwenyewe,nasi twasema twakuibia kwa namna ganii eeh. Tazama nyumba ya bwana ilivyo hali ya ukiwa,sisi twashughulikia nyumba zetu na kuacha nyumba ya bwana, twajaribu shughuli zote lakini hatuoni mafanikio ooh,sadaka tumeacha na zaka hatutoi twashughulikia nyumba zetu ooh, hasara tupu)
(Furaha ni kwake amwaminiye,baraka ni zake za tele lazima,maana Mungu ndiye abarikiaye mtolee aweza kukupa kupita yeyote Yule)
(Kwani aliyenacho huongezewa, furahia ndugu yangu eeh kutumika)
Hivyo basi imetupasa kumtumikia Mungu huyu wetu wa mwanzilishi ndani ya mchungaji katika hali na mali tumtolee Mungu, usiwe na shaka nalo kwani ndilo agizo lake, kila zao lako la kwanza umtolee Mungu,ukichagua kilichonona kwake Mungu wetu huyu.
Mungu ana njia nyingi, Mungu ana njia nyingi
Mungu ana njia nyingi, Mungu ana njia nyingi
Mungu ambaye alisema zamani na baba zetu, katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, Mwisho wa siku hizi amesema nasi katika mwana alivyosema na Petro kwa kwa njia nyingine kapata samaki wengi.
(Katika ugumu wote wa maisha yako,Mungu ana njia nyingi za kukutokea)
Anakuhitaji tu usiwe mkaidi, anakuhitaji tu usiwe mjeuri
Anakuhitaji uondoe kutojali, anakuhitaji uondoe kutotii
(Alifanya njia bahari ya Shamu,waisraeli wakavuka)
(Alifanya njia kumuokoa Yona baharini kupitia samaki)
(Atafanya njia kwa matatizo yako, yageuzwe ili yawe baraka)
(Atafanya njia usiye na mtoto, ili uwe mwenye watoto wengi)
(Atafanya njia uliyefutwa kazi, urudishwe kazini mwako)
(Atafanya njia ndoa imevunjika, ipatanishwe mrudiane tena)
Vita ulishinda Bwana Yesu ulishinda, Mauti ulishinda Bwana Yesu ulishindax2
--(Wakuu wa makuhani walimkamata bwana wakampeleka kwa pilato ahukumiwe)
(Ooh bwana wangu walimkamata)
(Na hakuwa na makosa bali walimtungia,walimtesa bwana mijeledi walimpiga)
(Ooh bwana wangu walimpiga)
(hawakumhurumia hawakumjali mkuki walimchoma yote ili tuokolewe)
(Ooh ubavuni walimchoma)
--(Bwana alijitoa kuugaramikia wokovu wetu sote tuwe huru)
(Ooh alijitoa tuwe huru)
(Dhambi zetu ndizo zilimsulubisha, tutendapo dhambi tunamsulubisha tena)
(Ooh tunamsulubisha tena)
(Na tuziungame dhambi tulizozitenda, na tuzitubie tusizitende tena)
(Ooh tusitende dhambi tena)
Alfajiri na mapema nchi ilitetemeka walinzi waliogopa na kujawa na wasiwasix2
Malaika wake bwana melivingirisha jiwe bwana Yesu kafufuka kaburini hayumo tenax2
Maria Magidalena likwenda kaburini alikuta bwana wetu Yesu amefufukax2
Kufufuka kwake bwana kumeleta ushindi kwetu wanadamu haleluya tushangiliex2
(Ooh nishangwe nishangwe bwana amefufuka)-(Ooh nishangwe nishangwe ushindi tumepata)- (Kifo kaburi vyote vimeshindwa)
(Ooh ni shangwe ni shangwe) Ni shangwe ni shangwe
(Bwana amefufuka, Ameuchukua udhaifu wetu, Ameyachukua magonjwa)
Na wale wanafunzi kila mtu kwa kadiri ya alivyofanikiwa, wakaazimu kupeleka msaada kwa ndugu zao waliokaa uyahudi.x4
(Wee azimu kutoa) hata kama una madeni
(Wee azimu kutoa) hata kama una upungufu
(Wee azimu kutoa) hata kama unayoshida
Wewe azimu, wewe azimu, azimu tu
(Unapoazimu mwingine naye) ataazimu kukubariki
(Toa sadaka zaka yako kwa kuazimu) Toa sadaka zaka yako hivi vyote kwa kuazimu
(Toka kwa hiyo mipango yako yote ya kiakili) Toka kwa hiyo mipango yako yote ya kiakili
(Kuvaa kwako na kula kwako achia Mungu) Kuvaa na kula kwako ndugu wewe achia –Mungu
(Unapoazimu naye mwengine ataazimu) Unapoazimu mwengine naye ataazimu kukubariki
Bwana asema asema hivi simameni katika njia kuu mkaulize habari ya mapito ya zamani iwapi njia iliyo njema mkaende katika njia hiyo nanyi mtajipatia raha katika aa nafsi zenu.
(Je chuki imekulemea uliza kwa mtumishi wa Mungu)
Iwapi njia iliyo njemax3 upate raha nafsini mwako
Zinaa imekulemea uliza kwa mtumishi wa Mungu
Uongo umekulemea uliza kwa mtumishi wa Mungu
Ulevi umekulemea uliza kwa mtumishi wa Mungu
Wizi umekulemea uliza kwa mtumishi wa Mungu
(Na hapa palikuwa na mtu ambaye amekuwa hawezi)x2
Muda wa miaka thelathini na minanex2
(Yesu alipomuona huyu amelala)x2
Naye akijua ya kuwa amekuwa hali hiyo siku nyingix2
Alimuambia wataka kuwa mzimax2
(Baada ya muda mrefu Yesu anakupitia leo)x2
(Anakuuliza je wataka, je wataka) kuwa mzima-pata baraka-pata amani
(Simama) Simama jitwike godoro lako, jitwike godoro lako na uende
(Bwana amekutakasa,bwana amekusamehe, bwana amekuponya, simama)
(Yesu anauliza je wataka kuwa mzima, kuna kutaka na kutakiwa ni wewe mwenyewe utake ndipo Yesu atakuwa nawe utajitwika godoro lako utaenda nalo)
(Haja zako ndugi yangu wamwambia nani pia na matatizo yako wamwambia nani, mwambie Yesu maana ni muweza anajibu haja za moyo wako)x2
Mahitaji ya moyo wako mwambie Yesu maana yeye ni muweza wa mambo yotex3
(Katika kazi zako mkiri Mungu wa mwanzilishi naye atayanyosha mapito yako)
(Katika nyumba yako mkiri Mungu wa mwanzilishi naye atayanyosha mapito yako)
(Katika kuimba kwako mkiri mungu wa mwanzilishi naye atayanyosha mapito yako)
(Katika shughuli zako zote mkiri Mungu wa mwazilishi naye atayanyosha mapito yako)
Katika njia zako mkiri yeye naye atayanyosha mapito yako
(Kenya , Uganda na Tanzania chezea Mungu wa mwanzilishi ukijua yeye peke yake ndiye ana uzima)
1. Nawe utajifurahisha kwa Bwana naye atakupa haja za moyo wako x2
{(Utajifurahisha kwa Bwana)x3 naye atakupa haja za moyo wako}x2
2. Nawe utatolea Mungu dhabihu naye ataibariki hazina yako
{(Utatolea Mungu dhabihu)x3 naye ataibariki hazina yako}x2
3. Nawe utaungama dhambi zako naye atakuponya na magonjwa yako
{(Utaungama dhambi zako)x3 naye atakuponya na magonjwa yako}x2
(Instruments Chorus)x2
{(Utajifurahisha kwa Bwana)x3 naye atakupa haja za moyo wako}x2
(Naye Daudi akatoka kuwalaki na kuwaambia) kama mmenijia kwa amani ili kunisaidia, moyo wangu utaambatana nanyi, moyo wangu utaambatana nanyi.
(Lakini kama mmekuja kunisaliti kwa adui zangu kwa kuwa hamna udhalimu mikononi mwangu) Mungu wa baba zetu na alitazame neno hili na kulikemea, na kulikemea.
(Ndipo roho ikamjilia Abishai naye akasema sisi tuwako ee Daudi na wa upande wako)
Amani naam iwe kwako na kwao wakusaidiao akusaidiaye ndiye Mungu wako ee mwana wa Yesse.
(Ndugu dada mpendwa umedai mema kutoka kwa Mungu siku nyingi lakini hujayapata, unajiuliza maswali mengi, je nimelaaniwa au nimekosa nini kwa Mungu, Mpendwa hujakosa lolote ila, uko upande wa nani, Je moyo wa mtu wa Mungu umeambatana nawe)
(Moyo wa mtu wa Mungu uambatane nawe)
(Ndipo utatulia maishani mwako,ndipo utaona furaha maishani mwako, ndipo utaona amani maishani mwako, Tafuta ewe baba uambatane naw, Tafuta ewe mama uambatane nawe)
(Furaha, Amani na utulivu utaambatana nawe baada ya kuwa moyo wa mtumishi wa Mungu umeambatana nawe, Ni cheo kazini, ni karo ya watoto shuleni, Mungu atakujazia maana ule moyo umeambatana nawe)
(Nilitafuta wa kufanana naye Mungu wake mwanzilishi sikumuona)
(Ooh nasema nilitafuta aliye kama Mungu wa mwanzilishi wa kuponya sikumuona mimi)
(Ooh nasema nilitafuta aliye kama Yahweh wa mwanzilishi wa kuponya sikumuona mimi)
(Nasema nilitafuta aliye kama Mungu wa mwanzilishi wa baraka sikumuona mimi)
(Ndiyo nilitafuta wa kufanana na Mungu wa mwanzilishi kwa kazi anazozifanya lakini sikumuona wa kubariki na kuponya hakuna kama yeye, yeye halinganishwi hafananishwi yeye ni namba moja haleluya)
(Ooh Yeye halinganishwi-Mungu wetu halinganishwi-na chochote halinganishwi- anaokoa halinganishwi-anabariki halinganishwi)(hafananishwi)x5 (yeye ni namba moja)x5
(Yeye ni namba moja-Anainua ni namba moja-yeye ni namba moja)
(Mungu wa mwanzilishi ndiye Mungu wetu aliyekuwako yuko na atakuweko,Ndiye Yule jana na hata milele ndiye wa Israeli ambaye waafilisti walijaribu kumlinganisha na mungu wao wa dagoni, wakachukua sanduku la agano wakaliweka pamoja na kinyago chao cha dagoni, kumbe kulipokucha dagoni alianguka na kukatika vitanga vya mikono yake-Halinganishwi,hafananishwi-yeye ni namba moja)
(Wakaamka asubuhi na mapema, wakaenda nje katika jangwa la Tekoa, nao walipokuwa wakitoka)
(Yehoshafati akasimama akasema)
(Nisikieni enyi Yuda nanyi wenyeji wa Yerusalemu)
Mwaminini Mungu ndipo mtakapothibitika, waaminini manabii ndipo mtakapo fanikiwa
(Maisha yetu hayafanikiwi hatumwamini nabii)
Twamwamini Mungu lakini nabii tumemuacha, twasahau kwamba nabii alitumwa naye Mungux2
Amini nabii upate fanikiwa
(Amini wewe baba, Amini wewe mama,)
(Ukitaka baraka amini,ukitaka furaha amini, ukitaka uzima amini, ukitaka amani amini)
Tupate wapi mtu kama huyu, mwenye roho ya Mungu ndani yake
Tupate wapi mtu kama huyu mwenye roho ya Mungu ndani yake
Yusufu katafasiri ndoto ya mfalme Farao iliyowashinda waganga na wote wenye hekima
Farao akamuweka Yusufu awe mkuu katika nchi hii yote ile ya Misiri
Sasa tumempata mtu huyu mwenye roho ya Mungu ndani yake
Ooh sasa tumempata mtu huyu mwenye roho ya Mungu nasema ndani yake
Sasa twashuhudia ndoto zetu kutafasiriwa shida zilizowashinda waganga wote na wenye hekima
Mtumishi atuhubira na kutufundisha yote yaliyowashinda wenye uwezo na wenye hekima
Ooh sasa tumempata mtu huyu mwenye roho ya Mungu ndani yake
Mwenye roho ya Mungu ndani yake
Ooh sasa tumempata nabii wetu,- Natumpokee mwonaji wetu,- Sote tumtii nabii wetu, -Sote tumuheshimu nabii wetu,- Sasa tumwamini nabii wetu, Mwenye roho ya Mungu nasema ndani yake
Amen halleluya x3
Halleluya tumsifu bwana
Kila mwenye pumzi amsifu, amsifu bwana
Kwa uuu wake ulivyo wa ajabu
Vinanda vinubi matari na mazeze
Vyote visikike vililisifu jina lake
Mshukuruni bwana kwa kuwa ni mwema
Kwa maana fadhili zake ni za milele
Yesu amezaliwa kristo mwana wa Mungu
Ndiye mwokozi wetux2
Tushangilie tushangilie tushangilie ee tushangilie
Yesu ametujia iliatuokoe
kutokana na dhambi
sasa umkubali azaliwe moyoni
upate msamaha
Kusulubiwa kwa bwana yesu kulikuwa kutuokoa kutokana na dhambi
Damu yake iliyomwagika ilikua ya kutakasa dhambi zetu zote
Itia jina (mwenzangu) lake Yesu, Itia jina lenye thamani kuu
Jina la Yesu ndilo jina pekee, liwezalo kuokoa
Mijeledi waliompiga ilikua ya kutuponya magonjwa yetu yote
Na maji yaliyo tiririka yalikuwa ya kusafisha maovu yetu yote
kufa na kuzikwa kwake yesu kulikua kuzichukua funguo za mamlaka
siku ya tatu alifufuka kutuondoa kifungoni mwake mwovu shetani
Mchagueni mungu wa kweli mtakae muabudu
(mtasitasita kwa mawazo mawili hata lini)
Ndipo uwe na uhuru wa kuabudu kwa hiari
Nawe uwe na hakika unapoomba kwa Imani
Kama Eliya alipowakusanya watu mlimani
(wakasadiki kuwa Mungu wa Eliya ndiye Mungu)
Ndipo uwe uhuru wa kuabudu kwa hiari
Nawe uwe na hakika unapoomba kwa Imani
Nanyi ombeni kwa jina lake Mungu mliyechagua
(Mungu ajibuye kwa moto ndiye Mungu tasikia)
Ndipo uwe na uhuru wa kuabudu kwa hiari
Nawe uwe na hakika unapoomba kwa Imani
(Mtumishi wake Elisha akafadhaika,alipoona jeshi kubwa limewawazunguka
Akalia ole wetu bwana wangu oole wetu tufanyeje)
Akamjibu usiogope maana waliopamoja nasi ni wengix2
kuliko wale waliopamoja nasix2
(Elisha akaomba akasema ee bwana nakusihi mfumbue macho yake apate kuona bwana akamfumbua macho yule mtumishi naye akaona)
(Na tazama) (kile kilima kilikuwa kimejaa) farasi (na magari ya moto yaliyomzunguka) Elisha.
Sasa mhubiri anatuambia ubaya unaouona sasa ni dhaifux2
kuliko wema aloandaa Mungux2
(magonjwa ni jeshi dhaifu linalokutisha wewe lakini uzima wa mungu) umekuzunguka
(madeni ni jeshi dhaifu linalokutisha wewe lakini utajiri wa Mungu) umekuzunguka
(umaskini ni jeshi dhaifu linalokutisha wewe lakini utajiri wa Mungu) umekuzunguka
Tazama mimi naona watu wane wamefunguliwa wanatembea katikati ya moto hali hawana dharax2
Shedraki meshaki Abednego walitupwa kwenye tanuru ya moto mtu wa nne kawatokea pale naye ni bwana yesu
(Na ninyi mnapopatwa na majaribu mbali mbali)
(Madeni) yote ni moto, (kufilisika) yote ni moto (kutatokea) mtu wanne mwokozi yesu akuokoe na tanuru.
(Magonjwa) yote ni moto (utasa) yote ni moto (kutatokea) mtu wanne mwokozi Yesu akuokoe na tanuru
(Umasikini) yote ni moto (kukosa kazi) yote ni moto (kutatokea) mtu wanne mwokozi Yesu akuokoe na tanuru
Japo walikua katika hali ngumu walitulia wakimsifu Mungu
Akatokea mtu wan ne yesu kuokoa
Kutulia kumtumainia Mungu katika majaribu yako yote hufanya mtu wa nee Yesu kutokea
Nilihangaika sana duniani mimi sikupata raha maishani mwangu
Nilizunguka nikitafuta wa kuniokoa sikupata ila Mungu wa mwanzilishi x2
(Mimi nampenda sana) Nampenda Mungu wa mwanzilishi.
(Kanipa amani) Ametenda makuu moyoni mwangu
(Mimi nampenda sana) Nampenda Mungu wa mwanzilishi.
(Ameniokoa) Ametenda makuu moyoni mwangu.
(Ooh nampenda sana) Nampenda Mungu wa mwanzilishi.
(Wewe wampenda nani ) Nampenda Mungu wa mwanzilishi.
(Amefanya nini) Ametenda makuu moyoni mwangu
(Je wewe wampenda nani) Nampenda Mungu wa mwanzilishi.
(Amefanya nini)Ametenda makuu moyoni mwangu
(Na sote twampenda nani) Nampenda Mungu wa mwanzilishi.
(Amefanya nini) Ametenda makuu moyoni mwangu
Nampenda Mungu wa mwanzilishi ametenda makuu moyoni mwangu
Nampenda Mungu wa mwanzilishi(ameniokoa) ametenda makuu moyoni mwangu
Nampenda Mungu wa mwanzilishi(ameniokoa) ametenda makuu moyoni mwangu
Wewe wampena nani
Nampenda Mungu wa mwanzilishi(amefanya nini) ametenda makuu moyoni mwangux2
Sote twampenda nani
Nampenda Mungu wa mwanzilishi(amefanya nini) ametenda makuu moyoni mwangu
(Nilihangaika sana duniani mimi sikupata raha maishani mwangu
Nilizunguka nikitafuta wa kuniokoa sikupata ila Mungu wa mwanzilishi)
(Utajiri na mali nilitafuta mimi ila havikuweza kunipa uzima nilipompata Mungu wa mwanzilishi magonjwa yangu yote aliyaondoa)
(Jamani nampenda)
Nampenda Mungu wa mwanzilishi (kanipa uzima)ametenda makuu moyoni mwangu
Hata Baraka nilizonazo
Nampenda Mungu wa mwanzilishi (amenipa yeye)ametenda makuu moyoni mwangu
Hata furaha niliyonayo
Nampenda Mungu wa mwanzilishi (amenipa yeye)ametenda makuu moyoni mwangu
Hata Amani niliyonayo
Nampenda Mungu wa mwanzilishi (amenipa yeye)ametenda makuu moyoni mwangu
Jamani tumpende
Nampenda Mungu wa mwanzilishi (kwa upendo)ametenda makuu moyoni mwangu
Ooh tumpende
Nampenda Mungu wa mwanzilishi (ametenda mema)ametenda makuu moyoni mwangu
(Lazima tukushukuru lazima tukuinue lazima tukusifu lazima tukuabudu
Ni lazima nimfifu nimtukuze nimshukuru)
Na siku hiyo watasema wote
(huyu ndiye Mungu wetu tuliyemgoja kwa siku nyingi tumfurahie x4)
Huyu ndiye Mungu wetu tumshangilieni
Huyu ndiye Mungu wetu tumfurahieni
Huyu ndiye Mungu wetu tumshangilie
Jina lake (jina lake muumba wetu)
(Tumfurahie tumshangilie)
Kanisa sasa tumfurahieni
Mungu tuliemngoja tuko naye
Kanisa sasa tumshangilieni
Mungu aponyaye sasa tuko naye
Kulia magonjwa sasa hakuna tena
Mungu mponyaji mungu wa mwanzilishi
Utajiri Baraka zi kwake milele
Huinua wanyonge kutoka mavumbini
Tuimbe tusifu tufurahi kwake
Mungu wa mwanzilishi anaweza yote.
Nitie kama muhuri moyoni mwako
Kama muhuri juu ya mkono wako
Kwa maana upendo una nguvu kama mauti
Maji mengi hayawezi kuuzimisha upendo
Wala mito haiwezi kuuzimisha upendo x2
Apataye mke apata kitu chema,
mke mwema nani awezaye kumuona x2
Apendaye mkewe ajipenda mwenyewe
maana hakuna achukiaye mwili wake x2
Kumtii mume kama kutii Yesu
mume kichwa cha nyumba na kristo cha kanisa x2
Mengi tuliona tukatia moyoni
likua maji mengi ya mito yamepita x2
Nitie kama muhuri moyoni mwako
Kama muhuri juu ya mkono wako
Kwa maana upendo una nguvu kama mauti
(Maji mengi) maji mengi hayawezi kuuzimisha upendo
(Wala mito) wala mito haiwezi kuuzimisha upendo x2
(nitie, moyoni mwako)
(maji mengi, wala mito)
(maji mengi kwa hakika hayawezi x2) --- kuuzimisha upendo
(wenye fitina hawawezi x2)
(kukosa mali hakutaweza x2)
(njaa na kiu haviwezi x2)
(magonjwa hayataweza x2)
(maji mengi kwa hakika hayawezi x2) --- kuuzimisha upendo
(wenye fitina na chuki hawataweza x2)
(pia umasikini hautaweza x2)
(shida njaa na kiu haviwezi x2)
(udhaifu magonjwa hayawezi x2)
……kuuzimisha upendo
Mungu wa mwanzilishi ndiye Mungu wetu
Tukumuomba yeye hakika hutimiza x 2
(Ooh Mungu wa mwanzilishi ndiye Mungu wetu
Tukumuomba yeye hakika hutimiza)
(Ooh mungu wa mwanzilishi ni Mungu aponyaye
Tukimuomba yeye hakika hutimiza)
Ooh Mungu wa mwanzilishi ni Mungu abarikiye
Tukimuomba yeye hakika hutimiza
Aah Mungu wa mwanzilishi ni Mungu ainuaye
Tukimuomba yeye hakika hutimiza
Ooh Mungu wa mwanzilishi ndiye Mungu wetu
tukimuomba yeye hakika hutumiza.
Ooh Mungu wa mwanzilishi ndiye Mungu wetu
Tukumuomba yeye hakika hutimiza x 2
Kweli Mungu wa mwanzilishi ni Mungu wa msamaha
Tukimuomba yeye hakika hutimiza
Ooh Mungu wa mwanzilishi ni Mungu wa Amani
Tukimuomba yeye hakika hutimiza
Ooh Mungu wa mwanzilishi ni Mungu wa upendo
Tukimuomba yeye hakika hutimiza x2
Aah kweli kabisa Mungu wa mwanzilishi ni Mungu wa kazi
Mungu wa mwnzilishi ni Mungu anayejibu maombi
Ametuinua, ametuponya, ametubariki ndio maana tunamsifu na kumtukuza
Hakika twende wapi isipokuwa kwa huyu Mungu wa mwanzilishi
Hakika hutimiza ----
Eee hakika hutimiza x2
Ukimuomba Amani
Ukumuomba Baraka
Hakika hutimiza…x5
Ooh hakika hutimiza x3
Eee Ukimuomba Amani
Eee Ukumuomba Baraka
Hakika hutimiza…
Nikitafakari upendo wake Bwana Yesu
Najikuta nimefika upeo wa mawazo
Nikizichunguza na rehema zake nyingi
Hapo ndipo ninakoma bila jawabu
Nikupe nini (nikupe nini Bwana)
Nikupe nini
Nikupe nini Bwana kwa rehema zako x2
Ulimchagua mtumishi wako Elisha
Ukampa kanisa na pia maongozi
Yatakayofaa katika maisha yangu
Hayo yote sikulipa hata garama
Mwanzilishi kajitolea na nyumba yake
Aliteseka sana na hata kufedheheshwa
Lakini ukampa sana uvumilivu
Umenirehemu sikwa wema wangu
Shukurani zangu kwa Mungu wa mwanzilishi
Kwa kunifikisha siku hii ya leo
Ninakuombea mama yetu mwanzilishi
Uwe na afya njema na uzima tele
(nikupe nini Mungu wa mama mwanzilishi umetulinda Zaidi ya miaka hamsini na mitano
Hakika wema wako kwetu leo tunauona)
(Jamani mungu atupenda) Mungu hakutuacha yatima x2
Ramani ya uinjilisti (tunayo ooh tunayo) Kuhubiri uliwengu wote,
kujenga hayo mahekalu Tuyajenge katika umoja
katika utumishi wetu tuwatunze wahubiri wote
(uinjilisti)kuhubiri ulimwengu wote (mahekalu)tuyajenge katika umoja)
(kwa utumishi) tuwatunze wahubiri wote
(Ni kweli Mungu atupenda) Mungu hakutuacha yatima x2
Ramani ya maendeleo(tunayoo ooh tunayo) makanisa yawe nazo shule
Wahubiri wawe imara, tusikose kuwa na semina,
Namna ya kusifu Mungu kwa vinanda magita na ngoma
(Maendeleo)makanisa yawe nazo shule (kuwa imara)tusikose kuwa na semina
(Kusifu Mungu) kwa vinanda magita na ngoma
(hakika Mungu atupenda) Mungu hakutuacha yatima x2
Ramani ya usambazaji (tunayoo tulipewa tunayo) runinga redio majarida
Namna ya uhusiano afrika na dunia nzima
Kuongoza kazi ya Mungu huyo roho ndiye kiongozi
(usambazaji)runinga redio majarida (Uganda Tanzania) afrika na dunia nzima
(Kazi ya Mungu) huyo roho ndiye kiongozi
(usambazaji)runinga redio majarida (na dunia yote) afrika na dunia nzima
(Kazi ya Mungu) huyo roho ndiye kiongozi
Tuushangilie (kanisa) kanisa( la Mungu) la Mungu lilivyo imara
(Uu)Umoja wetu( wadumu )wadumu( milele)milele tena na milele
Tumsifu baba Mungu(kanisa) kanisa(ladumu) ladumu milele x4
Shetani naye (hapendi) hapendi (kanisa)kanisa la Mungu lidumu
(Tuu)tuweni maho (na hila)na hila za huyu baba wa uongo
Kazi ya Mungu (aliyo)aliyo (anzisha)anzisha mtumishi wake
(Tuu)tuidumishe (kwa kumu)kwa kumu(heshimu)heshimu kiongozi wetu.
Matendo makuu yake mwanzilishi kwa kweli ni ya ajabu
Uvumilivu na ulezi yoye aliyaweza kwa upendo
(Kukaribisha wageni nyumbani mwake kulimgarimu watoto wake
Kukosa viatu hata na karo hivyo kukosa kwenda shuleni kwa mwaka mzima)x2
(Alipenda wengine waokolewe Zaidi ya kustarehe mwenyewe
Hivyo alijitolea kwa hali na mali ili wengine wapate Amani)x2
(Hakupenda kutendewa makuu na watu Zaidi ya kumtumikia Mungu
Alihimiza watu kujenga makanisa mwenyewe kawa kielelezo)
(Maombi yalikuwa nguzo kuu yake kwa ajili ya kanisa
Waumini walijua kwa maombi ya mwenye haki wao wako salama)
(Basi wakati singenitosha kuwaleteeni habari zote za matendo makuu
Aliyekuwepo aliyepo na atakayekuwepoo matendo makuu kwa kweli yamgusa)
Upendo wake Mwanzilishi ni nani hajauona
(Tulikuwa hatufai lakini kwa upendo wake Mwanzilishi
Katupatia neno la faraja sasa twaweza faa)
(Maovu yalitutenga mbali na upendo wake Mwanzilishi
Bali katuombea hata kwa kufunga Mungu katurehemu)
(Tulichukiana na dharau tele wivu manung’uniko
Lakini kwa upendo na Amani yake tunaheshimiana)
Upendo wake Mwanzilishi ni nani hajauona
Pongezi mama mwanzilishi kwa unyenyekevu
Na uvumilivu wako kuhesabu wengine bora x2
(Baba mwanzilishi wa Imani na viongozi wengine tuu
Uliwapatia mahali pa kazi ulionyesha upendo na unyenyekevu mama
Mama ee pongezi ewe mama)
(Penye jua pasi kivuli mavumbini na matopeni penye mazingira duni
Ndipo ulitia bidii kuifanya kazi ya Mungu pasi na kuchoka
Mama mema sasa tunayaona)
(Hukujitakia makuu kuwa nayo ofisi ukawahudumia watu wa tabaka mbalimbali
Penye udhaifu pamejitokeza utukufu
Mama ofisi uko nayo)
(Enzi yake mtumishi Imanueli Mungu wako pamoja nasi ni yupi kama si wako
Ametufariji atakufariji nawe ili ufanye kazi ya Mungu kwa furaha)
(Aah pongezi mama mwanzilishi kujipa moyo kufanya kazi hii japo kwenye mazingira magumu, kwenye jua mavumbini na matopeni,hukuchoka kamwe kuwahudumia watu wa tabaka mbalimbali,hongera mama mwanzilishi.)
Asante Yesu kumuwezesha mama mwanzilishi kuvumilia
(Japo palikuwepo na changamoto nyingi Mungu wako mama > hakukuacha,kamwe)
(Ukawafundisha watu wokovu kuimarika ni upendo ule wa kwanza > chanzo chake, kushangaa)
(Baada ya kuimarika kawafundisha kuinuliwa kwa njia ya Baraka > kumtolea,Mungu)
(Ulitekeleza haya yote pasi ofisi juhudi zako mama > haziwezi,linganishwa)
(Asante Yesu kumuwezesha mama mwanzilishi kuvumilia….)
(Mama mwanzilishi tunakupongeza kwa upendo mwingi katika kutuongoza)
Mama mwanzilishi ( ooh mama) tunakupongeza(tunakupongeza) kwa upendo mwingi katika kutuongoza x2
(Umetulea) umetulea (kwa Imani) kwa Imani
(Zaidi ya miaka) hamsini na mitano x2
Twakupenda,twakupenda, sote twakupenda ..(twakupenda x3 sote twakupenda)
Tanzania,na Uganda,hata Kenya yote..(twakupenda x3 sote twakupenda)
Ni mengi mama,Umetenda,sote twayaona..(twakupenda x3 sote twakupenda)
Twakupenda,kanisa lakupenda,twakupenda..(twakupenda x3 sote twakupenda)
Oh twakupenda,twakupenda> mama,twakupenda..(twakupenda x3 sote twakupenda).
(Nikitafakari upendo wake Bwana Yesu
Najikuta nimefika upeo wa mawazo
Nikizichunguza na rehema zake nyingi
Hapo ndipo ninakoma bila jawabu)x2
(Nikupe nini (nikupe nini Bwana)
Nikupe nini
Nikupe nini Bwana kwa rehema zako) x2
Nikupe nini ila kukushukuru
(Ulimchagua mtumishi wako Elisha
Ukampa kanisa na pia maongozi
Yatakayofaa katika maisha yangu
Hayo yote sikulipa hata garama)x2
(Mwanzilishi kajitolea na nyumba yake
Aliteseka sana na hata kufedheheshwa
Lakini ukampa sana uvumilivu
Umenirehemu si kwa wema wangu)x2
( Nikupe nini Mungu wa mama mwanzilishi
Umetulinda zadi ya miaka hamsini na mitano
Hakika wema wako kwetu leo tunauona)
(Ni mbali sana) ni mbali sana tumetoka (mahali tumefika) na mahali tumefika
(si kwa wema wetu)Sio kwamba tuwema (bali ni kwa rehema)bali ni kwa rehema zako
(Rehema zako) rehema zako Bwana (zanitunza mimi)zanitunza kila siku (nipe kuzitubu) nipe kutubu dhambi(nikashinde maovu) nikayashinde maovu)x2
(kuzitubu dhambi) nipe kutubu dhambi(nikashinde maovu) nikayashinde maovu
(katika kutoa) nipe kukutolea(nikapate baraka) nikapate Baraka
(kwa kusikiliza)nipe kusikiliza(nikapate Imani) nikapate Imani
(Maana mimi) (nimeokolewa kwa neemax2)x2
(Rehema zako Bwana)( nimeokolewa kwa neemax2)x2
(Ni mbali sana) ni mbali sana tumetoka (mahali tumefika) na mahali tumefika
(si kwa wema wetu)Sio kwamba tuwema (bali ni kwa rehema)bali ni kwa rehema zako x2
Mungu wetu ndiwe mtukufu na umkamilifu muweza
Mapenzi yako yatendeke unapoongoza kanisa
Ewe Mungu (sikia) tunakulilia tuongoze(Bwana) kwenye njia ya kweli
Tunamuombea kiongozi atawaliwe na roho wako
Kampe na uwezo wako ujasiri hekima yako
Na wazee wa kanisa hili wajaze nguvu zako ee Mungu
Waimbaji na waumini tuongozwe na roho wako
Tuna waombea wahubiri watangaze injili kwa moyo
Na wasio kujua Mungu wavutwe kwako waokoke
Imani ya miujiza na uvivio yasonga mbele
Hatuwezi kurudi nyuma wala hata kukata tamaa
Bali sote kwa nia moja tutazidi kusonga mbele
Ni sauti kutoka kwa Mungu kamjia mzee Elisha
Na kumwambia toka nchi yako hadi nchi ile ya ugeni
Nitakufanya uwe taifa kubwa kukubariki kulikuza jina lako
Na wewe uwe Baraka na wewe uwe Baraka
Na huyo mteule wa Mungu akasafiri nchi ile ya ugeni
Kwenye jangwa na tabu nyingi hapo ndipo alipotumwa
Chini ya mti injili ilianza kwa makofi na tenzi za rohoni
Utukufu wa Mungu ulishuka utukufu wa Mungu ulishuka
Na zamu yake ilipoisha Mungu wake hakutuacha
Lisimamisha mjumbe wake na akampa na ujasiri
Na injili sote tulisikia ya kwamba sisi ni mabalozi
Twawakilisha ufalme wake twawakilisha ufalme wake
Na zamu yake ilipoisha Mungu wake libaki nasi
Kwa kumwinua mchungaji wake mwenye hekima na ujasiri
Nayo injili pia tulisikia kitufundisha kizuizi cha mema
Tulifahamu tukaokoka tulifahamu tukaokoka
Haya yote yalitendeka kwa maongozi ya mama mwanzilishi
Aliyesimama kwa kazi hii yeye ni shujaa wa Imani kweli
Wasia wake twaukumbuka mioyoni mwetu umebakia
Mama mlezi siye mfano mama mlezi siye mfano
Na sasa Mungu twakushukuru kutuinulia mtumishi wako
Mnyenyekevu ndiye Imanueli yani ni Mungu pamoja nasi
Na Kama Petro sote twasema (tuende wapi na hapa ndipo)
Kwenye maneno yale ya uzima (kwenye maneno yale ya uzima)
(Sote kwa nia moja )x2--- tutazidi kusonga mbele
(Hata na wanakwaya) (katika kumsifu)
(Hata na wahubiri), (kueneza injili)
(Hata na washirika) ( katika utumishi)
(Kujenga makanisa)
(Sote kwa nia moja) (sote kwa nia moja)
(Tutunze Imani
Imani ya kweli Imani ile ya utakatifu)x2
(Imani ile ya kutubu dhambi hata kama dhambi ni kubwa sana
Uiungame na kuacha usirudie dhambi tena)x2
(Tutunze kutoa
Kutoa kwa kweli kutoa Mungu anavyokutuma)x2
(Kutoa mali kwa kazi ya Mungu zaka sadaka pia shukurani
Ubarikiwe kwa mapato ubarikiwe kazi yako)x2
Tutunze umoja
Umoja wa kweli umoja ule wa kukusanyika )x2
(Mmoja wetu asijaribiwe kufanywa mgumu katika dhambi
Ulete kwake muhubiri utaushinda ulimwengu)x2
(Tutunze kupona
Kupona kwa kweli kupona kule kwa jina la Yesu)x2
(Jina la Yesu laweza kuponya kwa kujitoa kwake tumepona
Utakasike na upone utayarike kwa mbinguni.)x3
Hubirini pande zote neno la Mungu watu wajue
(siri aliyofunuliwa) mtumishi wa Mungu x2
(ya kwamba)Watu wasumbuka maishani hakuna Amani
(dhiki huzuni) zimejaa mioyoni mwao x2
( Maana) watu hawa ni watu waasi(Watoto) watoto wasemao uongo
(wasiotaka) wasiotaka (kusikia)kusikia sheria za Bwana x2
Waambiao waonaji msione na manabii msitoe unabii wa mambo ya haki
Tuambieni maneno laini hubirini maneno yadanganyayo x2
( Maana) watu hawa ni watu waasi(Watoto) watoto wasemao uongo
(wasiotaka) wasiotaka (kusikia)kusikia sheria za Bwana x3
Hubirini pande zote neno la Mungu watu wajue
(siri aliyofunuliwa) mtumishi wa Mungu
Yatendeni mambo yote pasipo manung’uniko
Wala mashindano mpate kuwa wana wa Mungu x2x2
Msitende neno lolote kwa majivuno
Bali kila jambo kwa unyenyekevu
Kila mtu amuhesabu mwenziwe bora
Msiwe na lawama au hila yoyote x2
(Iweni na nia moja nia iyo hiyo idumu ndani yenu
ambayo ilikuwamo pia ilikuwamo ndani ya kristo Yesu)
Yatendeni mambo yote pasipo manung’uniko
Wala mashindano mpate kuwa wana wa Mungu
(U muhubiri wewe hubiri pasipo manung’uniko)
(U mwimbaji wewe imba pasipo manung’uniko)
(Ni sadaka yako wewe toa pasipo manung’uniko) x 2
(Yatendeni mambo yote pasipo manung’uniko) x2
(Nashangaa mimi najiuliza sipati jibu ninapolala ninani aniamsha
Mimi nashangaa tena najiuliza ninapotembea ni nani anilinda)
(ooh)
Huyu Mungu(huyu Mungu) atenda ya ajabu atuamsha atulinda hana mfano wake
(Huyu Mungu)
Huyu Mungu atenda ya ajabu atuamsha atulinda hana mfano wake
(hakuna kama yeye)
Huyu Mungu atenda ya ajabu atuamsha atulinda hana mfano wake
Mwanadamu nikimkosea asiponisamehe hakika Mungu yeye anisamehe
Majirani na marafiki waweza nikataa hakika Mungu hawezi nikataa
(ooh)
Huyu mungu atenda ya ajabu Atusamehe atuponya pia atubariki
(huyu Mungu)
Huyu mungu atenda ya ajabu Atusamehe atuponya pia atubariki
(hakuna kama yeye)
Huyu mungu atenda ya ajabu Atusamehe atuponya pia atubariki
Ni wa ajabu
Ni wa ajabu ewe Bwana ni wa ajabu
Baba wewe ni wa ajabux2
Masia wewe ni wa ajabux2
Umetenda mambo makuux2 maishani mwetu
Uzima na Amani umetupa x2 uinuliwe
Pokea sifa na utukufu
Wapendwa Mungu ametenda mambo makuu katika maisha yetu
Inua mikono yako juu na upige makofi
Bali kila anisikilizaye atakaa salama
naye atatulia bila kuogopa mabaya
(Bali kila anisikilizaye atakaa salama
naye atatulia bila kuogopa mabaya)
Atakaa salama ..atakaa salama
Anisilizaye bila kuogopa mabaya.. atakaa salama siku zote x2
Atoleaye Mungu bila kuogopa madeni.. atabarikiwa kwa mapato yake
Aungamaye dhambi bila kuona aibu.. atapona magonjwa yake yote
Yule atuliaye kwenye neno la Mungu.. ataka salama siku zote
Kwa Imani Musa alipokuwa mtu mzima-a
Alikataa kuitwa mwana wa binti Farao
Akaona vyema kuteseka pamoja na watu wa Mungu
( kuliko kujifurahisha katika dhambi kwa kitambo tuu x2) x2
Umelemewa ndugu na umasikini -----kwa sababu hujatoka nchi ya Farao
Umelemewa dada na hayo magonjwa
Umelemewa ndugu na roho ya wivu
Umelemewa dada na manung’uniko
(Musa na waisraeli, walitoka misri nchi ya farao wakaenda kwa mwendo wa siku tatu, ili kumwabudu na kumtumikia Mungu wao,nawe mpendwa, Mungu anakuagiza utoke kwa Farao,Farao ni ile roho mbaya na dhambi uliyonayo mpendwa,nawe ukitoka siku ya leo hakika Mungu huyu wa mwanzilishi atasikia maombi yako)
(Toka katika nchi ya Farao twende kanani tuliko ahidiwa)
Toka katika nchi ya Farao (twendeni)twende kanani tuliko ahidiwa
(Acha wivu mama )
Toka katika nchi ya Farao (twendeni)twende kanani tuliko ahidiwa
(Acha wivu dada )
Toka katika nchi ya Farao (twendeni wote)twende kanani tuliko ahidiwa
(Acha chuki baba)
Toka katika nchi ya Farao (twendeni)twende kanani tuliko ahidiwa
(Acha chuki mama)
Toka katika nchi ya Farao (twendeni wote)twende kanani tuliko ahidiwa
(Ndugu yangu mpendwa,umelemewa na madeni,na dhambi kwa siku nyingi, kwa sababu haujakubali kuhamishwa, katika nchi hiyo, kata shauri siku ya leo, naye hakika Mungu huyu wa mwanzilishi, atakufanya kuwa taifa kubwa,shangwe na vigelegele)
(Acha wivu dada)
Toka katika nchi ya Farao (twendeni)twende kanani tuliko ahidiwa
(Acha wivu mama)
Toka katika nchi ya Farao (twendeni wote)twende kanani tuliko ahidiwa
(Acha vita mama)
Toka katika nchi ya Farao (twendeni)twende kanani tuliko ahidiwa
(Acha vita ndugu)
Toka katika nchi ya Farao (twendeni wote)twende kanani tuliko ahidiwa
(Toka ewe baba)
Toka katika nchi ya Farao (twendeni)twende kanani tuliko ahidiwa
(Toka ewe mama )
Toka katika nchi ya Farao (twendeni wote)twende kanani tuliko ahidiwa
((Toka katika nchi ya Farao twende kanani tuliko ahidiwa))x2
(Ooh halleluya, sote tumshukuru Mungu, kwa wema wake
Ametupa uzima,ametupa Amani, ametuponya na magonjwa,nakutuondolea mambo mazito, shida zilizoshinda wenye uwezo na akili,wa dunia, lakini sisi kwa wema wa Mungu, tumeokolewa)
(Tunakushukuru ee Mungu kwa wema wako)
Tunakushukuru ee Mungu kwa wema wako
Tunakushukuru ee Mungu kwa wema wako Bwana
Umetupa Amani Bwana maishani mwetu
Umetusamehe na dhambi acha tukushukuru
Umetuponya magonjwa yaliyoshinda wengi
Umetuinua ee Bwana kutoka mavumbini
Ooh tunakushukuru ee Mungu kwa wema wako
Kenya Uganda Tanzania umetuunganisha
Umetupa umoja wakweli uliotuunganisha
Mayatima wameona Baraka zako Bwana
Hata wajane wameona Baraka zako Bwana
Familia zilotengana umeziunganisha
Wanandoa waloachana umewapatanisha
Tunakushukuru ee Mungu kwa wema wako
(Hee….na kama si Mungu kuturehemu akamwinua mwanzilishi wake na kumfunulia mema haya tunayoyaona hivi leo sote tusingelikua hapa hata hivi leo)
(Ooh acha tukushukuru) acha tukushukuru x2
(Umetupa Amani)
(Umetusamehe dhambi)
(Umetuponya magonjwa)
(Umetuinua Bwana)
(Umetufariji Bwana)
(Umetupa maisha mema)
(Umetubariki Bwana)
(Dunia yote yasema)
(Wewe ni Bwana wa wote)
(Umestahili sifa)
(Cha kukulipa hatuna)
(Ooh acha tukushukuru)x3
(Shangwe na vigelegele)
Ooh acha tukushukuru x11
All: Haki huinua taifa, bali dhambi ni aibu ya watu wowote
ili uweze kutenda haki, yakupasa uwe nao uaminifu x2
{
Solo: Kama vile Yusufu alivyokuwa mwanimifu
Kwa kumheshimu mke wake Potifa
Taifa lote la Misri likainuliwa
Halikupata njaa kwa usimamizi wa Yusufu
All: Haki huinua taifa, bali dhambi ni aibu ya watu wowote
ili uweze kutenda haki, yakupasa uwe nao uaminifu.
}x2
{
Solo: Bwana mmoja akawapa talanta watumishi wake
Akawaita akamwambia vyema, mtumwa mwema na mwaminfu,
Uliikuwa mwaminfu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi,
ingia katika furaha ya Bwana wako.
All: Haki huinua taifa, bali dhambi ni aibu ya watu wowote
ili uweze kutenda haki, yakupasa uwe nao uaminifu.
}x2
{
Solo: Haki ni neno jema kwa mwanadamu,
awaye yote, ni lazima atende haki,
kumbuka Anania na Safira walivyomtolea Mungu,
sadaka ya uongo nao wakaangamia.
All: Haki huinua taifa, bali dhambi ni aibu ya watu wowote
ili uweze kutenda haki, yakupasa uwe nao uaminifu
}x2
Break (instruments)
Solo: Uaminifu ni chemichemi ya haki, yakupasa uwe mwaminifu
All: usiogope dhiki unayopata-a, uwe mwaminifu hata kufa
Solo: Vita na uasi, chanzo chake eeh, ni ukosefu wa uaminifu
All: usiogope dhiki unayopata-a, uwe mwaminifu hata kufa
Solo: Ni kutubu, tubu dhambi eee , hata kama ni ya aibu namna gani
All: usiogope dhiki unayopata-a, uwe mwaminifu hata kufa
Solo: Ni kutoka tolea Mungu weee hata kama umpungufu namna Gani eeee
All: usiogope dhiki unayopata-a, uwe mwaminifu hata kufa
Solo: Ni kuomba muimbe Mungu wee! Wala ndugu usikate tamaa
All: usiogope dhiki unayopata-a, uwe mwaminifu hata kufa
Solo: Usiogope dhiki unayopata, uwe mwamnifu hata kufa
All: usiogope dhiki unayopata-a, uwe mwaminifu hata kufa
Solo: Bana usiogope
All: usiogope dhiki unayopata-a, uwe mwaminifu hata kufa
Solo: Mama usiogope
All: usiogope dhiki unayopata-a, uwe mwaminifu hata kufa
Solo: Wewe usiogope
All: usiogope dhiki unayopata-a, uwe mwaminifu hata kufa
(Instruments)
(Solo: wewe usiogope
All: usiogope dhiki unayopata-a, uwe mwaminifu hata kufa ) x3
Tnr Kuheshimu Mungu kuna faida, Kuheshimu Mungu kwafaa sana x2
Solo: [Heshima All: Yaweza kubadilisha hukumu yako
Solo: Heshima All: Yaweza kubadilisha kifungo chako
Solo: Heshima All: Yaweza kubadilisha utumwa wako
Solo: Na mambo All: Yakabalidilika ukawa huru]x2
2 solos: Watazame wale wevi waliosulubishwa na Yesu, mmoja wao alimdhihaki Mwokozi x2
All: Wewe uliokoa wengi, sasa jiokoe mwenyewe, hivyo hivyo utuokoe pia na sisi x2
2solos Lakini yule mmoja akajibu akamwambia wewe huogopi hata Mungu x2
All: Hukumu tunayoipata mwenzangu inastahilit kweli tuyapitiea mateso haya x2
Solo2 : [Kisha akasema ‘Eh Yesu unikumbuke utapokuwa katika ufalme wako,
Yesu akajibu amini nakuambia
2 solo Hivi leo utakuwa pamoja nami peponi] x2
Solo: [Heshima All: Yaweza kubadilisha hukumu yako
Solo: Heshima All: Yaweza kubadilisha kifungo chako
Solo: Heshima All: Yaweza kubadilisha utumwa wako
Solo: Na mambo All: Yakabalidilika ukawa huru]x2
Solo1: Japo alikuwa ni mwivi sana, lakini akaogopa Mungu akiwa msalabani, alipata msamaha, hapo hapo akaingia mbinguni kwa Baba Mungu, mbinguni….
All: kwa kumheshimu Mungu
Solo1: Hata Rahabu yule kahaba alipowahifadhi, wale wapelelezi wa nchi, alipata na fadhili, yeye na jamaa zake hawakuangamizwa kwa moto..
All: kwa kumheshimu Mungu
Solo1: Hata uwapo na dhambi wewe, yakupasa umwogope Mungu naye atakuokoa, utapata msamaha nawe utakuwa huru katika maisha yako, siku zote
All: kwa kumheshimu Mungu
Solo: [Heshima All: Yaweza kubadilisha hukumu yako
Solo: Heshima All: Yaweza kubadilisha kifungo chako
Solo: Heshima All: Yaweza kubadilisha utumwa wako
Solo: Na mambo All: Yakabalidilika ukawa huru]x2
Tnr Kuheshimu Mungu kuna faida, Kuheshimu Mungu kwafaa sana
1. Yesu akwita ewe ndugu yangu, atakata uje kwake,
anakungojea umkubali, naye akupokee x2
2. Na usifanye moyo mgumu, anapoita Yesu,
ujapokosa wewe umwendee naye akupokee
3. Yesu anao wokovu kamili, wa mwili na wa roho,
nimfariji na huruma nyingi, naye akupokee
solo
Njoo kwake leo, na yote matatizo nawe ukimwamini, atakuweka huru
Njoo kwake leo, lete matatizo nawe ukimwamini, atakuweka huru
Njoo uliyelemewa na mizigo ya dhambi itue kwake Yesu ili upumzishwe
Dhambi yako ni nyekundu hata iwe kama damu Yesu ataitakasa iwe kama theluji
Umeenda kwa waganga, hukupata uzima mtumainie Yesu akupe uzima
Umaskini na madeni vimekuponza moyo, mtumainie Yesu mwenye mali zote
Manyanyaso maonevu maadui wamekupangia, mtumainie Yesu baba mwenye upendo
Dhiki nayo misiba imekudhoofisha mtumainie Yesu yeye ni mfariji
Nawe ukimwamini atakuweka huru
Nawe ukimwamini atakuweka huru
Lete hayo magonjwa yaloshinda waganga
Lete umaskini ulokuponza moyo
Mizigo mizito ya dhambi itue kwake Yesu
Dhiki na misiba Yesu ni Mfariji
Dhambi nzito ulotenda ilete Kwake Yesu
Nawe uki, nawe uki, nawe ukimwanini
Ewe dada
Ewe ndugu
Ewe baba
Ewe mama
Ewe mzee
Nawe uki, nawe uki, nawe ukimwamini
1. Wakati wa siku ya kwanza ya juma, wanafunzi kumi na mmoja walijifungia kwa hofu ndipo Yesu mwokozi akawatokea
(Chorus)
Yeye anipendaye nitajidhihirisha kwake, mimi nitajidhihirisha x2
2. Simoni, Nathanaeli na Thomaso, na hao wana wa Zebedayo wakesha kuvua samaki, ndipo Yesu mwokozi, akawatokea.
3. Waheri wote wale wasadikio kwamba mwokozi kafufuka kutoka katika mauti ndipo Yesu mwokozi atawafufua.
1. Ni furaha mbinguni na hata duniani amefufuka yeye ndiye Yesu mwokozi shujaa ni Yesu Kristo.
(Chorus)
Tuimbe kwa furaha leo amefufuka amekaa mkono wa kuume wa Mungu naye atuombea sote.
2. Na alipofufuka kaambia wanafunzi msifadhaike niko pamoja nanyi amani na iwe kwenu.
3. Nasi tuwe hodari katika majaribu tusiwe na hofu wala tusiogope na yote tutayashinda.
1. Itazame hio misumari inavyopenya ndani ya viganja, itazame hiyo misumari inavyopenya ndani ya miguu yake Bwana Yesu.
(Chorus)
Ni uuuu uuuchungu mwingi Yesu aliteswa sana sababu ya dhambi zetu tupate kuokolewa.
2. Itazame taji ya miiba inavyowekwa juu ya kichwa, itazame hio mijeledi inavyopigwa juu ya mwili wake Bwana Yesu.
1. Mwokozi amefufuka kutoka yale mauti ( Yesu ameshafufuka ametoka kaburini) yu kwenye kiti cha enzi.
(Chorus)
Yesu amefufuka kutoka mauti (kifo na kaburi, mauti) ameshinda.
2. Maria magdalena alikwenda kwenye kaburi (alikuta lile jiwe limekwisha ondolewa) na Yesu amefufuka.
3. Thomaso hakuamini habari za ufufu (Yesu akamtokea akaziona alama) mbavuni na mikononi.
4. Na wewe ukiamini habari za ufufuo (Yesu atakufufua atakapo kuja tena) kuishi nawe milele.
1. Kilima cha Goligotha kando ya Mwokozi Bwana Yesu tazama ameuawa damu yabubujika (tayari kuosha makosa x2)
2. Kwa kuwa makuhani wamefanya shauri kwamba asulubiwe auwawe kwenye mti huyo mwana wa Mungu (aonje uchungu wa kifo x2).
3. Na wewe wataka nani wamtaka Baraba kwamba asulubiwe chagua Yesu Kristo ndiye Mwana wa Mungu (upate wako msamaha x3)
1. Mungu mkamilifu muumba mbingu na nchi na vilivyomo ahadi zake ni kweli halleluya halleluya ndiye mwanzo na pia mwisho.
2. Mungu mkamilifu na mwenye huruma kamtoa mwanawe kwa ajili yetu sisi halleluya halleluya kamtakasa mwanadamu.
3. Mungu mkamilifu mkweli ahadi ya wokovu kwa wote waaminio wapate halleluya halleluya waende kwake juu mbinguni.
4. Mungu mkamilifu muweza ameanza kazi njema kwako ndiye mkuu mtukuze halleluya halleluya atalitimiliza kwako.
1. Bwana Yesu alisema nitalivunja na kulijenga kwa siku tatu x2
(Chorus)
Kanisani mwili wako ni uwe mtakatifu x2
2. Yesu alimaansha atakufa na kuzikwa na afufuke siku ya tatu x2
1. Mungu ndiye wa kwanza kuonyesha pendo kamtoa mwanawe aje ulimwenguni afe msalabani kwa ajili ya dhambi zetu wanadamu.
(Chorus)
Halleluya twaimba kwa kuwa atupenda tumepata wokovu na uzima milele
2. Yesu alionyesha pendo kwa wanafunzi kawaosha miguu kisha kawaambia imewapasa ninyi kutembea na haya mpendane wenyewe.
3. Kwa sababu ya pendo kashinda mauti kaupata uzima naye anatuambia tuwapende wenzetu tuyashinde mauti tupate uzima
4. Wewe unayesema uko katika nuru na wachukia ndugu ambaye wamuona utapendaje Mungu ambaye humuoni wakaa gizani
1. (Ni furaha kubwa) Duniani kote (Kwa kuikumbuka) siku ya krismasi x2
(Chorus)
Mwokozi Yesu amezaliwa katika mji Bethilehemu walimlaza katika hori nafasi nzuri hawakupata
2. (Hata wachungaji) kule makondeni (walifurahia) kuzaliwa kwake x2
3. (Pia mamajusi) kule mashariki (walifurahia) kuzaliwa kwake x2
1. Uwe hodari wa moyo, na pia ushujaa mwingi
Hapatakuwa na mtu, mbele yako maishani
Utende kama alivyo kuagiza mwanzilishi
Mimi bwana nikuamuru
Ee Joshua usiache enda mbele
Mtumishi usiache enda mbele
Na wachache uliowapata, wenye hofu watupie mbali
Maana mimi Mungu sipendezwi naye
Mtu wakusitasita.×2
2. Mimi ni pamoja nawe kuwaongoza watu hawa
Watafuata popote kulia hata kushoto
Nami nikufanikishe wairithi nchi hiyo
(Chorus)
Mimi bwana nimeahidi
Ee Joshua usiache enda mbele
Mtumishi usiache enda mbele
Na wachache uliowapata, wenye hofu watupie mbali
Maana mimi Mungu sipendezwi naye
Mtu wakusitasita ×3
1. Mwana kondoo aongozwa kuelekea machinjoni ya sadaka.
(Chorus)
Huzuni x3 nyingi, walimpiga kwa husuda japo hakuwa na makosa
2. Mateso mengi alipata wala sauti ya uchungu hakutoa.
3. Pasipo damu kumwagika hakuna huo msamaha wa makosa.
1. (Yesu namwona mtini) aliuawa msalabani (afa kwa dhambi za watu) kwa sababu ya dhambi zetu x2
Eee Mungu wangu naomba unikumbuke kwenye maisha ya milele
Aliuawa msalabani kwa sababu ya dhambi zetu.
2. (Yesu alia Eloi) Alilia Elo Eloi (lamasabachthani)Mungu mbona umeniacha x2
Eee Mungu wangu mbona umeniacha kwenye mikono ya wenye dhambi x2
Aliia Elo Eloi Mungu mbona umeniacha. x2
3. (Yesu aishi yu hai ) Kaburini Yesu hayuko (ameyashinda mauti) kwa sababu amefufuka x2
Atatutoa kwenye haya mauti tuliyonayo siku akija x2
Kaburini Yesu hayuko kwa sababu amefufuka x3
1. Tazama zake bwana Yesu mikononi miguuni na mbavuni upendo wa ajabu.
(Chorus)
Dhambi zote zimelipwa na bwana Yesu jipe moyo sifadhaike sasa.
2. Je wewe ni dhambi gani kubwa sana waiona umetenda ni nyekundu haina msamaha.
3. Pokea upendo wake bwana Yesu zitumie dhambi zako uziache upate msamaha.
1. Nipakumbukapo pale Gehtisemane naona huzuni nyingi (kiniepuke) ( baba) ila yote yawe mapenzi yako hoo
(Chorus)
Mateso mengi mwokozi walimtesa msalabani mwokozi alikufa na akasema ee Baba uwasamehe ili dhambi zote zifutiliwe
2. Nitafakaripo yake mateso hayo naona huzuni nyingi (imekwisha) (baba) wasamehe hawajui watendalo.
3. Alipofufuka bwana mwokozi Yesu akawa na ishara nyingi (wakasema) (kweli) huyu alikuwa ni mwana wa Mungu
1. Je rafiki unamtafuta nani kaburini Yesu hayuko ameshafufuka x2
(Chorus)
Sanda ziko hizo ni nguo zake (lakini mwili wake umekwisha fufuka x2)
2. Bwana Yesu anapatikana katika maisha ya mtumishi aliyemtuma x2
3. Wana heri wote wamtafutao bwana Yesu watamuona kwenye neno lake x2
1. Kwa maana jinsi hii Mungu alitupenda kamtoa mwanawe tupate wokovu
(Chorus)
Amwaminiye mwana hatatayarika, atapata uzima ule wa milele (asema) asema bwana.
2. Kwa moyo uamini uhesabiwe haki na kwa kinywa ukiri uupate wokovu
3. Ndugu amini mwana uhesabiwe haki ukiri jina lake uupate wokovu.
1. Bwana Yesu leo amefufuka kutoka mauitini kifo na dhambi vimeshashindwa sasa bwana yu hai.
(Choru)
(Tutai)ishi naye (tukisha)ngilia pamoja milele mbinguni tutaishi na mwokozi.
2. Alipoangikwa msalabani alisema imekwisha uzima kwake tumeupata sasa bwana yu hai.
3. Kuteswa kwake bwana mwokozi kulileta wokovu tu huru katika damu yake sasa bwaa yu hai.
1. MIe kaburini, Yesu Mwokozi!
Alilazwa chini, Bwana wangu!
(Chorus)
Bwana amefufuka! Kifo kimeshindwa kabisa
Gizani mle alitoka chini, sasa atawala huko mbinguni
Yu hal! Yu hai! Bwana Yesu yu hai
2. Walinda kaburini, Yesu Mwokozi
Bure ni muhuri, Bwana wangu
3. Auugoja huo, Yesu Mwokozi
Mchana ujao, Bwana wangu.
4. Kifo kimeshindwa, Yesu Mwokozi
Pingu zimevunjwa, Bwana wangu.
1. (Hata walipokwisha kuomba alitwaa wanafunzi, wakaenda mpaka mlima ule mizeituni)
Ili kuomba pamoja mara akajitenga kando x2
Hapo akafadhaika kwa huzuni nyingi akaomba kimwepuke bali mapenzi ya Mungu x2
2. (Ndipo kawarudia mahali pale alipowaacha akawakuta wote usingizi ni mzito sana
Mbona sasa mnalala hamuwezi kwa saa moja x2
Ombeni ili msije jaridbiwa sasa kwani roho iko radhi bali mwili ni dhaifu. x3
1. Shinani mwake Yesse latimia tabirio mwanawake Mungu kweli amekwisha zaliwa
(Chorus)
(Ulimwengu) ni shangwe (Mkombozi) kazaliwa kaja ili kuokoa. x2
2. Mamajusi nao wachunga waongozwa nayo nyota wakienda Bethilehemu ili kumsujudu.
3. Ee ndugu umeshatambua kuwa hori roho yako isafishe hivi leo ili akazaliwe.
1. Yesu wewe ndiwe uliyeimwaga damu takatifu watoa mwili sadaka kamili.
(Chorus)
Ewe Yesu mpole mwenye huruma tele nisikie uitakase sana iwe nawe peponi roho yangu unikumbuuke bwana uwapo paradiso nakuomba.
2. Mimi ninaionda hofu kubwa kiza kuu sana kazi ya haki yakushuhudia
3. Maafa kati ya misalaba miwili kama mwenye dhambi uwe kwetu dhabihu kamili
1. Mukama wafe yesu yemurunji ye mwangu okukuwonya leta ebizibu vyovyona ye ajewo:
Terie e dagala Dala eriendwade omusai gwa yesu gegwonya. x2
2. Olwecho seluganda hurira ainza kukuonya akusanyie ebibivyo,obere momirembe jona,.
1. Baba, Mwana, Roho, Mungu mwenye enzi,
Kila tukiamka tunakuabudu,
Baba, Mwana, Roho, Mungu wa mapenzi,
Ewe Utatu, tunakusifu.
2. Baba, Mwana, Roho, wakuaminio,
Wanakutolea shukrani zao,
Wanakusujudia malaika nao,
Wewe u mwanzo, nawe u mwisho.
3. Baba, Mwana, Roho, sisi tu gizani,
Utukufu wako hatuoni kosa,
U Mtakatifu, nawe u mapenzi,
U peke yako, mwenzio huna.
4. Baba, Mwana, Roho, Mungu mwenye enzi,
Ulivyoviumba vyote vyakusifu:
Baba, Mwana, Roho, Mungu wa mapenzi
Ewe Utatu, tunakusifu.
1. Bwana Mungu nashangaa kabisa,
Nikifikiri jinsi ulivyo,
Nyota, ngurumo, vitu vyote pia,
Viumbavyo kwa uwezo wako.
(Chorus)
Roho yangu na ikuimbie,
Jinsi wewe ulivyo mkuu,
Roho yangu na ikuimbie,
Jinsi wewe ulivyo mkuu.
2. Nikitembea pote duniani,
Ndege huimba nawasikia,
Milima hupendeza macho sana,
Upepo nao nafurahia.
3. Nikikumbuka vile wewe Mungu,
Ulivyompeleka mwanao,
Afe azichukue dhambi zetu,
Kuyatambua ni vigumu mno.
4. Yesu Mwokozi atakaporudi,
Kunichukua kwenda mbinguni,
Nitaimba sifa zako milele,
Wote wajue jinsi ulivyo.
1. Damu Imebubujika, ni ya Imanweli,
Wakioga wenye taka, husafiwa kweli.
2. Ilimpa kushukuru mwivi mautini;
Nami nisiye udhuru, yanisafi ndani.
3. Kondoo wa kuuawa, damu ina nguvu,
Wako wote kuokoa, kwa utimilivu.
4. Bwana tangu damu yako Kunisafi kale,
Nimeimba sifa zako; taimba milele.
5. Nikifa tazidi kwimba sifa za wokovu
Ulimi ujaponyamaa vumbini mwa ufu.
6. Bwana, umenikirimu nisiyestahili
Kwa damu yako, sehemu ya mali ya kweli.
7. Nikubali kukwimbia, mbinguni milele,
Mungu nitakusifia Jina lako pweke.
1. Ewe Roho wa Mbinguni
Uje kwetu sasa.
Ufanye makazi yako
Ndani ya Kanisa.
2. Ndiwe mwanga, umulike
Tupate jikana;
Mengi kwetu yapunguka,
Tujalize, Bwana.
3. Ndiwe Moto, teketeza
Taka zetu zote:
Moyo na iwe sadaka
Ya Mwokozi, yote.
4. Ndiwe Umande, na kwako
Tutaburudika,
Nchi kavu itakuwa
Ni yenye Baraka.
5. Roho wa Mbinguni uwe
Nasi hapa chini,
Mwili uufananishe
Na kichwa Mbinguni.
1. Jina lake Yesu tamu;
Tukilisikia
Hutupoza, tena hamu
Hutuondolea.
2. Roho iliyoumia
Kwalo hutibika,
Chakula, njaani pia;
Raha, tukichoka.
3. Jina hili ni msingi,
Ngao, ngome, mwamba,
Kwa hili napata wingi,
Kwangu ni akiba.
4. Yesu, Mchunga, Rafiki
Mwalimu, Kuhani,
Mwanzo, Mwisho, Njia, Haki,
Uzima kifoni.
5. Moyo wangu hauwezi,
Kukusifu kweli,
Ila sifa zangu hizi,
Bwana zikubali.
6. Na utakaponiita,
Kuja kwako Bwana,
Huko kwako sitaacha
Kukusifu sana.
1. Nasikia kwitwa
Na sauti yako
Nikasafiwe kwa damu
Ya kwangikwa kwako.
(Chorus)
Nimesogea Mtini pako,
Unisafi kwa damu ya kwangikwa kwako.
2. Ni mnuonge kweli,
Umenipa nguvu,
Ulivyonisafi taka,
Ni utimilivu.
3. Yesu hunijuvya;
Mapenzi, imani;
Tumai, amani, radhi,
Hapa na Mbinguni.
4. Huipa imara,
Kazi yake, ndani:
Huongezeka neema,
Ashindwe Shetani.
5. Huishuhudia,
Myoyo ya imani
Ya kuzipata ahadi,
Wakimuamini.
6. Napata wokovu,
Wema na neema;
kwako Bwana nina nguvu
Na haki daima.
1. Ndiyo dhamana, Yesu wangu;
Hunipa furaha za Mbingu;
Mrithi wa wokovu wake
Nimezawa kwa Roho yake.
(Chorus)
Habari njema, raha yangu
Yesu ndiye Mwokozi wangu,
Habari njema, raha yangu
Yesu ndiye mwokozi wangu.
4. Kumsalimu moyo wangu,
Mara namwona raha yangu;
Aniletea malaika,
Wananilinda, taokoka.
5. Sina Kinyume, nashukuru,
Mchana kutwa huja kwangu;
Usiku kucha kuna nuru;
Mwokozi wangu; ndimi huru.
6. Hali na mali anitwaa!
Mara namwona anifaa,
Nami nangoja kwa subira;
Akiniita, nije mara.
1. Nitwae hivi nilivyo,
Umemwaga damu yako,
Nawe ulivyoniita,
Bwana Yesu,naja,naja.
2. Hivi nilivyo si langu
Kujiosha roho yangu;
Nisamehe dhambi zangu,
Bwana Yesu,naja,naja.
3. Hivi nilivyo sioni
Kamwe furaha moyoni;
Daima ni mashakani,
Bwana Yesu,naja,naja.
4. Hivi nilivyo kipofu,
maskini na mpungufu;
Wewe u mtimilifu;
Bwana Yesu,naja,naja.
5. Nawe hivi utanitwaa;
Nisithubutu kukawa,
Na wewe hutanikataa,
Bwana Yesu,naja,naja.
6. Hivi nilivyo mapenzi
Yamenipa njia wazi;
Hali na mali sisazi,
Bwana Yesu,naja,naja
1. Tafuta daima utakatifu;
Fanya urafiki na Wakristo tu;
Nena siku zote na Bwana wako,
Baraka uombe kwa kila jambo. x2
2. Tafuta daima utakatifu;
Uwe peke yako ukimwabudu;
Ukimwangalia mwokozi wako,
Utabadilishwa kama alivyo. x2
3. Tafuta daima utakatifu;
Kiongozi wako awe Yesu tu;
Katika furaha au huzuni
Dumu kumfuata Yesu Mwokozi. x2
4. Tafuta daima utakatifu;
Umtawaze Roho moyoni mwako;
Akikuongoza katika haki,
Hufanywa tayari kwa kazi yake. x2
1. Mkamilifu ni Mungu wetu
Mtukufu ndiye Bwana wetu
(Ndiye Mungu, tena Bwana wa yote, ulimwenguni.) x2
(Chorus -1)
Katuletea Bwana Yesu
Kazaliwa kwenye kihori
Tumpokee Bwana Yesu, Tuokoke x2
2. Ukimwamini huyu Jehova
Pia utamwamini na mwana
(Atukuwa, Bwana katika maisha yako yote) x2
(Chorus -2)
Ukiomba kwa jina lake
Yeye mwana atatimiza
Amepewa uwezo toka kwake Mungu x2
3. Kazi aliyoanzisha Mungu
Hakikisha haiharibiki
(Tudumishe, umoja kanisani, twendeni mbele) x2
(Chorus -3)
Tushikane pamoja sote
Tumheshimu kiongozi
Aliyewekwa mbele zetu naye Mungu. x2
1. Yesu alilia msalabani
Kwa huzuni kweli na kufadhaika
Kwa ajili yetu sisi wanadamu
Dhambi zetu kweli zilimsulubisha
(Chorus)
(Aliteswa) Aliteswa, (Bwana Yesu) Bwana Yesu
Alipigiliwa msalabani, (misumari) misumari, (mijeledi) mijeledi
Aliteswa kwa ajili yetu sisi
2. Makuhani walimshika bwana Yesu
Wakampeleka mbele ya pilato
Kusudi la kumwangamiza bwana Yesu
Walimtungia mambo ya uongo
3. Ndugu yangu, dhambi zako unazofanya
Unamregesha bwana mautini
Tubu leo atukuke moyoni mwako
Atakufanya kuwa kiumbe kipya.
Bwana Yesu alikwenda
Pale Gethsemani
Pamoja na Petero,
Yakobo, Yohana
Akajitenga na wao, kaomba kwa baba yake
Kikombe kimuepuke.
Bwana akahangaika, pia kafadhaika
Akawa na huzuni kiasi cha kufa.
Yule Yuda msaliti akambusu bwana
Akakamatwa bwana, kweli huzuni kubwa
Wakampeleka bwana, mbele ya huyo pilato
Apate kuhukumiwa
Harusi duniani ni tatu
Ya kwanza kuzaliwa ya pili ni ndoa
Ya tatu ni nimuhimu japo ni ya huzuni kwetu
Hivyo kwa harusi hii takasa roho yako
Ukapokee Yesu katika roho Yako.
Nawe utafika kwa Mungu muumba wako
U si ku wa ma na ne*
s s m m m m f
m m d d d d r
d d s s s s t
d d d d d d t
*Ye su a li po za li wa*
s s s s l s f m
m m m m f m r d
d. d d d r d t l
d d d d r d t l
*Be thi le he mu*
r d t l s
t l s f m
s f m d d
s f m d d
*Ma ri a mu na Yu su fu*
s s m m m m f s'
m m d d d d r m'
d d s s s s t d'
d d d d d d t d
*Wa li fu ra hi ku m pa ta*
s' s ' s ' l ' s' f m r d
m' m' m' f' m ' r d t l
d d d r d t l f f
d d d. r d t l t f
U si ku wa ma na ne*
s s m m m m f
m m d d d d r
d d s s s s t
d d d d d d t
*Ye su a li po za li wa*
s s s s l s f m
m m m m f m r d
d. d d d r d t l
d d d d r d t l
*Be thi le he mu*
r d t l s
t l s f m
s f m d d
s f m d d
*Ma ri a mu na Yu su fu*
s s m m m m f s'
m m d d d d r m'
d d s s s s t d'
d d d d d d t d
*Wa li fu ra hi ku m pa ta*
s' s ' s ' l ' s' f m r d
m' m' m' f' m ' r d t l
d d d r d t l f f
d d d. r d t l t f
testtest
testtest